Mtanzania aliechomwa Marekani hakuwa na ndugu, mwili wake ungerudishwa ungekosa wazikaji...

Kama ni hivyo sijui ni kitu gani kinachowatambulisha kama watanzania mkiwa huko baada ya kuukana uraia wa watanzania. Au ni suala la kusema tu mimi ni mtanzania basi? Ni sawa, tofauti na nchi nyingine Tz tumejitahidi kuuweka ukabila pembeni. Lakini muda wote mliishi naye hakuna anayejua alikuwa alikuwa kabila gani? Sio kwamba nawalaumu maana hata mkewe na watoto hawajui alitoka sehemu gani Tanzania - hapo ndio kwenye tatizo kubwa.

Uraia mtaupata au tuseme mtarudishiwa muwe na subira!

Nimepata kushuhudia Watanzania wengi licha ya kutoendekeza ukabila, lakini wamekuwa na kawaida ya kupambanua asili zao wanakotokea iwe ni Milima ya Usambara, Uruguru, Kipengere, Kilimanjara, Sekenke, Lyamba lya Mfipa, Udzungwa nk. Jambo la kushangaza kwa hayati hata kumtonya mmoja wapo wapi asili yake ingawa jina laelekea kama ni Mgosi wa Kaya. Hata hivyo nimeshangazwa na wengi wenye majina hayo kutojitokeza kwamba wanamfahamu.

Kuna baadhi kupendelea kutumia majina yao yasiyo halali na majina halali kutumia inapohitajika rasmi tu huweza kuleta mkanganyiko.

Tujaribu hata kama hatupendi kuwa karibu na ndugu walao wawili au watatu katika ndugu na jamaa au marafiki kuwafunda ambao wako nyumbani kwa mawasiliano.

Tunapojadili suala hilo hatumjadili hayati ila yatokanayo kwani kesho yanaweza kurejea kwa mtu mwingine.
 
Watu tuna matatizo ya kusoma na kuelewa!

Zile dola 6,000 hazikuwa kwa ajili ya marehemu kurudishwa Tanzania.

Zilikuwa ni kwa ajili ya marehemu kuzikwa mazishi ya kawaida huko huko Madison, WI, na si kuuchoma moto mwili wake.

Kusafirisha maiti kutoka Marekani kwenda Tanzania ni zaidi ya dola 6,000.

Sasa sijui kwa nini watu mnadhani kuwa hizo pesa zingekuwa ni za kuusafirisha mwili wake hadi Tanzania.

mkuu, with due respect naomba nitofautiane na wewe. dola buku 6 zinaweza kabisa kuleta mwili tz toka us. sbb pale zinapimwa kilo na human remains ni cargo. uzito mara nyingi hauzidi kilo 150kg depending na coffin lilivyo na hum weight.
 
Kwa hiyo unataka kuniambia kutoka Madison, WI mpaka JNIA dola 6,000 zingetosha kabisa?
 
Uraia tu mnamyima. Haya sasa toeni uraia basi hata kwa Watoto wake kama kweli mnaupendo huo.

Tanzania wakusaidiwa wapo kibao, kwa nini husaidii hao na unataka kusaidia Maiti?

Kama kweli unapesa ya KUZIKA, kwa nini usije hapa SKONGE na wewe uRITHI kijiji fulani? Hebu angalia jinsi familia huku zilivyo masikini za kutupwa. Fedha zako zitafanya la maana kuliko kulilia kuzika maiti.

Adopt-a-Village | Moravian Board of World Mission

DSCF6789.jpg

mkuu kwa hili natofautiana na wewe, sisi watz ni ndugu zake tungemzika popote ktk ardhi ya tanzania
 
Nimepata kushuhudia Watanzania wengi licha ya kutoendekeza ukabila, lakini wamekuwa na kawaida ya kupambanua asili zao wanakotokea iwe ni Milima ya Usambara, Uruguru, Kipengere, Kilimanjara, Sekenke, Lyamba lya Mfipa, Udzungwa nk. Jambo la kushangaza kwa hayati hata kumtonya mmoja wapo wapi asili yake ingawa jina laelekea kama ni Mgosi wa Kaya. Hata hivyo nimeshangazwa na wengi wenye majina hayo kutojitokeza kwamba wanamfahamu.

Kuna baadhi kupendelea kutumia majina yao yasiyo halali na majina halali kutumia inapohitajika rasmi tu huweza kuleta mkanganyiko.

Tujaribu hata kama hatupendi kuwa karibu na ndugu walao wawili au watatu katika ndugu na jamaa au marafiki kuwafunda ambao wako nyumbani kwa mawasiliano.

