brayzeking
JF-Expert Member
- Jun 23, 2016
- 259
- 186
Naomba kufahamu tiba ya kidonda cha muda mrefu tafadhali.
Naomba msaada wako doct kwamba mm kila nikiogea brashi basi mapaja yangu yanawasha kwa muda wa DKK(10). Ni kwa muda mrefu SAS hicho kitu kinanitokea mpaka Leo. Yaan naogopa hata kuoga doct.
Dr. sometimes ninapoenda kujisaidia haja ndogo mara nyingi nyakati za usiku ninapotokea usingizini hasa kama nimekunywa maji mengi, nahisi kama simalizi mkojo wangu, yaani nahisi kama umebaki ndani, aidha nikae muda mrefu nijaribu kuulazimisha au nirudi kulala halafu naweza kurudi tena kukojoa tena baada ya muda nakuta ndipo mkojo wote unatoka. Hali hii hunitokea nyakati za usiku tu nikitokea usingizini sio mchana, sina wala sisikii maumivu. Hii ni hali gani na huenda inasababishwa na nini?
KISUKARI NAMNA YA KU-CONTROL SUGAR
Hutokea mara moja moja kuamka sukari iko juu(8-10) nina 55yrs
Aidha kwa sbb zisizoeleweka(Malaria) au kubadilika muda wa kula au chakula hasa matunda/juice au hata kiwango cha chakula .
Hii hutokana na mazingira ya kazi yangu(safari n.k),
Dawa natumia Amarly M2 au Gema 2 asubuhi baada ya breakfast na usk baada Dinner.
Swali langu : je ukijikuta asb mfano sugar iko 9 na unasikia njaa na unahisi mwili uko weak unahitaji kula vizur na ushibe vzr, ni nini cha kufanya ?
1. Kuongeza dawa ? yaani badala x2 unywe x3 ?
2. Kuongeza dawa ? yaani badala 1 tab unywe kidonge 1na nusu x2 tu ?
Tafadhali naombeni USHAURI WENU Dr's na hata wagonjwa wenzangu.
DR. mamaangu jicho moja haoni lina mtoto wa jicho na nimejaribu kwendanae hospital wanasema amechelewa kutibu hivyo hataweza kuona tafadhal naomba ushauri wako daktari
Mm Nina mabaka meusi usoni,na pia miguuni nina madoa meupe,nipe ushauri
Naomba kufahamu tiba ya kidonda cha muda mrefu tafadhali.
Mtoto wangu ana miaka 2 sasa, akiwa na miezi 8-9 alianza kusumbuliwa na matatizo ya ngozi(ngozi kubabuka) hasa mgongoni na sehemu za joints, nikaambiwa hospital tatizo la joto(hali ya hewa),. lakini nilikaa kwa mda kama miezi miwili hali ikawa mbaya nikafanya vipimo vya allergy nikaambiwa asitumie vitu kama jamii ya samaki, karanga na maziwa ya kopo. nimezingatia lakini hali ilipungua kidogo. kuanzia mwezi 4/2016 hadi leo hali sio nzuri na imeanza kuzidi sana hasa 7/2016 yaani mtoto anajikuna hadi mgongo unakuwa mwekundu. kwenye mikono vinatoka viupele vyenye majimaji na kupasuka. sasa nimepita haspitali mbalimbali hadi wananichanganya hasa ni nini tatizo maana kila dr amekuwa akitaja ugonjwa tofauti na dr mwingine. Natanguliza shukrani kwa msaada wako.
dokta mimi naomba kuuliza wapi naweza kupata vifaa vya kuaminika vya EKG machines kwa Tanzania na Oxymetri, gasometri na bei zake kama wafahamu.
Dr nina tatizo la sikio yapata miaka 3 sasa, sikio la kulia linapiga kelele ya mluzi mfululizo, ila haliumi wala halitoi uchafu, na sasa kuna uvimbe umetokea chini ya hilo sikio karibu na taya nao hauna maumivu, nimekwenda muhimbili nimepima kipimo cha uvimbe wa kansa majibu sio, sasa naona na upande wa kushoto napo pembeni ya sikio kunavimba. Tafadhali dr hizi ni sadaka kwako
Doctor Dr. Sajjad Fazel naomba kuuliza kitu
mimi ni kijana wa kiume huwa nahisi ndani ya mwili wangu muscles zinakuwa zinachezacheza tena ni mwili mzima je tatizo linaweza kuwa ni nin na nin tiba yake
natanguliza shukran
Hivi kwa nini mbu hawezi kueneza ukimwi hali ya kuwa anaweza akamnyonya damu mwenye ukimwi at the same time akunyonya na wewe lakini maambukizi usipate.