Msiba wa Jasusi Agustino Mahinga umetufundisha mengi. Kuna mambo mengi ya kufanywa na Diwani Athumani

Hakuna jambo jema litakalofanyika hapa Tanzania under Magufuli.

LaZima nchi isubiri huyu Rais aondoke madarakani ndio itawezekana kulisimamisha taifa tena.

Economy is dead. No jobs no vision no plan.

Zidumu fikra potofu za Mwenyekiti ndio iliyopo.
And we are not going anywhere.
Diwani ana kazi yabkupambana Na chadema na kuhakikisha kura zinaibiwa na kupoteza wanaompinga Rais mitandaoni.

Sidhani kama an jambo lingine.

Na hao/ hio taasisi nzima ya TISS ni trash.
How they ended up allowing Magufuli to become President.
Its a Shame.
Msingi bora kabisa aliotuachia Watanzania ni kukubaliana kutokubaliana, huku tukibaki na dhana ya kuheshimu utu wa yeyoye ile.

Baadhi ya wazee ukiongea nao au hata makala mbalimbali tukisoma, ni kama 1985, Mwl. Nyerere hakuwa kalenga kumwachi nchi mzee Mwinyi. Yeye alidhani Dr. Salim Ahmed Salim angetufaa. Baada ya maamuzi ya wanaCCM wakati huo, Nyerere aliondoka madarakani na kumkabidhi kijiti mzee ruksa.

Kuna mambo mengi mazuri JPM anafanya, huenda hatakidhi matarajio ya kila Mtanzania na kuna huenda hata mawazo tunayijadiliana hapa wasilazimike kuyafuata.

Lililo ndani ya uwezo wetu ni kushauri what is the best practices kwa kulinganisha wenzetu wanafanyaje huko duniani. Ila utu na kuheshimu mkubwa kwa mdogo ubaki kama sehemu ya maadili ya Utanzania.
 
YEHODAYA pokea bonge la LIKE mkuu, umeshusha Tanzanite kama siyo dhahabu kwenye hii post yako. Nadhani wahusika watapita kuona hapa haya madini. Kwa hakika Tanzania itapiga hatua kwa kuwatumia watanzania wenye maono na moyo wa kuitumikia Tanzania. Hoja zako hakika zinaweza kabisa kufanyiwa kazi, vyuo vyetu vinaweza kutumika kupandikiza mawazo ya kibunifu na udhalendo. Suala si ajira bali ni watu kuwa wabunifu na kutengeneza miradi itakayo ajili vijana. Nimebarikiwa sana na andiko lako.
Vyuo vyetu si tija havifundishi kukabiliana na changamoto na mabadiliko ya mifumo ya maisha.Kuwa na vyuo vikuu vingi nchini visivyo na tija kwa muhimu timu ni kuongeza idadi ya masikini nchi.Mifano hai pana ndugu mume amesomea udokta lkn anaendesha Uber mke amesomea ualimu amefungua saloon Hawa wote Wana loans bord lengo la kusoma ili wakajiriwe lkn sababu ya ukosefu wa ajira tegemeo wangeingia ajira wasizotegemea ili maisha yasonge, means hapa Kodi yetu ya mkopo wa elimu imepotea.Gharama ya kumsomesha mtu mmoja chuo ambae akimaliza anarudi kuendesha bodaboda mtaani au kuuza juice mtaani Kama ingewekezwa kwenye kutoa elimu za ufundi na ujasilimali ingeweza saidia vijana wengi wakapata elimu ya ufundi.Mfano unampa loans milioni 9 mwanachuo mmoja Hali ingetumika kuwasaidia vijana si chini ya 100 kupata elimu ya ufundi kwenye vyuo vya maendeleo.
 
Hayo unayoongea ndio Rwanda wanaaply kwa kutap resourceful youth who are innovative. South Korea Ali apply ndio yamemfikisha kwenye dunia ya Kwanza.

