Ngongo
JF-Expert Member
- Sep 20, 2008
- 18,917
- 31,157
SI mara nyingi viongozi walioshika nyadhifa za juu katika Tanzania huamua kuandika vitabu vinavyoelezea maisha yao binafsi na ya utumishi wa umma wakati wanapostaafu.
Kwa sababu ya kasoro hiyo, baadhi ya mambo ya kihistoria waliyoyatenda wakati wa utumishi wao, hayafahamika kwa vijana wengi wa leo.
Pengine ni kwa sababu hiyo, mmoja wa viongozi hao wa zamani ambaye alipata kuwa Gavana wa kwanza wa Benki Kuu Tanzania na Waziri wa Fedha na Mipango, Edwin Mtei, aliona busara ya kuandika kitabu kinachoelezea maisha yake.
Kitabu hicho, kinachoitwa From Goatherd to Governor, kilizinduliwa Jumanne ya wiki iliyopita mjini Dare es Salaam katika sherehe fupi iliyohudhuriwa pia na watu kadhaa maarufu nchini.
Mmoja wa wazungumzaji katika hafla hiyo alikuwa mwandishi na mchapishaji wa vitabu nchini, Walter Bbgoya wa kampuni ya uchapishaji ya Mkuki na Nyota. Yeye hakutaka kuwa mnafiki mbele ya Mtei.
Akizungumza kwenye uzinduzi wa kitabu hicho From Goatherd to Governor (kutoka kuwa mchunga mbuzi hadi kuwa gavana) kwenye ukumbi wa British Council, Dar es Salaam, Bbgoya alisema kwamba alikuwa mmoja wa watu waliokuwa upande wa Mwalimu Nyerere alipotofautiana naye kuhusu sera za uchumi.
Bbgoya, ambaye sasa ni mmoja wa wanafamilia ya Mtei (kutokana na watoto wao kuoana), alisema wakati huo aliungana na msimamo wa Mwalimu na kukubaliana naye kwamba mashirika ya fedha ya kimataifa yalikuwa yanataka kuiburuza Tanzania.
Hata hivyo, alimsifu kwa kuwa na ujasiri usiokuwa wa kawaida wa kukisimamia kile alichokuwa akikiamini licha ya kupingwa na Mwalimu hivyo kuwasilisha yeye binafsi barua ya kujiuzulu kwa kiongozi huyo wa nchi.
Hata Mwenyekiti wa Bodi ya Uhariri ya gazeti hili, Jenerali Ulimwengu alipopewa nafasi ya kuzungumza, pamoja na mambo mengine, alimsifu Mtei kwa kulieza kwa ufasaha mkubwa tukio la kujiuzulu kwake uwaziri baada ya kutofautiana na Mwalimu mapema Desemba, 1979.
Aliyekuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Ibrahim Kaduma, ambaye alifanya kazi na Mtei katika Wizara ya Fedha, alimsifu Mtei kwa uzalendo aliokuwa nao wakati wote alipokuwa mtumishi wa umma.
Alisema kwamba mambo mengi leo yanakwenda ovyo kwa sababu watu hawaweki uzalendo mbele kama walivyokuwa wanafanya watu wa aina ya Mtei walipokuwa serikalini.
Alitoa mfano wa ujenzi wa jengo la makao makuu ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) mjini Dar es Salaam.
Alisema kwamba Mtei hakutaka jengo hilo lijengwe na kampuni ya ujenzi ya nje ya nchi hivyo akasisitiza ujenzi huo ufanywe na kampuni ya kizalendo ya Mwananchi Engeneering and Contracting Company (MECCO) iliyokuwa chini ya chama cha TANU ikapewa kazi hiyo baada ya kushinda zabuni.
Kwa hakika, ukisoma kitabu cha From Goatherd to Governor, sakata zima la kujiuzulu kwake uwaziri litakushangaza kama wengi walivyoshangazwa hata na Mtei mwenyewe kwamba hakupata kujikuta katika msukosuko mkubwa au kulazimika kuikimbia Tanzania.
Ndiyo, tukio kama hilo wakati wa enzi hizo za chama kimoja katika nchi nyingi za Afrika lilikuwa sababu tosha ya kuonekana au kuchukuliwa kuwa mhaini, hivyo lolote lingeweza kumpata.
