Mtanzania: Hali si shwari Zanzibar; Pemba yataka uhuru kamili

Hakika mtakatifu Julius Kambarage Nyerere alikuwa mtakatifu... Mungu alikuwa anampa maono... Hao wanao mlani wanajilaani wenyewe hao... Na nasema kwa jina la Mwenyezi watalaaniwa kabisa...
 
Ngoja kwanza tupate Zanzibar yenye mamlaka kamili, hao wazee tuta deal nao baadae wasitutoe kwenye lengo kuu.

Zanzibar na Tanganyika zenye mamlaka kamili kwanza!

Mkuu unaongelea Zanzibar ya Unguja au Pemba.!!
 
Wacheni kuwa na mawazo mgando make change if there is any need for it enzi zile alisema enzi zile alisema inamana watanzania sote hatuna akinili isipokua .......................... maneno huumba nia ya waliosema hayo ni kuumba huo mgawanyiko na sio prediction
 
Hiviiii mimi naomba kuuliza....Nikipanda boti pale feri ...nikisema nataka kwenda zanzibar...ntapelekwa wapi? unguja? au pemba? au kuna kasehemu kana ardhi tofauti ambako ndo zanzibar, ahha ebu tusaidiane kidogo hapa.
 
Nadhani bado hujapata kifungua kinywa mama! Hapo ni kuonyesha watu wanajadiliana kutengana wakiwa bado wako chini ya mwamvuli wa muungano, je muungano ukivunjika si itakuwa balaa!?

Ikiwa yanazungumzwa ndani ya Muungano basi hiyo quote ya marehemu uliyoiweka haina maana kabisa hapa, yeye alisema nje ya muungano.

Haya ya Wapemba na Waunguja waachie wenyewe, wewe huyawezi.
 
Kwa hali hii tanganyika inarudi haraka, tujiandae kupokea wenzetu weusi watakaobaguliwa na weupe[waarabu]
 
YAMETIMIA .NDIO YAMEANZA KILA MTU ANATAKA MADARAKA. Bara tutulie wenzetu wana wafadhili uarabunia watakula bila kufanya kazi .
 
Baada ya Zanzibar kujiona wakubwa wakatukataa sisi Wabara, Je suala wa Wao wapemba na sisi Waunguja, Linatuhusu nini bara? Si wapige kura wao kwa wao kujitenga?
 
Mimi sioni sababu ya kuendelea kuumiza vichwa kwa suala la muungano wa tanganyika na zanzibar, inatosha sasa, waachiwe nchi yao ibaki ujilani mwema kama kenya, uganda, burundi congo nk
 
Maneno yale ya mwalimu yalikuwa ni mtego kwa wa zanzibari.
Mtigo wa kuwatisha wasijekutaka kuomba kujitoa katika huu mungano,ili waogope na kutothubutu kudai kwa nchi yao ya znz.
Lakini hebu tufikiri jambo moja kabla ya kuunganishwa nchi hizi mbili hapo awali hiyo inayoitwa Unguja na hiyo inayoitwa Pemba kihistoria zilikuwa hazipo?
Pili je kihistoria kulishawahi kuwapo pemba pekee au unguja pekee?
Ikiwa jibu ni hapana kwanini leo izuke fikra hii nahasa baada ya muungano hamuoni kama huu ni mtego?
Nimtazamo tu ila tutafika tunakokwenda.
 
maneno ya NYERERE YALEEEEEEEEE TUNAYOONA DHAMBI YA UBAGUZI..............HAIHISHII HAPO TU
 
Ni ukweli kuwa nje ya Muungano Zanzbar na Pemba zitatengana. Kwa nini ziungane kama tayari zimeshawakataa wabara? Nashukuru kuwa dalili hizi zinaanza kudhihirika sasa taratibu ili wapime athari za kuuvunja muungano huu wa sasa ambazo ni maoni ya baadhi ya wazanzbari!
 
hiviiii mimi naomba kuuliza....nikipanda boti pale feri ...nikisema nataka kwenda zanzibar...ntapelekwa wapi? Unguja? Au pemba? Au kuna kasehemu kana ardhi tofauti ambako ndo zanzibar, ahha ebu tusaidiane kidogo hapa.

utafika unguja then kama utahitaji kwenda pemba utapanda boat tena
 
Back
Top Bottom