Mtanzania: Hali si shwari Zanzibar; Pemba yataka uhuru kamili

Ileje

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
8,827
12,280
*Wastaafu wataka Unguja na Pemba zitengane
KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida Waziri wa zamani na wafanyakazi wastaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), wametoa wito wakitaka visiwa vya Unguja na Pemba vijitawale. Wastaafu hao ni waliokuwa wanajeshi wastaafu, askari wa vikosi vya SMZ, wafanyakazi wa wizara na idara za mbalimbali za umma.

Katika kongamano lililofanyika siku chache zilizopita kwenye ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi uliopo eneo la Kikwajuni, walisema ipo haja ya kufanyika ‘mapinduzi ya heshima na adabu’, baada ya yale ya 1964.

Kongamano lilikuwa chini uenyekiti wa Ali Hassan Khamis, ambapo mbali ya wastaafu, pia lilihudhuriwa na wakulima na wafanyakazi wa SMZ.

Miongoni mwa walioshiriki ni aliyewahi kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Awamu ya Pili Zanzibar), Aboud Talib Aboud. Yeye aliondolewa madarakani pamoja na Rais Aboud Jumbe mwaka 1984, baada ya hali ya kisiasa kuchafuka visiwani humo.

Aboud alisema watu kutoka Oman walifika Zanzibar kama walowezi na kuigeuza ardhi mali yao hadi yalipofanyika Mapinduzi yaliyorejesha hadhi, utu na ukombozi wa wananchi wanyonge 1964.

“Jueni kwamba Zanzibar haitatawaliwa tena na wageni. Wanaosema ‘Zanzibar kwanza’, nawaeleza kuwa ni ‘wananchi kwanza’ na Mapinduzi ndio yaliyowakomboa Waafrika wanyonge, hatutakubali ng’o kuwa chini ya ukoloni mamboleo,” alisema Aboud.

Mbunge wa zamani wa Kikwajuni, Parmuk Hogan Sing, aliipoda Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) Zanzibar akidai haikutokana na ridhaa ya Wazanzibari wengi na kudai wameingizwa viongozi wapinga sera za umoja, Mapinduzi na Muungano, hivyo inakosa uzani wa uhalali na kuaminiwa.

Mshiriki wa kongamano hilo, Ali Machano Khamis, alisema matatizo yanayokikumba kisiwa cha Unguja ni kitendo cha kuchaguliwa wagombea urais ambao si chaguo la Wazanzibari.

Alisema wagombea hao wasiofaa ndio chanzo na kiini cha kuanza kulegelega kwa utetezi wa misingi ya Mapinduzi, na kuwataka wazee kuanza kujirekebisha kuhakikisha wanaoteuliwa lazima wawe na uchungu wa nchi, si wasaka maslahi binafsi.

Akizungumzia mchakato wa kuundwa SUK, Suleiman Omar Suleiman, alisema ulifanyika kibabe na kwa hila bila kuwaweka vituoni mawakala wa kusimamaia kura za maoni kujua idadi ya waliosema “hapana” na “ndiyo”.

Alisema hakuna kigezo halisi cha kuwapo Muungano wa visiwa vya Unguja na Pemba tangu asili na jadi, na kwamba muda umefika sasa kwa visiwa hivyo kujigawa, kila upande uwe na mamlaka yake kamili.

“Ni vipi Pemba iwe ya Wapemba, Unguja iwe ya wote? Viwanja vya Unguja wamepewa Wapemba wakati Pemba hakuna Muunguja anayeishi na kujenga nyumba. Jamani, Waunguja tumechoka! Tunataka mamlaka yetu haraka,” alisema Suleiman.


Kuibuka kwa madai hayo wakati huu huenda kukaiweka Serikali ya Rais Dk. Ali Mohamed Shein katika taharuki na kuitikisika SUK iliyopatikana baada ya mazungumzo kusaka muafaka, na kubadilishwa kifungu cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, hivyo kufanyika kwa kura za maoni ambapo asilimia 66 ya Wazanzibari waliikubali SUK.