Lakini Mtei, si tu hakupata msukosuko wa aina yoyote, lakini miaka mitatu baadaye Mwalimu Nyerere alimteua kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa IMF akiwakilisha nchi za Afrika zinazozungumza lugha ya Kiingereza isipokuwa Afrika Kusini enzi hizo za ubaguzi wa rangi nchini humo.
Hivyo akaenda kwenye makao yake makuu mjini Washington, Marekani ambako alifanya kazi hiyo kwa miaka minne akizunguka dunia katika kuifanya kazi hiyo kwani alikuwa anahitajika kusafiri sana.
Lakini ni nini hasa walichokuwa wamekosana na Mwalimu hata akalazimika kujiuzulu uwaziri wa fedha? Ni hadithi ndefu, lakini kimsingi ni kwamba Mwalimu alikataa kukubaliana na mpango wa IMF wa kurekebisha uchumi wa Tanzania wakati huo kama yeye alivyokuwa amekubaliana na ujumbe wa IMF ulioongzwa na Bo Karlstrom, raia wa Sweden.
Kulikuwa na mambo mawili ambayo Mwalimu hakukubaliana nayo na mambo hayo ni kupunguza thamani ya shilingi na kufanya marekebisho ya menejimenti ya mashirika ya umma ambayo mengi yalikuwa yakiendeshwa kwa hasara.
Kuhusu mashirika hayo yaliyokuwa yakiendeshwa kwa ruzuku ya serikali yalivyokuwa yakiendeshwa kwa hasara, Mtei anaeleza katika kitabu hicho jinsi alivyompatia mtaalamu mmoja wa Denmark kazi ya kuchunguza shughuuli za lililokuwa Shirika la Usagishaji la Taifa (NMC).
Ripoti ya mtaalamu huyo ilionyesha matumizi mabaya ya magari ya shirika hilo yaliyokuwa yakifanywa na viongozi wasio waaminifu na madereva.
Kutokana na ripoti hiyo, Mtei anasema aliona kwamba dawa ya kuyanusuru mashirika hayo ni kuwa na mameneja na wasimamizi ambao pia ni wadau katika uendeshaji wa makampuni hayo.
Mtei anasema wazo lake lilionekana kuwa na chembechembe za ubebari, kitu ambacho kilikuwa sumu wakati huo. Lakini ilikuwa muhimu kuwa muwazi kwa Rais, kwani sikuwa na ufumbuzi mwingine, anasema Mtei.
Kwa kuwa na wazo hilo, Mtei anasema alikuwa amefikiria kuwakaribisha watu au makampuni yanayomilikiwa na Chande Industries kurejeshewa sehemu ya hisa ili kuwepo na menejimenti nzuri na mali za shirika zipate kulindwa.
Kwa mujibu wa Mtei, mpango huo ungefanikiwa kwa kuwa Andy Chande mwenyewe aliyekuwa mkurugenzi mtendaji wa NMC na chini yake shirika hilo liliendedshwa kwa mafanikio makubwa.
Ujumbe wa IMF ulitoa wazo ambalo alikubaliana nalo kwamba kama taifa litapunguza matumizi ya ulinzi na kufanya marekebisho ya menejimenti za mashirika ya umma ili ziondokane na ruzuku kubwa inayotoka serikalini, thamani ya shilingi ingepunguzwa na kuanzia hapo mambo taratibu yangekwenda vizuri.
Kwa mujibu wa Mtei, suala la kuingilia menejimenti za mashirika ya umma na kupunguza thamni ya shilingi, ni mambo ambayo Mwalimu alikuwa hataki kuyasikia.
Baada ya kumweleza Karlstrom msimamo wa Mwalimu, Ofisa huyo wa IMF aliomba ujumbe wake ukutane naye Mwalimu. Ofisa huyo alikuwa na matumini kwamba angeweza kumfanya Mwalimu alegeze msimamo wake.
Mtei alifanya mpango wa kukutana na Mwalimu na akafanikiwa kuwakutanisha nyumbani kwa Mwalimu (Msasani), Novemba 29, 1979. Kilichotokea siku hiyo ndicho kilichomfanya Mtei ajiuzulu uwaziri.
Kwa mujibu wa Mtei, Mwalimu alishikilia msimamo ule ule na si tu hakuyumba; bali aliuupuza katikati ya mazungumzo kwa kuondoka ghafla kwenda kupunga upepo eneo la baharini nyuma ya nyumba yake ya Msasani.
