MAMA POROJO
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 4,974
- 785
Hivi kwa nini sisi tunapenda kulirusha rusha sana hili neno "msomi"
Utakuta kuna wengine wanajiita eti "learned" brother au sister (hasa waliosomea sheria). Mimi hili neno "msomi" halinipendezi hata kidogo. Limekaa kimajigambo majigambo. Eti "msomi"....yaani tunapenda visifa vya kijinga jinga tu visivyo na mbele wala nyuma.
Sipendi kujilinganisha sana na Marekani lakini ukiangalia congress ya Marekani, chemba zote mbili za House na Senate, zimejaa watu waliobobea ktk fani mbalimbali - kuna ma PhD. holders kibao lakini hata siku moja huwezi kusikia wakijitambulisha kwa kutumia academic qualifications zao. Kwa mfano Newt Gingrich...jamaa ana Ph.D. lakini kama hujui historia yake huwezi hata kujua kama anayo.
Haya, huyo Gordon Brown hata siku moja sijawahi kuona akitumia Dr.Gordon Brown.....lakini sisi lazima tuweke hizo herufi mbele ya majina yetu. Lazima watu wajue kuwa una u-dokta au ujinga ujinga mwingine. Tuko wa ajabu sana sisi.
Eti "learned" brother or sister...what da fak is that?
Wakuu wengi wa mikoa au wilaya ni wastaafu jeshini.
Lakini utakuta wanaitwa mkuu wa mkoa xyz Kanali mstaafu..... au meja general mstaafu.... Inaudhi kweli kweli.