mwacheni kidogo apumzike, amekuwa affected na matokeo!!!!!!!!!!!!!!!!!!Mananeo haya yamesemwa na Naibu Katibu mkuu CUF-Tanzania bara, ndugu Julius Mtatiro wakati akihojiwa na TBC1 kwenye viwanja vya halmashauri ya Igunga mara baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa mbunge katika jimbo hilo ambapo mgombea wa CCM alitangazwa kuwa mshindi!
wana chadema je mna utetezi wowote kuhusu tuhuma hizo?
kaka niyaneanayo ni kweli kabisa nakuomba uangalie taarifa ya habari tbc1 saa mbili usiku huu kama wata-cover vizuri nafikiri utamsikiamy bro! TAKEURABU!!
kama kweli Mtatiro ameongea maneno hayo ambayo ninaya-consider incredibly puking basi huyu jamaa atakuwa ana-confirm my theory that he's an authentic imbecile!!! Just yesterday i read his thread titled "CUF- tumefanya vibaya sana ktk uchaguzi mdogo wa Igunga" na ktk hiyo thread hakuwa anazungumzia hongo za CHADEMA bali alifanya what we can consider as a partial critical analysis and honestly speaking I appreciated his point of view, now what he says(?) today is completely and totally different from what he wrote yesterday - myself i'll tend to believe in what he wrote yesterday, verba volant scriptum manent - kama ataendelea kusisitiza kuwa CHADEMA wameonga pesa ili wachaguliwe basi nitazidi kuamini kuwa ana mtindio wa ubongo au hajui asemalo - ninaamini zaidi katika mtindio wa ubongo!!!
Umenijibia yote.Sikio la kufa...................
.
Julius Mtatiro
Yesterday 21:57
CUF tumefanya vibaya sana katika uchaguzi mdogo wa Igunga
Lazima nikiri kuwa washindani wetu wakubwa CCM na CHADEMA wametushinda katika uchaguzi mdogo wa Igunga. ...
Mimi kama kiongozi wa ngazi ya juu wa CUF - Tanzania Bara(Bila kujali nimekuwa kiongozi wa ngazi ya juu miezi minne tu iliyopita tu) nabeba dhamana kwa matokeo yote tuliyopita, najitwika mzigo wa kusimama imara kuiimarisha CUF. Sitatoka CUF na kukimbilia kwenye vyama vyenye nguvu Tanzania bara kama CHADEMA n.k. eti kwa sababu tu CUF imefanya vibaya kwenye uchaguzi. Ninaamini katika CUF na nitaisaidia Tanzania yangu nikiwa CUF, ninaamini siku moja wakati CUF imeimarika nitatajwa kati ya watu ambao hawakukata tamaa na hawakuyumbishwa na magumu yaliyowakabili na walisimama kidete kwenda mbele.
Tunawashukuru wale wote waliotuunga mkono katika uchaguzi huu na wale wanaotuunga mkono siku zote na wale watakaotuunga mkono siku zijazo. Kwa hakika wote tunawashukuru sana na CUF itasimama imara.
Mungu awabariki sana.
"HAKI SAWA KWA WOTE"
Julius Mtatiro,
Naibu Katibu Mkuu,
Chama Cha Wananchi - CUF,
Tanzania Bara,
02 Oktoba 2011,
Igunga - Tabora.