Msomi Ajitosa Kugombea Udiwani

RRONDO

JF-Expert Member
Jan 3, 2010
51,719
107,833
Msomi Ajitosa Udiwani Kata Ya Magomeni

1.Jengo la ofisi ya CCM Kata ya Magomeni.

2.Ndugu Ally Zawadi {kulia} ambaye ni mhadhiri(Lecturer) wa chuo cha usimamizi wa fedha {IFM} akichukua fumu ya kuwania kiti cha udiwani kata ya Magomeni wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam leo mchana.

3. Ngugu Ally Zawadi akisaini kitabu maalumu mara baada ya kukabidhiwa fomu katika ofisi za CCM kata ya Magomeni mapema mchana wa leo.{Piha:Victor Makinda}

Picha na Habari kutoka kwa MJENGWA BLOG.
 
hivi CCM na ufisadi wao wote wana ofisi mbovu hivi??halafu hawa ndio waboreshe maisha ya mlalahoi!!
 
Hivi kwa nini sisi tunapenda kulirusha rusha sana hili neno "msomi"

Utakuta kuna wengine wanajiita eti "learned" brother au sister (hasa waliosomea sheria). Mimi hili neno "msomi" halinipendezi hata kidogo. Limekaa kimajigambo majigambo. Eti "msomi"....yaani tunapenda visifa vya kijinga jinga tu visivyo na mbele wala nyuma.

Sipendi kujilinganisha sana na Marekani lakini ukiangalia congress ya Marekani, chemba zote mbili za House na Senate, zimejaa watu waliobobea ktk fani mbalimbali - kuna ma PhD. holders kibao lakini hata siku moja huwezi kusikia wakijitambulisha kwa kutumia academic qualifications zao. Kwa mfano Newt Gingrich...jamaa ana Ph.D. lakini kama hujui historia yake huwezi hata kujua kama anayo.

Haya, huyo Gordon Brown hata siku moja sijawahi kuona akitumia Dr.Gordon Brown.....lakini sisi lazima tuweke hizo herufi mbele ya majina yetu. Lazima watu wajue kuwa una u-dokta au ujinga ujinga mwingine. Tuko wa ajabu sana sisi.

Eti "learned" brother or sister...what da fak is that?
 
Mkuu Nyani thank you because hata mimi kitu hicho kina niboa sana. Halafu sasa una kuta "wasomi" wetu wengi wana degree feki.. Tunapenda sifa mno. Siku hizi hata wenye honorary degrees kama Karume wna taka kuitwa "dokta" wakati neyrere aliyekuwa na degree kibao za heshima hata siku moja haku kubali kutambulishwa hivyo. I think ni mchanganyiko wa sifa na watu kujua kwamba wakijitambulisha hivyo wata weza kujikweza zaidi kwa wapiga kura.
 
Msomi Ajitosa Udiwani Kata Ya Magomeni

Ndugu Ally Zawadi {kulia} ambaye ni mhadhiri(Lecturer) wa chuo cha usimamizi wa fedha {IFM} akichukua fumu ya kuwania kiti cha udiwani kata ya Magomeni wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam leo mchana.

Picha na Habari kutoka kwa MJENGWA BLOG.
Msomi my foot, if not just another fisadi in the making. Jamani msomi gani tena huyu, what lecturer can stoop so low - strike me pink, yaani udiwani kwa tiketi ya.... just look at him, yeah take a good good look !
 
jamani tunahitaji wasomi kwenye siasa......tuwape moyo wagombee.....hata udiwani na ubalozi wa nyumba 10-10.....:A S-eek:
 
Hivi kwa nini sisi tunapenda kulirusha rusha sana hili neno "msomi"

Utakuta kuna wengine wanajiita eti "learned" brother au sister (hasa waliosomea sheria). Mimi hili neno "msomi" halinipendezi hata kidogo. Limekaa kimajigambo majigambo. Eti "msomi"....yaani tunapenda visifa vya kijinga jinga tu visivyo na mbele wala nyuma.

