Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,476
- 39,995
Na. M. M. Mwanakijiji
Hakuna mgomo unaoitishwa na wafanyakazi ambao unawagawa wananchi mara moja tena kwa ukali kama mgomo wa madaktari. Mara moja mgomo wa madaktari unapoitishwa pande mbili zinazokinzana hujitokeza kwa haraka kama kufuatana kwa radi na ngurumo. Pande hizi zinakuwa na tofauti kubwa sana kiasi kwamba kwa haraka haraka ni vigumu kuona ni jinsi gani pande hizo mbili zinaweza kupatana au hata kukaribiana na kutafuta suluhu.
Upande mmoja kunakuwepo na wale ambao mara moja wanachukulia uamuzi wa madaktari kugoma kuwa ni mashambulizi dhidi ya afya za wagonjwa. Hawa huamini kuwa hakuna mazingira yanayoruhusu madaktari kugoma kwa sababu kufanya hivyo ni kupitisha sentensi ya kifo kwa wagonjwa ambao wanawategemea madaktari hao. Hivyo, upande huu mara nyingi hujenga hoja kuwa madaktari waendelee na kazi wakati matatizo yao yanashughulikiwa kwani kutofanya hivyo ni kuhatarisha maisha ya wagonjwa na watu wasio na uwezo.
Hoja ya hawa pia inaupande unaotokana na kile kinachoitwa wito wa udaktari yaani ni miongoni mwa kazi ambazo toka enzi na enzi zilionekana zina wito wa pekee. Miongoni mwa kazi nyingine zilizoonekana ni za wito ni zile za kidini, uwakili na ualimu. Kiongozi wa dini anatakiwa kutoa huduma ya kiroho bila kujali anayempatia huduma hiyo ni mtu wa namna gani, wakili anatakiwa amtetee mtu kwa uaminifu wa hali ya juu na mwalimu anatakiwa kumfundisha mtu mjinga na kumwondolea ujinga wake hata kama kufundishika kwa mtu huyo ni kugumu kupita kiasi.
Hata hivyo, tofauti na kazi hizo nyingine za wito ni kazi ya udaktari kwa namna ya pekee ambayo ina kitu kingine kinachokosekana kwenye hizi kazi nyingine uhai na kifo. Madaktari wanahusika na afya za wagonjwa na hivyo maamuzi yao (mazuri au mabaya) yana matokeo ya moja kwa moja kwa mwanadamu mwingine au wanadamu wengine. Daktari akigoma kusaidia mama mja mzito anayejifungua ambaye mtoto wake amekabwa na kitovu (umbilical cord) mama na mtoto maisha yao yanaweza kuwa hatarini.
Wakili akikataa kumtetea mtu au akimtetea mtu vibaya kuna uwezekano uamuzi mbaya (adverse decision) kwa mtu huyo unaweza kugeuzwa katika rufaa na kumpa nafasi nyingine. Mtu aliyefundishwa na mwalimu mbaya ana uwezo wa baadaye kupata nafasi ya kufundishwa na mwalimu mzuri; mtu ambaye amechukizwa na mafundisho ya kiongozi wa dini yake anaweza akaamua kwenda na kukumbatia mafundisho ya dini nyingine. Mtu ambaye amekufa kwa sababu daktari ameshindwa kufanya kitu au amekifanya vibaya hana rufaa wala nafasi ya pili.
Ni kutokana na hili ndio maana watu wanaoamini katika kiapo cha Hippocriti wanaamini kabisa kuwa madaktari hawatakiwi kuchukua uamuzi wowote ambao utasababisha madhara kwa mgonjwa kwani ameapa kutomsababishia madhara mgonjwa. Hivyo, kwa msingi wa hoja hii mgomo wa madaktari ni mwiko kabisa na hakuna mazingira yoyote ambayo mgomo unaruhusiwa. Kwamba, hata kama madaktari wanafanya kazi katika hali mbaya kiasi gani, hata kama madaktari wana matatizo ya namna gani yanayotokana na maslahi yao, na hata kama madaktari wananyanyaswa vipi na mwajiri wao jukumu lao la kwanza ni kwa mgonjwa na wanatakiwa kufanya lolote lile kuhakikisha kuwa wagonjwa hawadhiriki. Mgomo unavunja utakatifu (the sacredness) wa kiapo chao.
SOMA ZAIDI KWENYE FIKRA PEVU
Au Download: