Msichana auwawa kikatili na mumewe Dar

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,322
33,126
MSICHANA Khadija Daudi (22), mkazi wa Mbagala Charambe aliuawa kikatili na mumewe kwa kuchomwa na kisu mgongoni kwa kile kilichodaiwa kuwa ni baada ya kukataa kuamka usiku kwenda kuokota embe.

Tukio hilo la kusikitisha lilitoka mwishoni mwa wiki huko Mbagala jijini Dar es Salaam.


Ilidaiwa kuwa chanzo cha kifo hicho ni mume wa msichana huyo aliyetambulika kwa jina la Shariff Kondo alimuamsha marehemu kumtaka aende nje ya nyumba yao majira ya saa kumi kasoro usiku, aende akaokote embe lakini marehemu aligoma na kudai kwa kuwa ni usiku asingeweza kwenda nje kufanya kazi hiyo.



Inadaiwa kuwa kutokana na majibu hayo mumewe alikasirika na ndipo alipochukua kisu na kumchoma nacho mgongoni.

Baada ya kuchomwa kisu hicho alipiga kelele na majirani walijitokeza kumpa msaada wa kumkimbiza Hospitali ya Temeke huku akiwaambia kilichomtokea kwa mumewe huyo.


Kwa bahati mbaya msichana huyo alipoteza fahamu na kufariki mara baada ya kufikishwa hospitalini hapo.


Wakithibitisha tukio hilo baadhi ya majirani wa marehemu huyo, wamedai kuwa walisikia kelele za kuomba msaada katika chumba cha mpangaji mwenzao na mara baada ya kuingia ndani kwake kujua kilichotokea ndipo walipokuta kitanda chake kimelowa damu na huku akiugulia maumivu.

Majirani hao wamesema kutokana na hali hiyo walikwenda kutoa taarifa kituo cha polisi na baadhi yao walijaribu kumtafuta mumewe lakini hakupatikana ndipo walipokwenda kumwamsha baba mzazi wa msichana huyo anayeishi Charambe na kumuelezea yaliyompata binti yake.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Liberatus Sabasi, amesema kuwa, tayari mtuhumiwa aliyehusika na tukio hilo tayari ameshakamatwa yuko katika kituo cha polisi cha Chan’gombe na anatarajiwa kufikishwa mahakamani leo.




http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=3556198&&Cat=1
 
Jamani kiswahili kimenichanganya kidogo..! Hivi neno msichana maana yake nini? Ni umri? Ni kuolewa? Au?? Chombo cha habari kinaposema "Msichana auwawa kikatili na mumewe Dar" ni sawa kweli? Haikupaswa kuwa "Mke auwawa na mumewe kikatili.."?
Naombeni ufahamisho
 
Jamani kiswahili kimenichanganya kidogo..! Hivi neno msichana maana yake nini? Ni umri? Ni kuolewa? Au?? Chombo cha habari kinaposema "Msichana auwawa kikatili na mumewe Dar" ni sawa kweli? Haikupaswa kuwa "Mke auwawa na mumewe kikatili.."?
Naombeni ufahamisho

wasichana wote ni wanawake, lakini wanawake wote si wasichana
 
Back
Top Bottom