Tunapojadili suala hilo hatumjadili hayati ila yatokanayo kwani kesho yanaweza kurejea kwa mtu mwingine.
Nakubaliana na wewe mkuu.
Pamoja na kumhurumia marehemu kwa kuipata jehanamu ya moto hapa duniani, haingii akilini kwa nini hakuwa na mawasiliano na ingalau mmoja wa jamaa zake hapa nchini.

Mazingira ya kitatanishi hspa duniani tunsjiwekea wenyewe.
 
Mkuu lets call a spade a spade sio sepeto au chepeo.

Kosa ni la marehemu, hakuwa karibu na ndugu zake, na ndio maana hata mke na watoto wake hawajui alitokea wapi

Tunaambiwa kuwa mtoto wake wa kwanza alizaliwa 1989 which means ana umri wa miaka 25 sasa, umri tosha kuhoji baba ulitokea wapi?

Pia mwanamke anaishi na mtu miaka yote bila kujua mzee katokea wapi?

SOMETHING FISHY HERE....?????

uko right kbs chilisosi. mke hajui asili ya mumewe? na mtoto 25yrs lzm atakuwa inquisitive kumuuliza baba where is our roots. yameshatokea tumwache mgosi lukindo apumzike kwa amani na pole kwa familia yake.
 
mtanzania hana ndugu wa kumzika huku?wekeni jina lake kamili tuwatafutie ndugu zake sasa hivi!msiache kuweka jina la ukoo lile la kibantu
 
Watu tuna matatizo ya kusoma na kuelewa!

Zile dola 6,000 hazikuwa kwa ajili ya marehemu kurudishwa Tanzania.

Zilikuwa ni kwa ajili ya marehemu kuzikwa mazishi ya kawaida huko huko Madison, WI, na si kuuchoma moto mwili wake.

Kusafirisha maiti kutoka Marekani kwenda Tanzania ni zaidi ya dola 6,000.

Sasa sijui kwa nini watu mnadhani kuwa hizo pesa zingekuwa ni za kuusafirisha mwili wake hadi Tanzania.

Duh! Inamaanisha huyu jamaa alikuwa choka mbaya na je hata upande wa mke wake pia ni choka mbaya hadi kukosekana fedha hizo za kumzika huyo ndugu. Ni vema kuanzia sasa mkiwa huko muwekeze ili msipate aibu kama hii na hao mnaowaoa muangalie kwani ni aibu kuoa Mzungu masikini
 
uko right kbs chilisosi. mke hajui asili ya mumewe? na mtoto 25yrs lzm atakuwa inquisitive kumuuliza baba where is our roots. yameshatokea tumwache mgosi lukindo apumzike kwa amani na pole kwa familia yake.

Ni kweli kwamba watoto wake na mke wake watakua walitaka kutumia fursa hiyo kuwafahamu ndugu zake. Na ninatarajia watoto watafunga safari kuja Tanzania kuwatafuta ndugu za baba yao. Poleni wafiwa na Mungu awafariji ktk kipindi hiki kigumu.
 
Mkuu tatizo jamaa wanatushikia bango kluwa tumeshindwa kutoa hela wakati wenyewe wanajua hata ukiwa bongo kama aukijitenga na jumuia itakutenga.

Kama huendi misibani nao hawatakuja

Kama hutoi michango na wao hawatachanga.

Mimi hapo nawajibu watu kama Lemutuz wanaosema tunatia aibu kwa kushindwa kutoa hizo hela.#

Sasa hapo ndipo kwenye point..kumbe mlishindwa kwa kuwa alikuwa anajitenga nanyi na sio kuwa hana ndugu
 
Watu tuna matatizo ya kusoma na kuelewa!

Zile dola 6,000 hazikuwa kwa ajili ya marehemu kurudishwa Tanzania.

Zilikuwa ni kwa ajili ya marehemu kuzikwa mazishi ya kawaida huko huko Madison, WI, na si kuuchoma moto mwili wake.

Kusafirisha maiti kutoka Marekani kwenda Tanzania ni zaidi ya dola 6,000.

Sasa sijui kwa nini watu mnadhani kuwa hizo pesa zingekuwa ni za kuusafirisha mwili wake hadi Tanzania.

Mkuu hata mie nilishangaa mbona ni cheap sana kuna uzi humu jamaa mmoja wa dodoma alikuwa anasomeshwa na serikali nchini china, mwili wake ulichomwa moto na kusafirisha jivu baada ya ubalozi wa Tz nchini China kukosa $45000/= za kusafirisha maiti!!
 
