Taarifa imechelewa kwa sababu Marehemu alikuwa anaishi Dar ES salaam na mimi naishi nje ya bara la Afrika, ilikuwa kama bahati tu, baada ya kuona kwenye MSN kuwa yupo online, baada ya kuulizia kumbe alikuwa Binti yake na ndiye aliyenipa taarifa ya msiba.ooh!
r.i.p mpenzi wa islam
LAKINI.........
MBONA TAARIFA IMEKUJA KWA KUCHELEWA SANA?
Inna Lillahi wa Inna ilayhi Raj'oon
Verily to Allah we belong & to him we shall return
Taarifa ya Msiba wa MwanaJF
Kwa niaba ya Familia ya Ndugu yetu na mwanachama mwenzetu Aliyekuwa akijulikana kwa jina la Mpenzi wa Islam, wanasikitika kutangaza kifo cha ndugu yetu Mpenzi wa Islam Kilichotokea tarehe 19th - March - 2010.
Marehemu aliuguwa ghafla moyo na akafariki na kuzikwa siku hiyo hiyo, mjini Dar es salaam. Taarifa hizi nimeletewa na Binti yake na Marehemu.
Marehemu alikuwa si Swahibu yangu tu, ila alikuwa ni ndugu yangu na mshauri wangu wa karibu sana. Huu ni msiba mkubwa kwa kweli.
_____________
"Surely Allah takes what is His, and what He gives is His, and to all things He has appointed a time...so have patience and be rewarded." [Bukhari] -
Dhikr & Patience are the most befitting Remedy
Mkuu Tiba, ni kweli maneo yako, lakini kwa kuzingatia kuwa yeye mwenyewe (Marehemu), tangia uhai wake hakuweza kuweka bayana Jina lake halisi wala nasaba yake basi itakuwa si haki kuliweka hapa jina lake na nasaba yake. Kwa kweli itakuwa si kumtendea haki marehemu. Naomba turidhike kama mlivyo ridhika kulikubali jina lake la kupanga.X-PASTER, wanafamilia na wana JF poleni kwa kuondokewa na mpiganaji. Mungu Ailaze mahali pema peponi roho ya marehemu kama kweli anastahili. Je katika mazingira kwamba mwana JF sio hai tena kuna haja ya kuendelea kuficha identity yake halisi? Ningependekeza jina lake halisi litajwe kwani hakuna madhara yoyote yatakayomkuta katika mazingira kwamba hayupo pamoja nasi tena hapa duniani.
Tiba
Mkuu Tiba, ni kweli maneo yako, lakini kwa kuzingatia kuwa yeye mwenyewe (Marehemu), tangia uhai wake hakuweza kuweka bayana Jina lake halisi wala nasaba yake basi itakuwa si haki kuliweka hapa jina lake na nasaba yake. Kwa kweli itakuwa si kumtendea haki marehemu. Naomba turidhike kama mlivyo ridhika kulikubali jina lake la kupanga.