Kwa ufupi ni Mambo yanayowezekana lakini sio kwetu Tanzania

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna mambo unamuonea Mkurugenzi kumrundikia kila kitu.Ni.kwamba private sector wetu hawana vitengo vya TISS vya Kwao mfano wajapan private sector baada ya Vita kuu ya pili ya dunia walipigika wakawa so frustrated private sector ikajipanga kwenda kuiba teknologia Marekani wakatuma madoctor na maprofesa viwandani Marekani kuomba kazi za kufagia,kudeki nk wamarekani wakapna wajapani Ni cheap labour wakawaajiri viwanda I kibao kumbe walipelekewa walikuwa mainjinia nk Tena wenye akili nyingi wakaiba teknolojia wakarudi kwao kuanzisha Vita ya viwanda

Walibadili sera kuwa Sasa watapigana Vita ya dunia ya kibiashara na viwanda na waliweza

China imeendelea kwa wizi wa teknolojia Hadi Leo .Walianza kuiba teknolojia Urusi baadaye wamefanya Kama kitu official wanaishi kwa kuiba teknolojia na kumodify kidogo tu kuepuka mikesi .Wanaishi kwa wizi

Vijana wetu wanaenda Soma kila Kona ya dunia lakini hawaibi teknolojia wanaturudia na kingereza tu kilichonyooka!!!

Private sector ichangamke iajiri vijana bright iwape assignment
Wakati Mzee Paul Bomani akiwa Rais wa Victoria Federation walikuwa na ofisi ya mauzo ya pamba na products za pamba Uingereza. Mauzo ya pamba na faida yaliweza kujenga jengo la kwanza la kisasa mjini Mwanza nyakati hizo miaka ya 70 (kwa sasa KCB Bank tawi la Mwanza wamepanga).

Kuna jambo la kufanya ili mifumo ya masomo na mahusiano kati ya public na private sector yalenge kukuza biashara na uchumi wa nchi hii.

Naomba nikushirikishe nukuu moja toka chapisho moja, walau kupata picha kuwa uchumi ni kila kitu kama msingi na uimara wa taifa kujitawala.

Harold Ford, a former deputy assistant secretary for functional analysis and the research bureau of intelligence and research US Department of State, talks about "a misunderstanding of the appropriate role of economic intelligence compared to other intelligence factors. "Economic lntelligence is a traditional function of the intelligence community. First, economic policies need Economic lntelligence support. Second, the monitoring of technological development is an important issue for national security. Third, the existing threat to the national economy requires active counterintelligence measures.”

Waalau Covid imetupa akili hata kutumia vitambaa kwa kushona layer 3 ili kujikinga. Tanzania tunalima pamba, barakoa moja, inaweza kutengenezwa na kg ngapi za pamba. Mathalani, leo tuanzishe viwanda kadhaa kutengeneza barakoa zenye ubora unakidhi viwango vya who, vitambaa au uniforms za idara za afya ulimwenguni. How much will we make out of it.

Pamoja na vita baridi vya kiuchumi kati USA na China. Nadhani tukitengeneza hata barakoa zenye ubora unaokidhi viwango vya soko; chance yetu kuuza ni kubwa kuliko China ambae ni adui wa USA kiuchumi.

I wish Investment bank ingekuwa na idara kabisa walau ya competitive Intelligence and innovation. Ili kujua what is our global competitive advantage. Tunahitaji aina gani ya technology na know how, ili bidhaa ikitoka hapa bongo itauza na mkopo utarudi.

Tanzania, is the sleeping giant. Sijui kwanini hatuoni hili
 
Pamoja na vita baridi vya kiuchumi kati USA na China. Nadhani tukitengeneza hata barakoa zenye ubora unaokidhi viwango vya soko; chance yetu kuuza ni kubwa kuliko China ambae ni adui wa USA kiuchumi.

I wish Investment bank ingekuwa na idara kabisa walau ya competitive Intelligence and innovation. Ili kujua what is our global competitive advantage. Tunahitaji aina gani ya technology na know how, ili bidhaa ikitoka hapa bongo itauza na mkopo utarudi.

