Msiba Wa Mwana JF

X-PASTER

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
11,610
1,810
Inna Lillahi wa Inna ilayhi Raj'oon
Verily to Allah we belong & to him we shall return

Taarifa ya Msiba wa MwanaJF


Kwa niaba ya Familia ya Ndugu yetu na mwanachama mwenzetu Aliyekuwa akijulikana kwa jina la Mpenzi wa Islam, wanasikitika kutangaza kifo cha ndugu yetu Mpenzi wa Islam Kilichotokea tarehe 19th - March - 2010.

Marehemu aliuguwa ghafla moyo na akafariki na kuzikwa siku hiyo hiyo, mjini Dar es salaam. Taarifa hizi nimeletewa na Binti yake na Marehemu.

Marehemu alikuwa si Swahibu yangu tu, ila alikuwa ni ndugu yangu na mshauri wangu wa karibu sana. Huu ni msiba mkubwa kwa kweli.
_____________

"Surely Allah takes what is His, and what He gives is His, and to all things He has appointed a time...so have patience and be rewarded." [Bukhari] -
Dhikr & Patience are the most befitting Remedy
 
OMG...this is very hard to take....may his soul rest in peace...amen
 
Apumzike kwa amani..ukiwa mtu wa karibu nakupa pole na pia jamii nzima ya JF kwa msiba huu wa mwanachama mwenzetu!
 
Nakumbuka kuona jumbe zake nyingi humu ndani hasa kwenye mijadala ya dini. Tuwape pole wafiwa na jamaa zake wa karibu. Mungu alitoa na ametwaa. Ampe mapumziko mema huko alikotangulia.
 
oh ! mungu ailaze roho ya marehemu pema peponi, tuko njiani na hali tuko vitani. siku moja tutakutana tena.
 
Inallahwainailah rajiun, Mwenyezimungu amghufirie mazambi yake na amrehemu pamoja na wote waliotangulia mbele ya haki na atusamehe mazambi yetu tulie hai.
 
Mola amsamehe makosa yake na amkubalie yale mema aliyoyatenda.
Poleni sana wafiwa,Mola awajalie subra.
 
polen sana wafiwa
pole ndugu nafikiri wakati muafaka wa member waliobaki kurekebsha
maisha yao na kujua muda saa wakati wowote wanawezwa tangulia mbele
ya mwenyezi mungu...so wkaati muafaka wa mliobaki kurekebisha maisha
yenu na kuachana na uovu wote ambao mwenyezi mungu apendwzwi nayo

mwnzettu ameondoka we utaondokaje???polen tena wafiwa
 
.........Ohhh jamaniiiiii!!! Namkumbuka huyu kaka alikuwa maarufu sana kwenye jukwaa la dini kule........eheheheheheh masikini alikuwa anapigania kweli dini yake. Mungu amrehemu kwa kweli, siamimi mie bado kama amekufa. Poleni sana wafiwa, Bwana alitoa na Bwana ametwaa. Apumzike kwa amani huko alipo.
 
mungu amsamehe makosa yake na amuinuie katika daraja peponi. ameen

wafiwa poleni sana na mungu awajaalie moyo wa subira
 
Hakika sisi ni mavumbi
Na mavumbini tutarudi.
Roho ya marehemu ipate Rehema ya Mungu, apumzike kwa amani.

Poleni sana wafiwa, Pole sana X-paster na poleni sana wana JF wote kwa ujumla kwa kumpoteza mwanaJF mashuhuri na maarufu.
 
ooh!
r.i.p mpenzi wa islam

LAKINI.........
MBONA TAARIFA IMEKUJA KWA KUCHELEWA SANA?
 
Back
Top Bottom