Khamis Mwinyishehe Suleimna alisema Pemba haikushiriki katika harakati za Mapinduzi ya Zanzibar na hata walipotakiwa na Waingereza wakapigane Vita Kuu ya Pili ya Dunia (1939 hadi 1945), walikataa kwa madai kuwa wao walikuwa chini ya Wareno.

Alisema kati ya waasisi 14 wa Mapinduzi hakuna hata mmoja kutoka Kisiwa cha Pemba, hivyo suala la visiwa hivyo kujitenga halihitaji mapatano wala mazungumzo ya suluhu mezani.

Mzee Younus Haji alisema jambo hatari lililofanyika katika uundwaji wa SUK ni kuingizwa viongozi wenye itikadi za vyama vya zamani vya Zanzibar and Pemba Peoples Party (ZPPP) na Zanzibar Nationalist Party (ZNP), na kwamba sasa ni wakati muafaka wa kufanya tathmini kuhusu Serikali hiyo na kutafuta Katiba mpya ya Zanzibar.

Wastaafu wengi waliozungumza walionekana kusikitishwa na kuvunjwa kwa miiko ya Mapinduzi ya Zanzibar wakisema waliomrithi Rais Abeid Amani Karume, walipuuzia wosia ulioachwa na viongozi wa Afro Shiraz Party (ASP) na waasisi wake.

“Kama watu hawa wangependa umoja na maridhiano tangu awali hata Mapinduzi ya mwaka 1964 yasingetokea, kwani kiongozi wa ZPPP, Mohamed Shamte Hamad, angeunganisha viti vyake vitatu na ASP basi,” alisema Mzee Kheir.

Madai yao mengine ni kwamba wazee wa Pemba wamewahi kwenda hadi Ofisi za Umoja wa Mataifa Dar es Salaam mwaka 2000 wakitaka wapewe mamlaka, na kwamba ni heri wakapewa sasa kuepusha shari.

Ahmed Khamis Mcheju alisema kitendo chochote cha kuyapuuza Mapinduzi ya Zanzibar hakivumiliki kwa Waafrika waliobaguliwa na kudharauliwa tangu kuondolewa madarakani kwa kiongozi wa Kiafrika, Mwinyimkuu, na Waarabu kutoka Oman mwaka 1804.

Madai hayo mazito ni kama ishara ya kutimia kwa utabiri Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere aliyewahi kusema nje ya Muungano kutajitokeza Uzanzibari na Uzanzibara, kisha Uunguja na Upemba na Taifa halitabaki salama.


[h=4]Toa Maoni yako kwa habari hii[/h]
 
Baba wa Taifa aliona Mbali sana,dhambi ya ubaguzi haiishi kamwe.. kumbe Pemba na Unguja sio wamoja tena, na hawajawai kukubaliana kuwa pamoja.

Muda sio mrefu tutashuhudia Pemba ikiwa ngome kuu ya Allshababi.

Ili kuikoa Zanzibar dawa ni Serikali moja Ya Tanzania.!
 
Baada ya hapo kutatokea Operesheni kuwatimua Wapemba Tanzania Bara. Hakika lawama kamili ziwaendee rasmi viongozi wa CUF hususani Maalim Seif Shariff Hamad. Huyu amekuwa akihubiri utengano wa Bara na Visiwani hakuna hatua inayochukuliwa dhidi ya mtu kama huyu.

Kuukosa Urais baada ya umbea alioufanya kuleta memorandum aliyotakiwa kusaini Aboud Jumbe mwaka 1982 kulimfanya awe kichaa wa kuutenganisha Muungano wa Bara na Visiwani. Kwa maana nyingine ni kwamba alichokitaka Jumbe wakati ule Maalim Seif akakipinga ndicho anachokifanya sasa Maalim Seif leo, huyu naye anastahili yale yaliyomkuta Aboud Jumbe Mwinyi kufutwa katika nyanja za siasa.
 
