Msimamo wa CCM kuhusu tuhuma za kuhusika na mauaji ya wana-CHADEMA

It is a very simple logical which does not need one to be an intellectual to understand: Kama mauaji haya ni ya kawaida kwanini wauwawe wa upande mmoja tu,kwanini wasiuwawe na wa CCM?
 
Kwanza, si busara hata kidogo kuihusisha CCM katika matukio hayo, kwani uchunguzi unaofanywa na vyombo vya dola umeshindwa mpaka sasa kuhusisha matukio hayo na siasa, badala ya kuyahusisha na makosa ya jinai ambayo hufanywa na watu kwa malengo tofauti na yale ambayo Ndg. Mbowe anataka kuwaaminisha watu.

Nape ameshindwa pia kuonesha wazi motive ya mauaji haya ambayo yeye inaonekana anaijua na ndiyo maana ana 'Refute' kauli ya Mh. Mbowe. Nape na Serikali ya CCM wamevifanya vyombo vya dola kutoheshimika na kuaminika na wananchi, hasa pale vyombo hivyo vinapotoa kauli kuwa 'Upelelezi bado unafanyika kugundua sababu za mauji, ila mauaji haya hayatokani na siasa': Kauli kama hizi zinafanya Polisi na Kauli kama ya Nape kuwa Unreliable. Unapofanya uchunguzi maana yake ni kwamba huna taarifa ya kilichojiri na ndiyo unakitafuta hivyo all possibilities must be on the table.

Pili, CCM haijawai, haiwezi, na haitakuja fanya jambo lolote lenye lengo la kuvuruga Amani na Usalama wenye utulivu ndani ya taifa letu, hivyo uzushi na usingiziaji uliofanywa na Mtu Kama Ndg. Mbowe, si vema kuuacha kimya, badala yake nimetumia wasaa Huu muhimu Kujibu, na kutoa ufafanuzi ili Kuupa umma wa watanzania habari sahihi.

Nape ulitakiwa kutumia busara zaidi ya maneno haya. Hivi ni nani asiyejua leo hii kuwa CCM ndiyo chanzo cha uvunjifu wa amani?. Ni chama gani kinaweka vijana kambini kuwafundisha kufanya umafia kwa wananchi na kuwatisha nyakati za uchaguzi. Ni chama gani huwa kinabadili matokeo ya kura na kusababisha watu kuuwawa au Ofisi kuchomwa moto kama tulivyoona Shinyanga?, je haya si matokeo ya kuvunjika kwa amani?. Ni chama gani kimekuwa kikiteka watu wasiokubaliana nao na ama kuwaua kama tulivyoona Igunga ama kuwatesa?. Ni chama gani ambacho kimekuwa kikiagiza vyombo vya dola kupiga wananchi kwa kisingizio cha kulinda amani?.

Ni chama gani ambacho Kada wale alituma mtu akamuue katibu wa wa kata ya Isamilo kwa ajili ya siasa?.

Ningekuwa Nape ningesema hivi "Kwa kuwa CCM ni chama kikubwa na kinavutia watu wa aina mbalimbali wakiwamo wahalifu, CCM haitakuwa tayari kuwalinda watu hawa kama watabainika kuwa ni kweli wamevunja sheria za nchi au kutenda jinai, hivyo tunaiomba CDM iviachie vyombo vya dola viendelee kufanya kazi kuwagundua watu hawa na kuwafikisha katika vyombo vya sheria" - Kauli hii Ingeonekana imetolewa na Chama kinachoongoza nchi ambacho kina dhamana ya kuhakikisha usalama wa raia na mali zake.

Ni aibu kwa Chama kama Chadema kujitahidi kwa nguvu zote kujaribu kuficha ukweli wa mauaji yanayotoa roho za watanzania wenzetu kwa kuyapa sura ya kisiasa. Hizi ni juhudi za makusudi za kutaka kuficha ukweli wa kinachotokea.


Ni aibu kwa chama kama Chadema kujaribu kutumia mauaji mabaya kama haya kutafuta mtaji wa kisiasa. Huku ni kuonyesha jinsi gani wamefilisika kisiasa mpaka wanafikia mahali pa kuamini kuwa wanaweza kutumia chochote kama mtaji wa kisiasa, vikiwemo vifo vya watanzania wenzetu. Huku si kufilisika tu ila kwakweli ni unyama unaotakiwa kulaaniwa na kila muungwana.