Sipendi kujilinganisha sana na Marekani lakini ukiangalia congress ya Marekani, chemba zote mbili za House na Senate, zimejaa watu waliobobea ktk fani mbalimbali - kuna ma PhD. holders kibao lakini hata siku moja huwezi kusikia wakijitambulisha kwa kutumia academic qualifications zao. Kwa mfano Newt Gingrich...jamaa ana Ph.D. lakini kama hujui historia yake huwezi hata kujua kama anayo.

Haya, huyo Gordon Brown hata siku moja sijawahi kuona akitumia Dr.Gordon Brown.....lakini sisi lazima tuweke hizo herufi mbele ya majina yetu. Lazima watu wajue kuwa una u-dokta au ujinga ujinga mwingine. Tuko wa ajabu sana sisi.

Eti "learned" brother or sister...what fak is that?

Mkuu NN
Culture na kasumba inatusumbua, hasa ukizingatia kuwa kwa bongo kupata qualifications kama hizo lazima uchubuke sana. Hii ni mentali ya pale mlimani. utakuta mtu anasomea vitu vya ajabu kweli ili mradi aitwe Dr na one day Prof kama yupo kwenye academic. Waingereza wao hawa mind hizi title bali wanaangalia how well can their education benefit the society via research and job performance. kuna usemi mmoja kuwa "Education without application is useless" ndiyo tulivyo bongo.
 
wasomi hawa hawa kama kina Lowasa, Chenge ( Havard), Prof Costa Mahalu mambo yakiharibika wanasema walipotoshwa na kuingizwa mjini na vijana wasiosoma .

Wanajamvi tusimlaumu mtajwa kwenye hii mada unless kama yeye mwenyewe ndo kapost na kujitambulisha kama msomi. Lakini naungana na wachangiaji kuonyesha kuanza kugundua janja ya vyombo vya habari kuuza walengwa.
 
...
Sipendi kujilinganisha sana na Marekani lakini ukiangalia congress ya Marekani, chemba zote mbili za House na Senate, zimejaa watu waliobobea ktk fani mbalimbali
Hupendi kulinganisha lakini unalinganisha! Kwani kila kitu lazima tuwaige Waamerika/Wazungu et al? Mpeni Kaisari yaliyo ya Kaisari.
 
Hupendi kulinganisha lakini unalinganisha! Kwani kila kitu lazima tuwaige Waamerika/Wazungu et al? Mpeni Kaisari yaliyo ya Kaisari.

Si lazima ila kwa mazuri ni better kuwaiga....tatizo la misomi yetu inayojiita misomi 'haidelivi kitu cha maaana ......inapenda kuitwa dr lakini weupeeeee! cha maana ht km wanaitwa madokta basi wadelive sio dokta mbumbumbu! jina hilo lanini? nick name?
mix with yours
 
Naamini mimi ni msomi. Kwa kufahamu hilo nimekumbuka njia rahisi ambayo Msomi kama mimi hutumia kuwasiliana na wasomi wenzangu ni kupitia machapisho (publications).

Ajabu nimeiona baada ya kutafuta jina la Ally Zawadi ktk google. Jina hili linapatikana kwenye facebook tu!

Huuu ndo usomi?
 
Aisee.... Hawa wasomi wa kwenye.... sijui mjengwa blog... michuzi blog... etc si walewale 'wasomi' wetu?! Watu kama hawa hata ukikamata watano watano kila siku na kunyonga hawataisha! Wasitutibue nyongo....
Siku hizi hata mainjinia wameamka yakhe.. Mtu hakubali kuitwa jina bila ya kutanguliza title ya 'injinia' so and so. Na akistaafu anataka aitwe 'injinia mstaafu' kama mmoja niliyesoma amechukuwa fomu ya ubunge leo.
 
