Mtaalamu wa Dawa na Tiba: Ninakaribisha maswali kuhusu Magonjwa, Tiba na Dawa

Dkt pole sana na majukumu. Kuna katatizo kameanza sio muda mrefu. Nikiamka asubuhi na kufanya mazoezi ya jogging basi nawashwa sana kwenye mapaja baada ya mwendo wa dk kadhaa kiasi cha kushindwa kumaliza na nikisimama tu baada ya sekunde kadhaa hali inatulia. Nini yaweza kuwa shida.
 
Dr, mtoto wangu anasumbuliwa na maumivu ya miguu, nyuma ya kisigino hadi kwenye vidole, kun wakati maumivu yanazidi hadi anachechemea kutembea, ametumia dawa za hospital (Prednisolone na calcimag) bila mafanikio. Msaada tafadhali, ni binti 13 yrs old
 
Habari wakuu,

Nakaribisha maswali yoyote kuhusu magonjwa, dawa, tiba na afya kwa ujumla. Kama una maswali kuhusu ugonjwa wowote, vipi kuishi na magonjwa, kufanya mabadiliko kwenye maisha baada yakupata ugonjwa, matibabu, matumizi ya dawa, matumizi ya dawa pamoja na dawa nyingine au athari zake.

Karibuni sana.

View attachment 361607

Kama umejibiwa maswali na mtu mwingine na haijakufaa ni kosa lako.
Mimi nitajibu maswali zote mwenyewe kama Daktari.

me nataka niwasiliane nae direct...ugonjwa ni siri ya mtu
 
Dr nakuomba kwa maelekezo yako uliyonipa na mizunguko niliyozunguka kwa matabibu nashindwa ni dr yupi ndio bingwa wa matatizo ya uzazi kwa wanawake naomba kwa msaada wako niambie nimuone dr gani au hospital gani ambayo naamini kwangu sasa itakuwa ni fainal
 
Doctor Dr. Sajjad Fazel naomba kuuliza kitu
mimi ni kijana wa kiume huwa nahisi ndani ya mwili wangu muscles zinakuwa zinachezacheza tena ni mwili mzima je tatizo linaweza kuwa ni nin na nin tiba yake
natanguliza shukran
 
Dr nina tatizo la sikio yapata miaka 3 sasa, sikio la kulia linapiga kelele ya mluzi mfululizo, ila haliumi wala halitoi uchafu, na sasa kuna uvimbe umetokea chini ya hilo sikio karibu na taya nao hauna maumivu, nimekwenda muhimbili nimepima kipimo cha uvimbe wa kansa majibu sio, sasa naona na upande wa kushoto napo pembeni ya sikio kunavimba. Tafadhali dr hizi ni sadaka kwako
 
Pole na majukumu docta!Nina mtoto wa dada angu wakiume umri miaka kumi na nne,alipata ajali seat ikambana tumboni nimempeleka hospital wakampa aspirin ila chakushangaza baada ya wiki mbili kuisha kila akila chakula tumbo linavimba!naomba unisaidie je hilo nitatizo gani?
 
pole sana ila ninaushauiri kbla dokta hajaja kukujibu, mrejeshe hospital akafanyiwe vipimo zaidi,
 
Pole na majukumu docta!Nina mtoto wa dada angu wakiume umri miaka kumi na nne,alipata ajali seat ikambana tumboni nimempeleka hospital wakampa aspirin ila chakushangaza baada ya wiki mbili kuisha kila akila chakula tumbo linavimba!naomba unisaidie je hilo nitatizo gani?

Pole na majukumu docta!Nina mtoto wa dada angu wakiume umri miaka kumi na nne,alipata ajali seat ikambana tumboni nimempeleka hospital wakampa aspirin ila chakushangaza baada ya wiki mbili kuisha kila akila chakula tumbo linavimba!naomba unisaidie je hilo nitatizo gani?
 
Mtoto wangu ana miaka 2 sasa, akiwa na miezi 8-9 alianza kusumbuliwa na matatizo ya ngozi(ngozi kubabuka) hasa mgongoni na sehemu za joints, nikaambiwa hospital tatizo la joto(hali ya hewa),. lakini nilikaa kwa mda kama miezi miwili hali ikawa mbaya nikafanya vipimo vya allergy nikaambiwa asitumie vitu kama jamii ya samaki, karanga na maziwa ya kopo. nimezingatia lakini hali ilipungua kidogo. kuanzia mwezi 4/2016 hadi leo hali sio nzuri na imeanza kuzidi sana hasa 7/2016 yaani mtoto anajikuna hadi mgongo unakuwa mwekundu. kwenye mikono vinatoka viupele vyenye majimaji na kupasuka. sasa nimepita haspitali mbalimbali hadi wananichanganya hasa ni nini tatizo maana kila dr amekuwa akitaja ugonjwa tofauti na dr mwingine. Natanguliza shukrani kwa msaada wako.
 
Dr. sometimes ninapoenda kujisaidia haja ndogo mara nyingi nyakati za usiku ninapotokea usingizini hasa kama nimekunywa maji mengi, nahisi kama simalizi mkojo wangu, yaani nahisi kama umebaki ndani, aidha nikae muda mrefu nijaribu kuulazimisha au nirudi kulala halafu naweza kurudi tena kukojoa tena baada ya muda nakuta ndipo mkojo wote unatoka. Hali hii hunitokea nyakati za usiku tu nikitokea usingizini sio mchana, sina wala sisikii maumivu. Hii ni hali gani na huenda inasababishwa na nini?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom