Mtandao wa majambazi wanaswa, wamo matajiri wawili na mwanafunzi wa kidato cha 5

Power G

JF-Expert Member
Apr 20, 2011
3,886
1,194
POLISI mkoani Shinyanga, wamewatia mbaroni watu wawili wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wakiwa na silaha ambazo wangezitumia katika kufanya uhalifu katika maeneo ya Wilaya za Kahama na Bukombe.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Diwani Athuman, alisema watu hao walikamatwa juzi jioni na kwamba wote ni wenyeji wa Mkoa wa Kigoma.“Mmoja wa watuhumiwa anatoka katika Wilaya ya Kasulu na mwingine wa Wilaya ya Kibondo,” alisema kamanda. Alisema watuhumiwa hao wamekamatwa wakiwa na bunduki mbili aina ya SMG zenye namba UG 6815 na UG 310198 pamoja na magazine tano za SMG ambazo hata hivyo hazikuwa na risasi.

Lakini pia walikutwa na risasi 361 za SMG/SAR na nyingine 16 za G3. Bunduki zao zilikuwa zimetengenanishwa vifaa vyake na kufungwa kwa mpira na baadaye kuzihifadhi katika mfuko wa plastiki,” alisema.

Alisema katika mahojiano nao, watuhumiwa waliwataja washirika wao sita akiwemo mwanafunzi mmoja wa kidato cha tano katika Shule ya Sekondari ya Mwilamvya, wilayani Kasulu. Kwa mujibu wa kamanda huyo, washiriki wengine wa mtandao huo ni pamoja na matajiri wawili wanaofadhili shughuli za mtandao wa uhalifu.Alisema mmoja wa matajiri hao ni mkazi wa Kibondo na mwingine ni mkazi wa Bukombe.

Source: Mwananchi
 
Kigoma kunatisha kwa kutapakaa silaha sababu ya wakimbizi......ni hatari sana!huyo mwanafunzi nae ni balaa!!!sijui sheria inasemaje ukitajwa na washukiwa wa ujambazi na uko mbali na tukio au walipokamatwa.....ushahidi hapo ndio utakuwa issue kuwatia hatiani watajwa...vipi kama
 
Huyu mwanafunzi kwa vyovyote vile wazazi watakuwa wanafahamu na kuhusika katika hii mipangilio.
 
Back
Top Bottom