Nadhani huyu bwana anaonewa katika mjadala huu. Inawezekana kabisa yeye hajajitambulisha kuwa ni msomi ila mwandishi amemuita msomi. Na hakuna hata sehem moja aliyojiita yeye ni Dr zaidi ya kusema ni mhadhiri. Labda km tunajadili dhana nzima ya USOMI its ok maana watu wamepitiliza na kugoogle eti yupo kwenye facebook tu! Alah inamaana facebook ni ya jamii fulani peke yake?
 
Ndio Tanzania hii, inaonekana kujipa matitle ni sehemu ya kukubalika na jamii, hata kama huendani na hiyo title. Kinachonishangaza ni kuona kuwa wasomi hao hao wanashabikia namna utawala wa nchi hii ulivyo, na wanafanya kila linalowezekana kujipachika huko ili wafaidi. Ile dhana ya usomi kusaidia maendeleo haipo. Mtu akifika chuo kikuu, anatamani hata avae lile joho mtaani watu wamwone yeye msomi, hao ndio watu wanaojiona wapo katika tabaka lingine kisa degree.
Lakini sio hao tu, utakuta kila nyanja ipo hivyo hivyo Tz, ukikuta wanajeshi wanadhani wengine sio watu, raia hawana thamani, wanaweza wakaanzisha kipigo bila kosa lolote. Wanasheria nao wanajiona wapo kwenye tabaka tofauti. Waandishi wa habari hivyo hivyo, wanaona kama wameshika mpini, ndio utamaduni wa kijinga tulioujenga.
Ninaamini kizazi fulani cha kati hapo kilifanya haya makosa ya kutukuzana na kutafuta sifa za kijinga, matokeo yake kila mtu anamdharau mwenzake. Hata barabarani mwenye gari kubwa anamdharau anayeendesha gari ndogo na mara nyingine kusababisha ajali kwa sababu ya ushindani usio wa kistaarabu. Ninaamini itabidi tuanze elimu ya ustaarabu mashuleni ili jamii zetu ziweze kuelewa kuwa tunapaswa kuheshimiana, si kwa sababu ya mali na utajiri, elimu, taaluma tulizonazo, bali kwanza kwa sababu wote ni binadamu, ambao tunastahili sawa.
 
Mkuu Nyani thank you because hata mimi kitu hicho kina niboa sana. Halafu sasa una kuta "wasomi" wetu wengi wana degree feki.. Tunapenda sifa mno. Siku hizi hata wenye honorary degrees kama Karume wna taka kuitwa "dokta" wakati neyrere aliyekuwa na degree kibao za heshima hata siku moja haku kubali kutambulishwa hivyo. I think ni mchanganyiko wa sifa na watu kujua kwamba wakijitambulisha hivyo wata weza kujikweza zaidi kwa wapiga kura.
Hii ni ngumu saana kusubstantiate km wao wanataka kujiita au wanaitwa!!!
 
Aisee.... Hawa wasomi wa kwenye.... sijui mjengwa blog... michuzi blog... etc si walewale 'wasomi' wetu?! Watu kama hawa hata ukikamata watano watano kila siku na kunyonga hawataisha! Wasitutibue nyongo....
Siku hizi hata mainjinia wameamka yakhe.. Mtu hakubali kuitwa jina bila ya kutanguliza title ya 'injinia' so and so. Na akistaafu anataka aitwe 'injinia mstaafu' kama mmoja niliyesoma amechukuwa fomu ya ubunge leo.

Hapo usomi na hizo blog zinahusiana vipi? Halafu unavyoongea hizo blog as if zilipofikia hapo ni kazi rahisi na pia si lolote. Tunatatizo saana la kudhihaki achievement/success za watu. (nazungumzia blog am not refering to the title wasomi)
 
Msiwasahau akina Dk. Manyaunyau, Prof. Vulata, Dr. Remmy Ongala......yaani shaghalabhagala tu.
 
Back
Top Bottom