Mtaji wa Tsh. Milioni 1 hadi 5: Naweza kufanya Biashara gani Tanzania?

Jamaa yangu ana mtaji wa milioni nne,anahitaji kuanza biashara ya vinywaji vya jumla(viroba na vya chupa),pia sigara na vocha za jumla.
1.Je mtaji huu unatosha?
2.Faida yake ikoje?
Hajawai kufanya biashara yoyote ile,natanguliza shukrani nakaribisha mawazo yenu.Anaishi Kahama mjini.

mwambie anicheki 0659116111 nimuelekeze
 
Ni hiv mkuu,inakua kama mikataba ya mabodaboda au bajaji,kwa gharama ya laki tano ni kama mtaji na vitu vya kuanzia,pia sehemu nyingi za chipsi huwa hawalipi kwa miezi,so ni makubaliano kati yako na mwenye eneo.

Napo sema mahitaji namaanisha,Vit,Meza,sanduku la chipsi,pango lasehemu ,viazi,mishkaki,kuku hata wawili kwa kuanzia,kachumbali na mengineyo.

Kuhusu mkataba badala ya kukubaliana nae kumlipa kwa siku au kwa sahani.wewe unamwambia nitafutie 15,000.00 kwa siku vingine ni juu yako.kama sehemu ipo vizur unaweza ukaona wivu kwani kiepe kina pesa balaaa.NB:WATANZANIA TULIO WENGI HATUPIKI SOO NDO TUNAPOJIDAI HAPO.

Kribu mkuu kwa swali zaidi

crukstaa Hata mimi sijakupata sawasawa! Fafanua zaidi. Inamaana hayomahitaji ukishayakamilisha (ikiwamo, tuseme junia la viazi) unatafuta mwuuzaji ambaye atakuwa na wasaidizi wake, yeye atafanya kazi ya kuuza kila siku na atakuletea TShs. 15, 000/- kila siku?
 
Unachokifanya mkuu ni kutafuta vitu vya kuanzia tuu,habari ya wasaidizi ni juu yake kulingana na ukubwa wa biashara eneo husika.

Labda niongelee kwenye pango kidogo,sehemu ya jiko na viti vya kukalia ambapo biashara inafanyika kwa asilimia kubwa huwa wanafanya malipo yake kwa siku,so haitaweza kukubana kua utoe kodi ya miezi sita au mwaka kama kwenye fremu za biashara.

Nawakilisha mkuu na karibu kama una swali lingine
 
Hapo nimekuelewa. Kwa hiyo 15,000/- inabidi kuichukua kila siku biashara inapoisha? Itahitajika kuwapo kwenye shughuli wakati wote wa kuuza?
 
hapo nimekuelewa. Kwa hiyo 15,000/- inabidi kuichukua kila siku biashara inapoisha? Itahitajika kuwapo kwenye shughuli wakati wote wa kuuza?

ili muuzaji awe huru na wewe uendelee na mambo yako sii muhimu kuwepo ila unatakiwa kuweka time line ili uweze ku monitor iyo pesa yako(mfano kila saa moja mpaka saa mbili kila siku ni lazime akuwekee kwenye account yako yeyote ile na una fanya follow up pasipo kua na masihara)

cha muhimu asilimbikize pesa hata ya siku moja,atakuzingua,lakini mengine muache afanye mwenyewe.
 
Nimekupata!!!
 
Habarin watu wa Mungu, Mm ni mwanfunzi toka moja ya vyuo vikuu hapa nchini na muda huu nipo field Mwanza. Nina hela ndogo saana nilitaka niiingize ktk biashara (1MILLION) but hapa sijui biashara gani nianzishe na hela yangu ndogo hyo ili niweze kusaidia wadogo zangu.
MUNGU AWABARIKI SAAANA MNAPOFIKIRI KUNIINUA NAMI KUICHUMI
 
Fanya biaashara ya kuuza nguo na viatu hpo chuon kwenu kwan vijana wengi wa chuo wanapenda kupendeza na kwenda na fashion za mavazi!
 
Ni ngumu kwa pesa ndogo kama hiyo na ulishangaa unakuta tayar umeshafilisika ipo sehemu ya uhakika ukipeleka mil 1 unapewa riba ya kila siku ya sh 5000 na mil 2 ni sh 10000
 
Wakuu muda umefika sisi kama vijana wakitanzania kuwa na aidea ambazo ni sustainale, Tuachane na biashara za uchuzi na tufanye project zenye feature kwaa baadae,

Safari ya maisha yako katika biashara inaanzia hapa, Ni bora unapo kuwa na wazo la biashara kuwa na wazo la kudumu miaka 100 ijayo hata kama hutakuwepo duniani kipindi hicho ila biashara yako itakuwepo,

Watu kama hawa waliangalia mbali sana

1. Michaele Dell- Ingawa hayupo Duniani ila kazi yake ipo, huyu jamaa hakuangalia kwenye kupata faida ya muda mfupi

2. Honda- Hon da hayupo duniani- Ila kazi yake bado ipo

3. Henry Ford- Aliona mbali sana

Wako wengi sana, Kuna post nili iweka humu Kuhusu CHINA ingawa watu hatutaki kuisoma ila ina ujumbe mkubwa sana, CHINA KUNA WATU WANAANZA TRANSPORT COMPANY NA BAISKELI LAKINI MWISHO WA SIKU WANAKUJA KUMILIKI MAGARI MAKUBWA YA MIZIGO huyu aliona mbali na alivyo anza Transport company na baiskeli pekee alijua anako tarajia kuwepo siku moja,

Wakuu turudu kwetu, UNAPO KUJA NA WAZO HAKIKISHA WAZO LAKO HALIISHII NJIANA NA HAKIKISHA NI SUSTAINABLE WAZO,
Mfano

1. Kuuza Mitumba- Hapa hakikisha unataka kuwa wapi siku moja? Je kuuza mitumba Dunia nzima?

2. Ukianza Biashara ya Mugahawa jiulize unataka kuwa wapi siku moja? Je unataka kuwa na migahwa East and Centre Africa?

3. Samaki- Je unataka kufika wapi na hao samaki?

4. Salooni- Je unata kufika wapi na saluni?

5. Tex- Je lengo lako ni nini? Je ni siku moja kuwa na kampuni kubwa ya Tax Africa?

6. Kufuga kuku- Je unataka kuwa na nini katika hii biashara ya kuku?

7. Kufuga ngo'ombe- Je unataka kuwa wapi siku moja na ufugaji ngo'ombe?

WAKUU TUMEKUWA TUKIFANYA BIASHARA KAMA ZIMA MOTO- Leo utasikia anafuga kuku. kesho kaisha acha kuku ana miliki Tex; kesho kutwa kaachana na Tex ana miliki kibanda cha M- pesa, mara kaacha kibanda cha M-PESA sas ana nunua viazi kutoka Iringa na kuleta Dar,

Wakuu kuna thread yangu kuhusu Ni muda upi sahaihi wa kuanza biashara, someni hiyo thread,

UNAPO TANGAZA KUINGIA KATIKA BIASHARA INGIA MOJA KWA MOJA UKIWA NA LENGO LA KUFIKA MBALI SANA NA HIYO BIASHARA YAKO

Umemaliza. Naomba nitumie link ya threa yako hiyo.
 
Back
Top Bottom