Tumekuwa tukipiga kelele kudhibitiwa Uamsho kwa hatua kali zaidi bils mafanikio makubwa.
Uamsho, waarabu, Maalim Sefu .lao moja.
Sasa inaelekea udhibiti wao utatoka huko huko Zanzibar, kumekucha, mapinduxi mengine yananukia!
 
tuache utani Nyerere alikua jembe na aliona mbali sana sana kuwa baada ya kujitenga Tanganyika na Zanzibar, mtajikuta na nyie hamko pamoja, mnagawanyika tena (Pemba na Unguja) NA KAMWE HAMTABAKI SALAMA.......
Wewe ndiyo unaleta utani!. Mwl. Nyerere kwenye swala la Zanzibar kujitenga hakujenga hoja kwa kuona mbali, bali alitumia historia kwa njia ambao ionekane kama anajenga hoja kwa kuona mbali wakati alichokuwa anafanya ni ku-rewind historia na kumbusha tu ambao hawakuijua au waliosahau.

Ukisoma vizuri hii article atagundua kuwa matatizo yalikuwepo na yaliendelea kuwepo chni ya kapeti kwa vile kuyatoa nje ni kupambana na kosa la uhaini ndani ya katiba ya nchi. Kamuulize Mzee Aboud Jumbe na Maalim Seif Shalif Hamad watakueleza nini maana ya hiki ninachokisema

Tusipende kutoa sifa na pongezi kwenye jambo ambalo halistahili.
 

Madai hayo mazito ni kama ishara ya kutimia kwa utabiri Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere aliyewahi kusema nje ya Muungano kutajitokeza Uzanzibari na Uzanzibara, kisha Uunguja na Upemba na Taifa halitabaki salama.


Toa Maoni yako kwa habari hii


Sasa wewe nawe wacha kuleta porojo hapo yanazungumzwa ndani ya Muungano au nje ya Muungano? fikiri japo kidogo.
 
Sasa wewe nawe wacha kuleta porojo hapo yanazungumzwa ndani ya Muungano au nje ya Muungano? fikiri japo kidogo.
Nadhani bado hujapata kifungua kinywa mama! Hapo ni kuonyesha watu wanajadiliana kutengana wakiwa bado wako chini ya mwamvuli wa muungano, je muungano ukivunjika si itakuwa balaa!?
 
Kuna watu wanakaa wanamtukana Mwalimu Nyerere hapa JF kama huyu FaizaFoxy na wenzake. Hivi haya mwalimu Nyerere akutahadharisha mapema? Mwalimu aliwai sema, kama Zanzibar ikijitenga, tena kwasababu ya ulafi, ulafi wa madaraka, wakishajitenga watagundua kuwa hakuna Zanzibar tena ila kuna UNGUJA NA PEMBA. Na hii ndio dhambi ya ubaguzi, itawatafuna na mimi naomba iwatafune kweli kweli.

Wazanzibar wanajidanganya kuwa ni wamoja, ila kama ni mfatiliaji wa historia ya ile nchi hakuna umoja pale. Watu wa Unguja wanamalalamiko mengi kweli kweli. Wao wanadhani wanachukuliwa kama daraja la pili kule Zanzibar. Zanzibar sio wamoja wanajidangaya hao watu. Mimi naomba dhambi hii IWATAFUNE MPAKA WAKOME. Maana ni wabaguzi sana hawa watu.
 
Serikali mbili zimekuwa kandamizi na zimeshindwa kuondoa matatizo ya muungano hata baada ya zaidi ya miaka 49.

Kama tunataka kuwepo na Muungano IMARA lazima tuwe na serikali MOJA, na kama tunataka muungano uendelee kuwa kandamizi (unbalanced) na wenye matatizo yanayoongezeka kila siku lazima tuendelee kuwa na serikali MBILI, na kama tunataka muungano uvunjike lazima tuwe na serikali TATU.

Kupanga ni kuchagua.

Mimi nimeisha panga na kuchagua kuwa, huu muungano tegemezi lazima uvunjike bila hata ya kupitia serikali TATU kwa sababu kufanya hivyo kutapunguza gharama za kisiasa na kiuchumi.
 
Ngoja kwanza tupate Zanzibar yenye mamlaka kamili, hao wazee tuta deal nao baadae wasitutoe kwenye lengo kuu.

Zanzibar na Tanganyika zenye mamlaka kamili kwanza!
 
Back
Top Bottom