Mtandao inapoweka mnara kwenye eneo lako huwa wanalipa kuanzia Tsh ngapi?

Ongeza24

JF-Expert Member
Mar 5, 2023
239
349
Habari Wana JF,

Samahani naomba msaada nataka kujua gharama wanazolipa Hawa wamitandao wanapoweka mnara kwenye eneo la mtu kuanzia Malipo ya mwanzo na Malipo ya Kila mwezi eneo lipo kijijini mkoa wa Kagera.

Tunaogopa wasije kutupiga hatujui chochote.

Ahsanteni
 
Kagera-Muleba-Kamachumu jamaa alikuwa analipwa laki tano kwa mwezi mnara ulikuwa chini ya kampuni ya vodacom lakini alipewa pesa ya mwanzo ambayo kiasi sijui but kiasi kinatofautiana kulinga na eneo na anayemiliki huo mnara
 
Hao wenyewe ni Tigo eneo lipo kakindo,
 
Uongo. Tigo hamiliki mnara. Bali anapanga kwa Helios tower.

Mnara mmoja wa helios tower ndio unafungwa vifaa vya kampuni zote yaani tigo, voda, airtel wote ni wapangaji wa helios. Ila tigo, voda hawapangi ardhi yako waweke minara wenyewe
Mimi sifahamu chochote ndiyo nipo kwenye kujua hao waliokuja wamesema wanataka kuweka mnara wa Tigo Sasa Mimi unadhani hapa ningesemaje ndugu.
 
Uongo. Tigo hamiliki mnara. Bali anapanga kwa Helios tower.

Mnara mmoja wa helios tower ndio unafungwa vifaa vya kampuni zote yaani tigo, voda, airtel wote ni wapangaji wa helios. Ila tigo, voda hawapangi ardhi yako waweke minara wenyewe
Kwa ujuzi wako Malipo yanakuaje Hilo ndiyo muhimu sisi kujua
 
Kwa ujuzi wako Malipo yanakuaje Hilo ndiyo muhimu sisi kujua

malipo yanatokana na location ambapo ardhi ilipo. mfano sisi tupo ubungo uswahilini ndio tunalipwa laki 5 kwa mwezi.

mnara huo huo ungewekwa kwenye ardhi ya masaki ama kariakoo ungelipiwa kodi milioni 3 ama tano kwa mwezi.

ni kama nyumba za kupanga vile. location ndio inaamua bei
 
Back
Top Bottom