Nape Moses Nnauye
Chama Cha Mapinduzi
Ideology and Publicity Secretary


Nape wewe ndiyo unaleta siasa hapa. Sijaona sehemu yoyote ile CDM inapotumia mauaji haya kisiasa. Lugha uliyotumia ni lugha ya mtu aliyepoteza rational thinking capacity. Hebu fikiria, Igunga walikufa watu, vyombo vya dola vimesuasua kuwatia kuwatafuta wahusika, Wabunge wa Mwanza wamekatwa mapanda mbele ya Polisi, Wananchi wanne wamekutwa wamenyongwa Arumeru, siku tatu baadae Mwenyekiti wa CDM kakatwa spinal cord. Hivi tufanye kwamba matukio haya yote ymewakuta wana-CCM, Polisi wangesema hayahusiani na siasa?. Si tungeona utaratibu unafanywa wa kuwakamata wahusika na wasio husika na hata kutishia kuifuta CDM?. Nape hebu kwa mfano leo hii mwenyekiti wa CCM Usa River anakutwa amechinjwa (god forbid) utakuja na kauli kama hii?. Kauli yako Nape haijengi inabomoa. Na vile vile haikisaidii Chama Cha Mapinduzi na serikali yake bali inavididimiza.

Nape ulitakiwa kuja na kauli iliyo responsible zaidi yenye kulenga kulinda amani na kujenga kuaminiani siyo yenye kulenga kuanzisha political game kwenye sensitive issue kama hii. Kumbuka kuwa wafiwa bado wana uchungu na ndugu zao hata ipite miaka hamsini. Kauli yako hailitendei favour jeshi la polisi hata kidogo ila inaongeza ugumu wa kazi yao. Kauli yako haiponyi machungu ya wafiwa bali inajenga hisia za visasi. Kama hawa ndiyo wasemaji wa CCM basi nchi ipo rehani. Ipo wapi busara ya Mwalimu????
 
Nape nakuonea huruma maana wewe umewekwa km chambo vuvu zela wezako wote washasoma alama za nyakati wanajenga pakukimbilia nakwambia nakuhakikishia nape nakurudia nchi hii 2015 mtanyongwa kwa damu zawatu
 
Hatuna akili ya ngiri eti tuamini kuwa CCM watafanya uharamia halafu watangaze kupitia Nape Nnauye kuwa wameufanya.
Hii kukanusha ni kama mtoto mmoja anapompiga mwenzie,anachofanya ni kuhamaki siyo mimi hata kabla hujamwuliza ili kuficha uovu.Nape angelipelekwa shule kama viongozi wake wangekuwa waumini wa shule ama Elimu Dunia.
 
Si muda mrefu hawa tutawazika wazima wazima! It is just a matter of time! CCM siyo Mungu hata itawale milele. Vyama vyote vya siasa Africa vilivyo-take over baada ya wakoloni mwishoni mwa miaka ya 1950 na mwanzoni mwa miaka ya 1960 kusini mwa Sahara imebaki CCM tu. Very soon tutawazika wazima wazima. VERY VERY SOON!

kwel mkuu Waangalie KENYA,ZAMBIA,MALAWI,..n.k Shame on 'EM
 
Kwa tamko hili Nape is Vampire! hata kama kusoma hujui basi kuona picha pia anashindwa!

Mwanangu (3yrs) ananiuliza: "Baba ulikuwa wapi"
Namjibu: Nilikwenda usa kwenye mazishi ya kiongozi wetu wa chama
Mwanangu:Amekufa? alikuwa anaumwa nini?
Namjibu: hakuwa mgonjwa bali ameuwawa na watu wasiojulikana
Mwanangu:Ni ccm hao watakuwa wamemuua!

Sasa ikiwa mwanangu kwenye age kama hii anawezakuhisi hivi Mjinga Nape huyu anajivua ubinadamu wake kijinga hivi ili iweje! Ikitokea ukatangulia mbele ya haki leo utamweleza nini Muumba wako?? Stupid Nape!!
 
