Mtambo wa kuzalisha umeme umewasili?

furahi

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
945
195
Naangalia TBC1 Habari. Mtambo mmoja kati ya mitatu iliyopelekwa kwa matengenezo umewasili. Inanikumbusha 2006 tulipoipokea mitambo ya Richmond kwa mbwembwe. Dah! Sijui!
 
Hii ni danganya toto tu...umesahau kesho ni bajeti ya wizara ya nishati na madini? Watanzania tunadanganyika kirahisi!!!!!

On the red: Spot on. Na kama mtagunduwa walichoonesha ni MABOXI makubwa ya mbao. Waandishi wetu wametuangusha maana sikumsikia hata mmoja akiuliza kuna nini ndani ya maboxi? Ni kweli yalikuwa na mitambo? na kama kulikuwa na mitambo ni kweli ndiyo mitambo iliyopelekwa kutengenzwa? Na inakuwaje mitambo inawasili a day before bajeti ya Ngeleja? Waandishi waliona nyaraka za kusafirisha hiyo mitambo ku-establish ukweli wake?

Kama kuna mtu mwenye mawasiliano na Mnyika, ambipu ili afuatilie huu mchezo wa kuigiza kabla kesho Ngeleja hajawasomea POROJO za kuwa mitambo imetengenezwa na tayari imeletwa!.
 
Yale yale,hiyo mitambo inaendeshwa na gas na ya richmond gas.
Uwezo wa kuleta gas kwa mabomba toka gas inapotoke mdogo sana
maana mabomba ni madogo sana. Sasa jiulize utazalishwa vipi??????
 
Wajanja hawa watu wanaleta sana usanii kuliko kutumia akili,kesho bajeti leo wanatuambia haya sasa tutaamini vipi kama sio ujinga huu......
 
huku wanasema mabomba ya gesi hayakidhi mahitaji,huku unaongeza mitambo huo ni usanii uliotukuka
 
Tanesco wametoa ahadi kuwa mwezi agosti ndiyo mwisho wa mgao baada ya kuingiza majenereta manne yatakayozalisha megawati elfu moja source ITV
 
Ni megawati 100 na siyo 1000 kama ulivyo sema wewe, na majenereta hayo yatafungwa mwenzi Agosti na bado mgao wa umeme upo pale pale.
 
WELCOME!!!! nawasihi TANESCO wawape ushirikiano. MAISHA YETU NI BAHATI NASIBU. thnx ngeleja kwa kutuletea matatizo
 
km mlisikioiza vizuri lile lililoshushwa leo ni la megawati 35 tu kati ya hayo majenereta yanayotarajiwa kuzalisha megawati 100. so bado hazijatimia mia hapo!
 
Nia ya JK na serikali yake ya kifisadi ni kuua kampuni ya Tanesco kama alivyofanya BWM kuua NBC.
 
Ni megawati 100 na siyo 1000 kama ulivyo sema wewe, na majenereta hayo yatafungwa mwenzi Agosti na bado mgao wa umeme upo pale pale.
Ni megawatt 35 bana; kwa muujibu wa mkurugenzi wa hao walioleta hiyo mitambo alipokuwa anaongea TBC1 habari. By the way nimependa hiyo avatar, yani kama akili ya JK + Ngereja + CCM = 0.
 
Nia ya JK na serikali yake ya kifisadi ni kuua kampuni ya Tanesco kama alivyofanya BWM kuua NBC.
Tanesco imekufa zamani inangojea kuzikwa tu. Kuna shirika gani la umma lenye uhai?
 
Back
Top Bottom