Tanzania, is the sleeping giant. Sijui kwanini hatuoni hili
Mkuu Jambo uliloongea Ni zito Sana idara zote za intelligence kwenye private sector huwa zinajificha kwenye kitu kinaitwa product research and development huko ndiko mashushushu wa kampuni iwe bank au kampuni huwepo kila kampuni inatakiwa kuwa na mashushushu kwenye R&D department

Private sector inahitaji Sana capacity development
 
Uzi wa kijinga na kikasuku sana huu. Nimeusoma ila nimegundua ni mkusanyiko wa sentensi tu hauna maana.

Mradi wa JK Heart Centre pale MNH ulibuniwa mwaka 2010 na ujenzi itakamilika 2012. Installation ya Cardic Unit ilifanywa kuanzia mwaka 2012 na kukamilika 2013. Procurement na mobilization ya accessories na consumables ilifanyika mwaka 2014. Centre ilikuwa fully operational by January 2015.

Stop bragging guy
Unaweza kuwa una taarifa ila zikawa sio taarifa sahihi.Mimi binafsi nimeuguza mzazi wangu katika ICU ya Jakaya Kikwete Cardiac Institute mwaka 2014 na taasisi ilikuwa inafanya kazi na mpaka surgeries zilikuwa zinafanyika kwa wakati huo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Kuna mtu kanishirikisha ahadi ya Rais JPM kwa waandishi wa habari Nov 7, 2016.

Nataka kuamini kuna waandishi wa habari walifungua kampuni na kutumia fursa hii.

Kwa mujubu wa chanzo kimoja pia nimejuzwa, TIB wanatoa mikopo kwenye agro-processing.

Nitoe rai kwa vijana mnahusika moja kwa moja na masuala ya uwekezaji na kukuza uchumi kwenye idara, ofisi ya PM-Uwekezaji au TIC.

Kama jinsi ambavyo multinational companies kwa kushirikiana na serikali zao huwa wanapanga ya kukuza biashara ili kuwa na market share na kukuza uchumi wa nchi zao (mipango kwa njia za wazi (overt) au za kificho (covert)) mwisho wa siku wanaingia sokoni. Iko haja serikali izishike mkono start-ups, SMEs na firms kubwa.

Ghirardelli Sweet Ground Dark Chocolate & Cocoa Powder, 3 Pound Can with Limited Edition Measuring Spoon | Buy Products Online with Ubuy Denmark in Affordable Prices. B07S1R98NJ
2378437_1587744755335.png



hii ni 1.3kg inauzwa DKK258 (sawia na 86,000TZS) COCOA
McCafe Colombian Ground Coffee, 30 Ounce | Buy Products Online with Ubuy Sweden in Affordable Prices. B01M226ESB



2378439_1587744863078.png


Hii ni Kahawa Arabica toka Colombia bei SEK148 gm 850(sawia 33,000 TZS)
McCafe Colombian Ground Coffee, 30 Ounce | Buy Products Online with Ubuy Sweden in Affordable Prices. B01M226ESB

Vitu kama hivyo hapo juu kwa nilichoambia minimum loan requirement kwa Mtanzania mwenye kampuni, lets hope for the best kwenye kujenga uchumi jumuishi kwa mfumo wa viwanda ili kutoa ajira na kuongeza thamani kwenye fursa kibao Tanzania.
 

Attachments

  • 1588681862216.png
    1588681862216.png
    37.6 KB · Views: 1
SHIDA YA TISS NA VIONGOZI WALIOPO SERIKALINI NIKUFIKILIA KAZI KUBWA NIKUPAMBANA NA WATU WANAOTOA MAWAZO KINZANI BASI
 
Unaweza kuwa una taarifa ila zikawa sio taarifa sahihi.Mimi binafsi nimeuguza mzazi wangu katika ICU ya Jakaya Kikwete Cardiac Institute mwaka 2014 na taasisi ilikuwa inafanya kazi na mpaka surgeries zilikuwa zinafanyika kwa wakati huo.