Hili la kuwauwa binadamu wenzenu hivi kwa sababu za kilevi tu tena ulevi wenyewe wa ujambazi wa rasilimali zetu ! Mtalipa tu na kama si hapa duniani basi kwa Mungu! shetan wakubwa nyie "wewe na aliyekutuma kuandika tamko hili."
 
Huyu Nape ndiyo yule asubuhi alikuja kuchota watu akili humu JF?

Kumbe uwezo wa dogo Nape ndiyo huu?
 
Nape,
Nia aibu kwa CCM kuficha njama za mauaji ya Mwakyembe aliyoyapeleka mbele ya vyombo vya sheria na kuwataja makada wa CCM kujihusisha na uchafu huo Morogoro

Ni aibu CCM kutotoa tamko mtoto wa Mengi alipotaka kubebeshwa kesi jambo lilofanywa na makada wa CCM tena walioomba ubunge.

Ni aibu kwa CCM na serikali yake kutotoa maelezo juu ya vinasa sauti ndani ya chumba cha Dr Slaa

Ni aibu kwa CCM kuficha ukweli kwa jaribio la kutaka kumuua aliyekuwa spika wa bunge Mzee S, jaribio liloratibiwa na makada waandamizi wa CCM ambao wako huru na kwenye uongozi wa chama

Ni aibu kwa CCM kutotoa tamko kuhusu vifo vya akina mama na watoto vinavyotokana na ukosefu wa huduma bora huku makada wa CCM katika ngazi za uwaziri, ubunge wakijihusisha na ufujaji, ubadhirifu na wizi wa fedha za umma.
Makada hao wanafichwa kwa vigezo vya kustaafishwa, kubadili baraza la mwaziri n.k
Ni aibu CCM kutotoa tamko la kumlaani mwenyekiti wa chama kwa kulea ufisadi na mafisadi

Ni aibu kwako Nape kutolaani mauaji ya wanasiasa kule Igunga, Arusha, Kibaha n.k huku ukikimbilia kukisafisha chama chako ambacho uharamia wa kupora mali, ufisadi visasi na majaribio ya kuuana sasa ni sehemu ya kazi za kawaida za chama.
 
Ushauri wangu kwa Nape,nikuombe utambue kuwa kuna hoja ya serikali na ya chama sasa katika hili sijakuelewa umelizungumzia kama nani? Je msemaji wa serikali au chama cha mapinduzi? nakuomba uwe na tafakari kabla ya kuzungumza unayo zungumza na kujipima pia.
 
Nepi kweli nyie mmeonewa hamhusiki na mauwaji yoyote na mnaushahidi kuwa CDM kupitia mwenyekiti wake Mbowe kawasingizia si mumpeleke mahakamani. kwa nini hilo halikuwa msimamo wa chama?
 
Usijeshangaa Nape ndo IGP na DCI. Hawa wenyewe akina Mwema na Manumba wapo sababu wapo, hawajui wafanye nini! Ndiyo wafanye nini wakati chama kimeshika hatamu?


Inashangaza kuona kada wa chama anatoa tamko linaloihusu jeshi la police,hv kinamanumba kz imewashinda.Sasa napata picha ni kweli policesisiem wanawaham wauwaji,ila kwakuwa jeshi le2 halipo huru ndo vile watoto wa mama kina nape wanadantia mambo.
 
NAPE kwisha kazi! Ni kelele za Mfa maji tu. CDM haiui kimwili mtu yeyote, inaua DHANA,MTAZAMO,FIKRA NA MAZOEA yote ya KIFISADI.Na hatimaye CCM itakufa.
Nape ni kilaza kweli hawezi kujenga hoja .Nape my young brother why are you unrealistic you can think hata kidogo
 
Hana akiri na anafikiria kwa kutumia masaburi. umma upi utamwamini mtu kama Nape, wakati yeye mwenyewe amanusulika kufa juzi tu. ukweli ni kwamba ccm kuna MAJAMBAZI, mfano mzuri ni tukio la mwanza wabunge kukatwa mapanga, watu wale wanajulikana na magari yao yalithibitisha hilo kuwa ni wanaccm pasipo shaka hata kidogo.
 
Back
Top Bottom