Baada ya kuwaacha solemba kwenye veranda, Mtei alimfuata Mwalimu ili angalau amwambie kwamba wanaondoka. Alipomwendea, Mwalimu akamwambia kwamba wageni waliokuja walikuwa wajeuri na yeye hawezi kuiacha nchi yake iongozwe kutoka Washington (Marekani).
Alimwambia kwamba awaambie warudi Washington; kwani yeye hatathubutu kuishusha thamani ya Shilingi ya Tanzania.
Mtei anasema katika kitabu hicho kwamba hakulala usingizi siku hiyo aliporudi nyumbani. Akakata shauri ajiuzulu uwaziri. Siku inayofuata ilikuwa ya mapumziko lakini pamoja na hivyo akaenda ofisini asubuhi kuandika barua hiyo ya kujiuzulu.
Aliandika barua hiyo ya kujiuzulu kwa mkono wake ili baadaye ipigwe chapa. Baada ya kumaliza kuiandika barua hiyo akapokea simu kutoka kwa John Malecela aliyekuwa Waziri wa Kilimo kwamba wanatakiwa nyumbani kwa Mwalimu Msasani.
Mwalimu alikuwa amewaita kuzungumza nao suala la Serikali kununua kiwanda cha Tanganyika Planting Company kilichokuwa kinamilikiwa na Denmark.
Baada ya kufika ofisini kwake alidhamiria kuiwasilisha barua ile ya kujiuzulu aliyoiandika kwa mkono; hivyo alipotoka ofisini kwa safari ya Msasani, nje ya ofisi hiyo akakutana na msaidizi wa Mwalimu ambaye alimpatia barua.
Akaitupa barua hiyo kwenye kiti cha gari yake bila ya kuisoma. Akakaa kwenye kiti cha dereva tayari kwa safari ya kurudi tena Msasani kuwasilisha barua yake ya kujiuzulu.
Baada ya kuisoma barua yake, Mwalimu alimwuliza iwapo msaidizi wake alikuwa amempatia barua aliyomtuma ampe. Mtei akamweleza kwamba alikuwa amekutana naye nje ya ofisi na kumkabidhi barua hiyo ambayo hajaisoma kwani iko kwenye gari.
Mwalimu alionekana kufikiria kidogo na kumwambia kwamba anamshukuru kwa barua yake. Akamwita msaidizi wake kumwambia kwamba akatangaze kwenye vyombo vya habari kwamba Waziri wa Fedha amejiuzulu na kwamba yeye amekubali.
Kumbe barua ambayo Mtei alikuwa bado hajaisoma ilikuwa inatoka kwa Mwalimu ikimweleza kwamba ametengua uteuzi wake wa uwaziri wa fedha!
Katika barua hiyo fupi, Mwalimu alimweleza kwamba ameamua kutengua uwaziri wake wa Fedha na Mipango na kuongeza kwamba asingeruhusu serikali kuongozwa na Washington.
Katika aya nyingine ya barua hiyo, Mwalimu alisema kwamba alikuwa amemuelekeza awafukuze nchini watu hao wa IMF; lakini yeye (Mtei) hakufuata maelekezo yake.
Mtei anasema katika kitabu hicho kuwa asingeweza kuijibu barua hiyo au kumwandikia barua Rais kwa ufafanuzi kwa sababu aliamini kwamba kwa kupokea barua yake ya kujiuzulu na kuikubali, ile ya kwake ya kutengua uwaziri wake ilikuwa imefutwa.
Hata hivyo, alisikitika kwamba Mwalimu bado alikuwa ameshikilia msimamo wake kwamba juhudi walizokuwa wakizifanya zilikuwa zinatokana na maelekezo kutoka Washington.
Pia Mtei anasema alishindwa kutafisri maneno ya Mwalimu alipomwambia kwamba watu hao warudi Washington kuwa ni sawa na kwamba wafukuzwe nchini.
Mtei anashangaa katika kitabu hicho kwa kutupiwa kazi ya kuwafukuza maofisa hao wa IMF nchini wakati yeye hakuwa waziri anayehusika na kuwafukuza nchini wahamiaji haramu.
Mtei, ambaye sasa ni mkulima wa kahawa mkoani Arusha, ni mwanzilishi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Hicho ni chama pekee ambacho Mwalimu aliwahi kukisifu kwamba kina sera nzuri miongoni mwa vyama upinzani nchini
Source: Raia Mwema