Askari Feki wanaswa Mkoani Mbeya wakipora mali za Wananchi

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,462
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya katika kipindi cha kuanzia Septemba 28, 2023 hadi Oktoba 02, 2023 limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 22 kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo mauaji, unyang’anyi, uvunjaji, kupatikana na nyara za serikali, kupatikana na bunduki bila kibali, kupatikana na dawa za kulevya na upigaji ramli chonganishi @ lambalamba. Mafanikio hayo yamepatikana kutokana na misako na doria zilizofanywa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya huku baadhi likishirikiana na Jeshi la Uhifadhi [TANAPA] na Polisi Mkoa wa Songwe.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa EZEKIEL RUBEN [28] Mkazi wa Ilolo na JOEL RUVANA [33] Mkazi wa maendeleo Iyela Jijini Mbeya kwa tuhuma za kujihusisha na matukio ya uvunjaji na wizi

Watuhumiwa walikamatwa huko mtaa wa kingani – sokoni jijini Mbeya na kukutwa na mali mbalimbali za wizi ambazo ni TV 3 aina Ailyons inch 32, Contex inch 40 na Zume inch 32, monitor moja ya Kompyuta, key board moja, ipad, headphone moja, stand ya TV, Microphone, cable za Kompyuta, DSTV Decoder, Spika mbili ndefu aina ya Sony, remote mbili za TV.

Aidha, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa 8 kwa tuhuma za kujihusisha na matukio ya mauaji, unyang’anyi na uvunjaji katika maeneo ya Jijini Mbeya, Kasumulu – mpakani mwa Tanzania na Malawi na Tunduma Mkoa wa Songwe.

Watuhumiwa waliokamatwa ni:-
  • HAMIS IBRAHIM [33] Mkazi wa Ilomba
  • JORDAN RAPHAEL NZUNDA [29] Mkazi wa Mlowo Wilaya ya Mbozi Mkoa wa Songwe
  • SALVATORY MAPUNDA [31] Mkazi wa Isengo
  • FURAHA SAMWEL MGALA [24] Mkazi wa Ifisi Mbalizi
  • HAPPY SICHALO [32] Mkazi wa Tunduma Wilaya ya Momba Mkoa wa Songwe
  • BRUCE CHEPELA [32] Mkazi wa Iyunga
  • STEWART AURON [25] Mkazi wa Kiwira - Tukuyu na
  • HAMADY ANTHONY [24] Mkazi wa Mama John
Watuhumiwa wamepekuliwa na kukutwa wakiwa na mali za wizi ambazo ni Pikipiki MC.437 DXY Kinglion, Plate namba ya pikipiki MC 963 DCW, Laptop 18 kati ya hizo hp ni 11 na dell 7, TV moja inchi 32 aina ya LG.

Sambamba na hilo, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa watatu 1. ERICK S/O SINKALA [33] Mkazi wa Ilembo - Sumbawanga 2. SAID ERNEST MIHAYO [41] ña 3. AMOS BENARD NYANZANDU [25] wote wakazi wa Mbagala D’Salaam kwa tuhuma za kupiga ramli chonganishi @ lambalamba kwa lengo la kujipatia pesa isivyo halali.

Watuhumiwa wamekuwa wakiwalaghai wananchi kwa kufanya kafara za kuwaua ndugu zao ili kuwa matajiri na kumiliki mali. Watuhumiwa wamekutwa wakiwa na vitu mbalimbali ikiwemo simu 09 za mkononi aina tofauti za kufanyia uhalifu, mabunda 15 ya karatasi zilizotengenezwa mfano wa noti, chekeche moja ya kufanyia shughuli za uganga, dawa za kienyeji aina mbili zilizofungwa kwenye gazeti na kwenye chupa ndogo, kitambulisho 01, cheti cha uganga wa tiba asili pamoja na vipeperushi viwili vya uganga wa tiba asili.

Washikiliwa kwa kujifanya maafisa wa Jeshi la Polisi Tanzania
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia JUMA SELEMANI MAPUNDA [47] na SAID SAID WANYIKA [27] wote wakazi Songea Mkoa wa Ruvuma kwa tuhuma za kujifanya maafisa wa Jeshi la Polisi Tanzania.

Watuhumiwa walikamatwa katika Mji mdogo wa Mbalizi maeneo ya Stendi ya Tunduma katika Misako inayoendelea wakijitambulisha kwa wananchi kuwa ni maafisa wa Jeshi la Polisi kisha kufanya kazi na walimkamata MECK FRANK MPEPO na kujitambulisha wao ni Askari Polisi kisha kumnyanganya pesa taslimu 700,000/= pamoja na simu 03.

watuhumiwa wamehojiwa na kukiri kufanya matukio kadhaa ya utapeli katika mikoa ya Mbeya, Songwe na Ruvuma kwa kujitambulisha kuwa ni maafisa wa Polisi.

Watuhumiwa wa dawa za kulevya mbaroni kwa kusafirisha na kuuza dawa hizo.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa wanne kwa tuhuma za kupatikana na dawa za kulevya aina ya bhangi kiasi cha kilo 87 na gramu 60.

Watuhumiwa walikamatwa katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mbeya katika Misako inayoendelea wakiwa wanasafirisha na kuuza dawa hizo za kulevya. Watuhumiwa waliokamatwa ni 1. BLANDINA SILVESTER [25] Mkazi wa Tarafani Mbalizi 2. SAMSON SAMWELI @ MGOGO [23] 3. BRUNO ZUBERY @ DUMELA [30] wote wakazi wa Itumbi na 4. JOFREY OMONDI [25] Raia na Mkazi wa Migori nchini Kenya ambaye alikamatwa akiwa na bhangi kilogram 30 zikiwa zimezungushiwa kwenye mifuko mieusi ya plastick na kuwekwa kwenye begi mbili rangi nyeusi.

Mtuhumiwa alikuwa anasafirisha bhangi hiyo kwenye Gari Basi la abiri lenye namba za usajili T.205 DKG aina ya Scania mali ya kampuni ya Premier line akitokea Mwanza Kwenda Mbeya.

Watiwa mbaroni kwa kupatikana na nyara za serikali na silaha [gobole] bila kibali.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa watatu 1. ISIKARI AUGUST @ MBANGA [52] Mkazi wa ubaruku 2. FIKIRI S/O FUNDIKIRA [36] Mkazi wa Ruiwa na 3. PAUL JOHN [43] Mkazi wa ubaruku wilayni Mbarali kwa tuhuma za kupatikana na nyara za serikali na bunduki aina ya Gobole bila kibali.

Watuhumiwa walikamatwa huko eneo la Chamkonda - Upagama ndani ya hifadhi ya taifa ya ruaha iliyopo Wilaya ya Mbarali, Mkoa wa Mbeya baada ya Jeshi la Polisi kuendesha msako wa pamoja kwa kushirikiana na askari wa Jeshi la Uhifadhi [TANAPA].

Watuhumiwa walikutwa wakiwa na nyara za serikali vipande 12 vya nyama ya Mbuni, vipande 05 vya nyama ya Swala, ndege aina ya Kanga 04 na ndege wengine wadogo wadogo 105.

Aidha, watuhumiwa walikutwa wakiwa na silaha moja aina ya gobole lisilokuwa na namba, baruti na vipande 06 vya nondo. Watafikishwa mahakamani mara moja baada ya taratibu kukamilika.
 
Back
Top Bottom