Fahari omarsaid
Senior Member
- Feb 8, 2011
- 101
- 13
Kuna ndugu yangu amenipa kiasi cha Tsh 500000 nifanye biashara,je wanajamii wenzangu nifanye biashara gani?nimeisha umiza kichwa sana kuwaza lkn cjafanyikiwa,nisaidieni.
Nakushauri kuanzisha BABA LISHE; Tafuta eneo ambalo utaweza kulisha watu wasiopungua 20 kila siku kwa siku 5 za kazi; unaweza kutafuta ofisi mojawapo, gereji, soko, wauza mitumba etc. Kwa sasa tafuta gharama ya kununua vifaa kama majiko, sururia, containers (vyombo vya kuwekea chakula - zile za plastic); nafikiri gharama hizi haziwezi kuzidi 200,000/= halafu utatumia 100,000/= msingi wa kununulia vyakula na utabakiwa na 200,000/=. Ikiwezekana tafuta mpishi mmoja na wewe mwenyewe utasaidiana nae, Baada ya kumaliza kupika pack chakula kwenye container sawa na idadi ya wateja wako halafu unasambaza. Biashara hii haihitaji mlango wa kukodi (unafanyia nyumbani kwako), hulipi kodi. Mahitaji ya chakula ni ya lazima hivyo soko ni la uhakika.