Sent using Jamii Forums mobile app
JKCI imeanzishwa wakati JK akiwa madarakani; na alimteua; Prof. Janabi kukaimu Ukurugenzi wa taasisi hiyo.
JPM alipoingia akamthibitisha kama DG kamili.
Msingi wa manunuzi ya equipment kwa JKCI au popoete pale wakati wa Mkapa, JK hata JPM yanawapa nafasi wataalam wa Kitanzania kutoa huduma za tiba na kupunguza gharama za kupeleka wagonjwa India.
Hata hivyo, mara kadhaa, Prof. Janabi amekuwa akitoa taarifa namna gani namba ya wagonjwa waliokuwa wanapelekwa nje kwa matibabu imekua ikipungua na nchi kuokoa ghamara. Huu ndio msingi wa hoja, mkuu
 
Mkuu Jambo uliloongea Ni zito Sana idara zote za intelligence kwenye private sector huwa zinajificha kwenye kitu kinaitwa product research and development huko ndiko mashushushu wa kampuni iwe bank au kampuni huwepo kila kampuni inatakiwa kuwa na mashushushu kwenye R&D department

Private sector inahitaji Sana capacity development
Na capacity development inaweza kutolewa na Public in term of govt back-up, kwa kuwa biashara ikifanya vizuri 18% ya mauzo inaingia serikalini. 18% ya manunuzi ya utilities kama umeme, maji, vipuri au huduma nyingine yoyote 18% inakwenda serikalini.
Kampuni binafsi ikitengeneza faida, 25% corporate tax inakwenda serikalini kama kampuni imesajiliwa DSE au 30% corporate tax kwa kampuni isiyosajiliwa DSE.
Mishahara inakuwa taxable. 20% ya mshahara toka kwa muajiri na muajiriwa inakwenda pension funds.

Kuna baadhi ya watu, kweenye public sector hawajali kuona private sector ikikua kwa kuwa wao mwisho wa mwezi wanapata paycheck.

Kumbe kukua kwa private sector kukua pia kwa fursa fedha kuingia public sector.

Tunawajibu kuijienga Tanzania kwa pamoja.
 
Unaweza kuwa una taarifa ila zikawa sio taarifa sahihi.Mimi binafsi nimeuguza mzazi wangu katika ICU ya Jakaya Kikwete Cardiac Institute mwaka 2014 na taasisi ilikuwa inafanya kazi na mpaka surgeries zilikuwa zinafanyika kwa wakati huo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nakubali variation ya mwaka mmoja 2014 baada ya 2015 niliyosema. Je na huyo mtoa mada anaye msifia huyo Magufuli kwa kuanzisha JKHI unamuambiaje?
 
Nakubali variation ya mwaka mmoja 2014 baada ya 2015 niliyosema. Je na huyo mtoa mada anaye msifia huyo Magufuli kwa kuanzisha JKHI unamuambiaje?
Kila mmoja anafahamu JKCI imeanzishwa na JK. Kazi ya JPM kwa nafasi yake ya Urais anawajibika kuendeleza mifumo ya huduma za jamii ikiwamo hospitali kama JKCI.
Sasa, sijui, mchangia mada ni wapi hujaelewa.
Nakiri wazi, sina Rais mwingine zaidi ya JPM kwa taratibu tulizojiwekea. Ntamsifu kwa mema anayofanya. Ntashauri kwa jukwaa la wazi kama hili kwa mambo ambayo nadhani yakifanyika yataongeza assets kwa mama Tanzania.

Pengine hata ungekuwa wewe ni Rais wa Tanzania, au mgombea wako 2015 angekuwa rais, ungefanya mema, ningesifia. Ungefanya yasiyokidhi matarajio yangu, ningetoa hoja mbadala ambayo kama ingefanyiwa kazi wewe sote tungefaidika
 
Kumekuwa na michango mbalimbali ya vijana kushangaa ilikuaje Mwl. Nyerere alimwamini Balozi Dr. Agustine Mahiga kuwa Director wa TISS akiwa na miaka 35 tu. Ikumbukwe, kwa mujibu wa wasifu wake, unaonesha Balozi Mahiga alikuwa Mkurugenzi wa Utafiti na Mafunzo Ofisi ya Rais akiwa na miaka 32 (hiyo ni mwaka 1977). Hii inatupa taswira vijana wanaweza na inawezekana kufanya mapinduzi ya kiuchumi/kibiashara kupitia vijana.

