Mtatiro: CHADEMA wameanza kuiga mbinu chafu za CCM za kuhonga wapiga kura

Great thinkers nawashauri kuachana na huyu dogo is another Nape kwenye hii forum .Dogo kwa umri ule hawezi kusoma alama za nyakati yet una amini kwamba ni mtu wa maana? Mwacheni aropoke maana hata akiulizwa kama anaweza kuonyesha hongo ipi na wapi ataishia ku waya waya .What he is doing ni kuwasaidia CCM ili watu waseme kwamba Chadema sawa na CCM wana honga lakini hajui timing ni mbovu mwache ale cha nyuma ataamka late .Leave the guy alone tuendelee na mijadala ya kuijenga Tanzania .Tujipange kuitetea Tanzania ni si hawa CCM ambayo wameshindwa mizengwe pamoja na bakwata yao na CUF nyuma .
 
Dhambi ya kuungana na mafisadi kuhujumu nguvu ya ummaa itaendelea kuitafuna CUF mpaka kifo kiwafike
 
Mtatilo anaongea kama vile ni kijana wa mtaani. Mbona haoneshi kuwa ni kiongozi wa Chama kitaifa???????????? Anaropoka tu. Hakumbuki aliyokwisha sema na hapimi anayoyasema kwa sasa....
 
Ajaona mashehe waliotangaza watu wainyime kura cdm,maskini weeh mtatiro akajua kafu watakuwa na kura nyingi ya cdm ,mfa maji huyo anatapatapa
 
Mtatiro hana hoja. Yeye (CUF) kama mwaka jana walipata kura zaidi ya 20,000 iweje leo wapate 2,000? ina maana wamewagawia CCM hizo 18,000 ili washinde?. Akubali tuu kwamba chama chake kimepoteza mwelekeo kwa sababu ya muafaka wa Zanzibar.
 
Mananeo haya yamesemwa na Naibu Katibu mkuu CUF-Tanzania bara, ndugu Julius Mtatiro wakati akihojiwa na TBC1 kwenye viwanja vya halmashauri ya Igunga mara baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa mbunge katika jimbo hilo ambapo mgombea wa CCM alitangazwa kuwa mshindi!

wana chadema je mna utetezi wowote kuhusu tuhuma hizo?
Haya ni maneno aliyoyanena jana humu JF na kukiri CUF imefanya vibaya na kukiri kuwa yeye binafsi abebeshwe mzigo wa matokeo mabaya ya CUF Igunga. Mtatiro anavyosema kuwa abebeshwe mzigo wa matokeo mabaya ya CUF ktk uchaguzi wa Igunga inadhihirisha anakiri kuwa siasa zake za maji taka anazozitumia yeye binafsi ndio zimekiponza chama chake Igunga. CUF inauliwa na inafukiwa kaburi lake na siasa za kipopo za Mtatiro.Amekiri pia ile kashfa ya CUF kuwa ni CCM-B inawatafuna sana ila badala ya kupambana na hili la CCM-B ili kuiweka CUF katika level ya jeneza na sii katika level hii ya kaburi iliyopo sasa yeye anaendekeza siasa za maji ya chooni dhidi ya chama kingine cha upinzani chenye nia moja na chama chake dhidi ya chama tawala.
Jana kakiri makosa ila leo anarudia kosa kama la wali kwa kusema CDM inahonga kama CCM kwani kauli hizi ni moja ya siasa za maji machafu alizozoea kuzifanya na zilizokiponza chama chake kama alivyo kiri hapa chini kwenye thread yake ya jana.


user-offline.png
Julius Mtatiro

Yesterday 21:57


Junior Member
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png



Join Date : 4th September 2011
Posts : 4
Rep Power : 0



[h=2]
icon1.png
CUF tumefanya vibaya sana katika uchaguzi mdogo wa Igunga[/h] Lazima nikiri kuwa washindani wetu wakubwa CCM na CHADEMA wametushinda katika uchaguzi mdogo wa Igunga.

Kwa matokeo ambayo nimeyashayapokea kutoka kwenye asilimia 88 ya vituo kwa ujumla tumefanya vibaya sana. Japokuwa tumekuwa na mgombea mzuri sana na tumemnadi kwa kutumia uwezo wetu wote ambao kwa hakika kila mtu ameuona, lakini matokeo hatuwezi kuyageuza.

Ninachojifunza zaidi ni kuwa wapiga kura wengi ndani ya Tanzania bado wanaamini zaidi propaganda kuliko hali halisi ya mazingira yanayowakabili na hii ikizidi kushabikiwa ndivyo ambavyo wananchi watakosa fursa bora siku za mbele.
Ikiwa hali hii itaendelea hivi ina maana bado nchi ina safari ndefu ya kufikia demokrasia ya kweli na maendeleo yatakayoonekana kwa macho.

