Mtaji wa Tsh. Milioni 1 hadi 5: Naweza kufanya Biashara gani Tanzania?

Oky,nimepata kitu hapa ,ngoja nifanyie kazi baadhi ya ideas alafu nitapita kwa kuleta feedback
 
mara nyingi binadam huwa tuna kuwa na ndoto nyingi sana ktk maisha na kuna mipango ming ambayo kina mmoja anakuwa nayo kufanikisha ndoto zake ikiwemo biashara,kaz,cerebrity,investing,franchise,winning a lotary na nyingine nyingi na unatakiwa kuangalia mazingira uliyo nayo.kwa mpango wangu wa biashara ya mtandao,hautaacha kaz yako,na busines plan umetengenezewa na kampun we ni kuifuata tu na kutengeneza kipato cha kimataifa,mtaji kidogo laki saba tu, bidhaa zetu ni za afya na urembo ambavyo ni vit vya matumiz ya kila siku,kwa upande wangu biashara ya mtandao ndiyo mkomboz kwa jamii zetu.

Inekua vizuri ukaelezea hapa jukwaani juu ya hiyo biashara ili watu wajue ni kitugani na hiyo kazi inafanyika vipi na faida yake inapatikana vipi, Lasivyo inakua ngumu kuamini.
 
uliombaje mkopo alafu ndio uka kaa chini kufikiria wazo la biashara. ilitakiwa iwe umepata wazo ndio uombe mtaji.
 
Katika entrepreneurial skills unatakiwa kuwa na business plan kwanza, then plan itagharimu kiasi fulani. Hivyo capital ni swala linalojileta lenyewe. Usipofuata principle hii hutafanikiwa kama mjasiria mali.

Naomba kuwakilisha

Sio capital tu, kuna vitu zaidi hivyo,
Business plan
Capital or location
People demand
Huwezi kufungua biashara ambayo sio mahitaji Ya eneo, kwa mfano ukagungue hardware shop karibu na university wakati kama unafungua stationary na mkahawa ukawa unapiga bao
 
Nina hiyo milioni moja naombeni ushauri nifanye biashara gani itakayo nilipa vizuri na maisha kwenda vizuri.

Msaada wenu ndugu zangu
 
Kuna biashara ya kuwa na cooler na kuuza vinywaji baridi eneo ambalo wapita njia ni wengi mijini. Kinachotakiwa ni kufanya makubaliano na mwenye duka ukawa unalipia kiasi fulani. Ikiwa eneo ni zuri kuna uwezekano wa kuuza creata tatu hadi tano kwa siku za soda na juice. Faida ya Tsh 200 kwa chupa kama kwa siku unaweza kupata faida wastani Sh 20,000 nakuhakikishia mtu umetoka kabisa hapo. Hivyo kwa mwezi wastani wa pato la faida ya lakin tano si pesa ndogo wakati mtaji wako uko palepale. Ukikaa nyumbani hiyo huipati. Cooler za vinywaji barizi zipo ziazopatikana kwa ghrama ya laki nane hadi millioni.
 
Mkuu sijajua mazingira unayoishi, lakini fanya hivi kwani huo mtaji sio mdogo kwakuanzia; Binadamu anakula kila siku hivyo basi kwakuwa binadamu anakula kila siku, fanya biashara ya nafaka kama mchele. Langua vijijini kisha leta mjini nauuze kwa bei ambayo itakufanya usikawize bidhaa, ikiisha rudi tena kijijini kusanya na atilisti fanya mizunguko mi 3 kwa mwezi halafu urudi hapa utupe majibu kwani ni lazima utakua tu!
 
Jamaa yangu ana mtaji wa milioni nne,anahitaji kuanza biashara ya vinywaji vya jumla(viroba na vya chupa),pia sigara na vocha za jumla.
1.Je mtaji huu unatosha?
2.Faida yake ikoje?
Hajawai kufanya biashara yoyote ile,natanguliza shukrani nakaribisha mawazo yenu.Anaishi Kahama mjini.
 
Jamaa yangu ana mtaji wa milioni nne,anahitaji kuanza biashara ya vinywaji vya jumla(viroba na vya chupa),pia sigara na vocha za jumla.
1.Je mtaji huu unatosha?
2.Faida yake ikoje?
Hajawai kufanya biashara yoyote ile,natanguliza shukrani nakaribisha mawazo yenu.Anaishi Kahama mjini.
mtaji unatosha sana kama alishafanya market research na kuona ubora wa soko, competition na mengineyo .. mtaji unaeza tosha lakn factor zingne zikawa kizuizi...
 
mtaji unatosha sana kama alishafanya market research na kuona ubora wa soko, competition na mengineyo .. mtaji unaeza tosha lakn factor zingne zikawa kizuizi...
Competition ni kana hakuna kwa eneo analotaka kufungua,soko kwa jinsi eneo lilivo nadhani atauza kwani wauza maduka wa rejareja, vibaa vipo kibao pia ni barabarani.Kinachompa hofu hajawai kufanya biashara hata mara moja,je inalipa biashara hii kwa waliowahi kufanya na faida yake ikoje.
 
Back
Top Bottom