Mjadala mwingine ulijikita pale Balozi Mahiga aliweza kuzima jaribio la mapinduzi dhidi ya Mwl. Nyerere 1983. Baada ya hapo ndipo aliondoka na nchini na kutokomea kwenye shughuli za kidiplomasia.

Naendelea kutoa pole kwa familia na Watanzania kwa kupoteza jembe. Balozi Mahiga kamaliza safari yake kwa kutatua changamoto za usalama, ki-diplomasi, kijamii na kisiasa.

Pengine nitoe rai kwa Diwani Athumani, boss wa sasa Idarani ni namna gani anaweza kuongoza juhudi za kimkakati ili jamii kubwa ya Kitanzania (ambao ni vijana) wasipinduliwe. Mapinduzi ya kimkakati toka magharibi ni kuwafanya vijana kuwa busy kwenye vitu ambavyo ukipima huoni uzalishaji unaojenga biashara na uchumi endelevu kupitia shughuli wanazofanya.

Tanzania tuna nguvu kazi ya vijana wanamaliza elimu ya msingi, sekondari na vyuo; iko haja kuchukua hatua madhubuti kutumia akili na nguvu zao ili kujenga platform wazalishe na kukuza uchumi kwa biashara. Kuliko kutumia fedha nyingi kwenye udhibiti wa uhalifu usifanywe na watu ambao wangekuwa busy, basi kiwango cha uhalifu, usaliti na “kutumiwa” kingepungua.

Director Diwani Athumani una kazi kubwa kulifanya hili litokee kwa ku-set strategic investment models ili tufike nchi ya “maziwa na asali” kwa muda mfupi zaidi.

Howard Gardner mtafiti wa mifumo mbalimbali ya uwezo wa akili (intelligence); anasema, moja ya aspect ya kufika mbali kwenye nchi au organization ni kutumia intuition, imagination, interdependencies na ubinadamu. Mambo haya, yanakuwa msingi wa kila kinachofanyika kwenye nchi, taasisi za umma na binafsi zilenge kutatua matatizo ya wanadamu wengine.

Tukinukuu tafsiri ya Howard Gardner, inasema “Intelligence is the ability to solve problems, or to create products, that are valued within one or more cultural settings.”

Katika Makala hii sitajikita katika ukachero ambao wengi huwa recruited kwa merits za recruitment ni familia zao ni wasiri sana, au wana historia fulani. Hao nao wana sehemu yao ila kuna haja ya “kupanua goli”. Kumbe tunaweza kuwa na intelligence recruits kwenye eneo la creativity & innovation ili kujenga mkakatu wa kitaifa kwenye biashara na uchumi. Muktadha wetu Tanzania ni fikra za namna gani ya kutumia competitive advantage kwenye mauzo ya madini, gesi, mauzo ya agro-products, mauzo ya products za utalii kwa soko la nchi 8 zilizotuzunguka na ughaibuni pia. 1993 Rais wa USA, Bill Clinton moja ya mkakati wake ulikuwa usalama wa uchumi kwa kuifanya Marekani ipate kodi kupitia ongozeko la shughuli za biashara na uchumi.

Baada ya Covid19; DNA ya creativity & innovation haikwepeki ili usalama wa uchumi wetu, u-boost usalama wa taifa. Esau alipofanya shughuli zake za mawindo na kukosa chakula, ali-negotiate ya mdogo wake na kuuza uzaliwa wa kwanza akiwa na njaa. Wakati huu wa “utandawazi”, inaweza kuwa rahisi sana baadhi ya vijana “kutumika” kwa kuwa wana “njaa”

Role ya Public Sector ni kujenga mazingira wezeshi ili private sector iweze ku-bloom. Inahitaji jicho la ku-scout "new brains" ambazo zipo, kuleta mapinduzi ya uchumi na biashara ili tax base iwe kubwa kwa serikali ili Tanzania izidi kuchanua.