Katika uchaguzi huu wa Igunga CUF tumepambana na changamoto kubwa ya kujibu propaganda zilezile kuwa eti "Sisi ni CCM B", kila tulikoenda tumekutana na kikwazo hiki, tumejaribu kwa dhati kuwaelimisha wananchi bila mafanikio na muda umekuwa ukikimbia kuliko upepo.

Hata hivyo bado naamini kuwa tutapata fursa kubwa ya kuwaelimisha wananchi siku za usoni. Mimi na wenzangu hatutakata tamaa kwani MAFANIKIO KATIKA NYANJA YA SIASA huhitaji mioyo migumu.

Natambua kuwa uongozi ni dhamana nzito inayohitaji kujipanga zaidi na zaidi, Na CUF itazidi kujipanga zaidi na zaidi na kila tutakapoanguka tutanyanyuka na kuanza safari, hakika TUTAFIKA.

Chama changu kinakabiliwa na changamoto kubwa sana mbele ya safari na kwa hakika inahitaji tuzidi kujipanga na kujiimarisha. Kama chama hatutajilaumu kamwe, tumeonesha uwezo mkubwa na kufanya kampeni sahihi tukiwa na mgombea wa kiwango kizuri kwa mpiga kura yeyote anayehitaji kiongozi. Lakini kusimamisha mgombea mzuri na kufanya kampeni nzuri wakati mwingine siyo sababu ya kufanya vizuri. Maamuzi ya nani awe mbunge, ni mzuri au mbaya, anafaa au hafai yako kwa wananchi.

Wananchi wa Igunga tunawashukuru kwa namna walivyotuunga mkono na tunawaomba wawe kitu kimoja katika kuiendeleza Igunga yao kwani mshindi akishatangazwa yeye ni mbunge wa wananchi wote. Vyama vyetu hivi vipo ili kuisaidia jamii kupata kiongozi mzuri tu, nasi kama chama tumetimiza wajibu wetu.

Mimi kama kiongozi wa ngazi ya juu wa CUF - Tanzania Bara(Bila kujali nimekuwa kiongozi wa ngazi ya juu miezi minne tu iliyopita tu) nabeba dhamana kwa matokeo yote tuliyopita, najitwika mzigo wa kusimama imara kuiimarisha CUF. Sitatoka CUF na kukimbilia kwenye vyama vyenye nguvu Tanzania bara kama CHADEMA n.k. eti kwa sababu tu CUF imefanya vibaya kwenye uchaguzi. Ninaamini katika CUF na nitaisaidia Tanzania yangu nikiwa CUF, ninaamini siku moja wakati CUF imeimarika nitatajwa kati ya watu ambao hawakukata tamaa na hawakuyumbishwa na magumu yaliyowakabili na walisimama kidete kwenda mbele.

Tunawashukuru wale wote waliotuunga mkono katika uchaguzi huu na wale wanaotuunga mkono siku zote na wale watakaotuunga mkono siku zijazo. Kwa hakika wote tunawashukuru sana na CUF itasimama imara.

Mungu awabariki sana.

"HAKI SAWA KWA WOTE"

Julius Mtatiro,
Naibu Katibu Mkuu,
Chama Cha Wananchi - CUF,
Tanzania Bara,
02 Oktoba 2011,
Igunga - Tabora.
 
Hakuna utetezi, ila inabidi kumshangaa. Anatakiwa ajifunze wapinzani wameteleza wapi. Maana katika matokeo ya jumla tofauti ya ccm na wapinzani itz too narrow ikiwa ni dalili kwamba upinzani umeingia igunga jimboni kwa kasi ya ajabu sana. By keeping the same trend ccm kinaweza kuwaka by 2015. Assume kuwa hakuna uchaguzi tena hapa katikati...
 
Mtatiro nenda kachemshe hayo masifuri mle na wenzio,hiyo ndio zawadi yenu.
 
Mwisho wa CUF umekwishafika na mwisho wa CCM unakaribia (2015). Waliona raha kuungana na CCM na ndio maana wameangukia pua. Nawashauri CDM waanze kufanya kazi ya kujitolea kuelimisha wananchi kujiandikisha na kujitokeza kupiga kura. Hawa NEC hawafanyi ili CCM iendelee kuchaguliwa na watu wa vijijini huku wakiwarubuni waislamu wa watu kupitia bakwata.

WAISLAMU toeni tamko dhidi ya BAKWATA.
 
CUF ni vichaa hawa yaani wanadhani siasa ni maigizo warudi kule kule Pemba si huku bara .
 
Huyu jamaa nazani kakosea tu,,,,alikuwa anamaanisha CCM aka magamba!
 
Great looser CUF aka CCM B!Nahisi mliwapatia kura zenu ili wasije kuwaletea tifu ndani ya nyumba maana mmefunga ndoa ya mkeka!Bravo cdm!you paved the way!excellent
Yeah, wanaita "Terrible loser"
 
Back
Top Bottom