Hivi wabeba boski ni watu gani, huwa naona watu wanawazungumzia na hata wengine kujiita hivyo lkn sielewi kitu?
Ndugu zanguni,

Kama mjuavyo, Le mutuz ameshikilia bango suala la mbongo kuchomwa moto Marekani baada ya kukosekana dola $6,000. Lakini nataka niwaulize mnaotukosoa, JE MNAMFAHAMU MARAEHEMU?, MNAWAFAHAMU NDUGU ZAKE?

Katika pitia pitia kwenye mitandao na baada ya kuongea na wabongo wawili watatu walioko boksi la US nimegundua kuwa jamaa hakuwa karibu na ndugu zake na hajawahi kanyaga Bongo miaka thelasini. Tunaambiwa kuwa hata mke na watoto wake hawajui jamaa alitokea wapi.

Sasa kama hata mke na watoto wake hawajui asili yake kwa nini watu walikuwa wanangangania arudishwe bongo?

Mnapigania maiti irudishwe bngo wakati angekuwa mzima mngemnyima uraia?

Mimi nawaasa tu jamaa zangu wabeba boksi, mkiwa huku nje muwe mnakumbuka nyumbani, msisahau kwenu na mhakikishe hata watoto wenu mliozaa na vishoka wanakwenda home waumwe na mbu kidogo ili wajue wazazi walitokea wapi.

Pia jamaa yangu Le mutuz acha kutulaumu, sisi hata hatujui jamaa katokea wapi ulitaka tuchange hela apelekwe wapi? Unaweza kwenda kuzika mtu Tanga kumbe katokea Angola, huoni kama ni dhambi hapo?

Kama mimi mwongo naomba kama kuna mtu anaemfahamu hata ndugu mmoja tu wa marehemu ajitokeze hapa
 
Mkuu hata mie nilishangaa mbona ni cheap sana kuna uzi humu jamaa mmoja wa dodoma alikuwa anasomeshwa na serikali nchini china, mwili wake ulichomwa moto na kusafirisha jivu baada ya ubalozi wa Tz nchini China kukosa $45000/= za kusafirisha maiti!!

Kuna upotoshaji wa hali ya juu uliofanyika kuhusu kukosekana kwa hizo fedha, dhumuni la lake, na kadhalika.
 
Msihangaike kujitetea saana, angalieni mlijikwaa wapi, muweze kujirekbisha.
 
Binadamu ukishakufa umekufa, suala la kuzikiwa wapi sio ishu unazikwa popote panapostahili period!

Ni kweli ukifa umekufa, kwako hakuna tatizo na hakuna jipya lakini kwa nduguzo hali siyo hiyo! Hata kwa anayeishi akiwa na akili timamu lazima awaze, baada ya kifo hali nyumbani kwake itakuwaje, watoto wake wataishije, mali yake itagawiwaje, n.k.

Tusijitoe utu kwakuwa yametokea ya kuchomwa moto.
 
Ndugu zanguni,

Kama mjuavyo, Le mutuz ameshikilia bango suala la mbongo kuchomwa moto Marekani baada ya kukosekana dola $6,000. Lakini nataka niwaulize mnaotukosoa, JE MNAMFAHAMU MARAEHEMU?, MNAWAFAHAMU NDUGU ZAKE?

Katika pitia pitia kwenye mitandao na baada ya kuongea na wabongo wawili watatu walioko boksi la US nimegundua kuwa jamaa hakuwa karibu na ndugu zake na hajawahi kanyaga Bongo miaka thelasini. Tunaambiwa kuwa hata mke na watoto wake hawajui jamaa alitokea wapi.

Sasa kama hata mke na watoto wake hawajui asili yake kwa nini watu walikuwa wanangangania arudishwe bongo?

Mnapigania maiti irudishwe bngo wakati angekuwa mzima mngemnyima uraia?

Mimi nawaasa tu jamaa zangu wabeba boksi, mkiwa huku nje muwe mnakumbuka nyumbani, msisahau kwenu na mhakikishe hata watoto wenu mliozaa na vishoka wanakwenda home waumwe na mbu kidogo ili wajue wazazi walitokea wapi.

Pia jamaa yangu Le mutuz acha kutulaumu, sisi hata hatujui jamaa katokea wapi ulitaka tuchange hela apelekwe wapi? Unaweza kwenda kuzika mtu Tanga kumbe katokea Angola, huoni kama ni dhambi hapo?

Kama mimi mwongo naomba kama kuna mtu anaemfahamu hata ndugu mmoja tu wa marehemu ajitokeze hapa
Jamaa alikuwa anaitwa nani? itisha rambi rambi tuchangie mzee wa kazi
 
Back
Top Bottom