Tuangalie project models za nini tulifaya Tanzania, nini wenzetu walifanya nchi zingine na matokeo yake yalikuaje baada ya muda

Hii ni taarifa ya toka gazeti la ndani ikinukuu miradi yenye thamani ya 2TRIL.

Pension funds spend Sh2tr on investments in one year

Chanzo kingine kinaonesh ghorofa PSPF Golden Jubelee Tower ilijengwa kwa USD 70 million (sawa na TZS 112bn kwa exchange rate ya 2012. Yaweza kuwa TZS 161 bn kwa exchange rate sasa)

Nimeweka hii mifano kuonesha baadhi sources za hela ziko wapi, licha ya uwezekano wa kupata mikopo toka vyanzo vingine vya ndani na nje ikiwamo dhamani ya serikali kupitia BOT.

Zile USD 70 mil za kujenga ghorofa. Je tunaweza kupata dhamana ya serikali ili tungeziweka kwenye Public Private partnership tukitumia kwa kuwekeza kwenye kuchakata walau 25% ya kahawa ghafi inayozalishwa Tanzania kwa ajili ya exports. Kwa kila mwaka tungeuza kwa uchache tani 10,000 ya kahawa (Consumable coffee). Kahawa kg moja inauzwa USD 30 au zaidi. Kama tukipata 60% ya mauzo ya mwisho kwa 25% ya wastani wa kahawa tunayozalisha. Ina maana kwenye mzunguko wa fedha za ndani kupitia kahawa pekee kwa miaka 5 ya JPM zingekuwa zimepita TRIL 3.45;

Check sites hapa chini bei za consumable coffee kwenye soko.

Ubuy Canada Online Shopping For instant coffee nestle in Affordable Prices.

Ubuy Sweden Online Shopping For instant coffee nestle in Affordable Prices.

Amazon.com : instant coffee

Kuziba hili pengo la nini tunauza kama raw coffee vs mauzo ya mwisho ambapo tunatumia strategic competitive intelligence tool na consulting marketing firms tuongeze market share finished products za kahawa, chai, korosho, pamba badala “kulaliwa” kila siku.

Henry Ford anasema “Coming together is the beginning. Keeping together is progress. Working together is a SUCCESS” Umoja ni Nguvu na utengamano ni udhaifu’ wahenga walituasa.

Honestly, hatuwezi kujenga uchumi endelevu kama nguvu kazi ya vijana wataendelea kuwa absorbed kwenye bodaboda, kukaanga chips… These are hand to mouth kutoka kwenye 10% ya makusanyo ya halmshauri. Iko haja kujenga sustaible inclusive economy ili dira ya maendeleo ya Taifa itimilike kwa udhahiri zaidi.

Investment financing kwa kununua “technology & know-how” mrejesho wake ni mkubwa kwa fedha itakayowekezwa wakati huo huo kazi mpya kwenye mifumo rasmi zimezalishwa.

Nguvu ya vijana ikijengewa mazingira, basi ndege, SGR, bandari, Nyerere Hydropower na miradi mikuwa kama hiyo itajengwa huku tax base ikipanuka.

Tujipongeze Watanzania na hasa Hongera sana Mhe. Magufuli kwa kuweza kununua technology kufanyia operation za moyo JKCI. Kuna hela nyingi sana tumeokoa malipo ya fedha ili kupata huduma ya matibabu.

Hivyo basi, usalama wa Taifa letu pendwa Tanzania, kwenye karne ya 21, hatuna budi kuamua kwa haraka zaidi ili vijana wawe sehemu ya “jeshi” la kuzalisha ili kuongeza mauzo ya soko la nje la finished products ili tuanze kutengeneza balance of trade surplus.

Kitabu cha what is next; How to use theories using the theories of innovation to predict industry change anatupa basic principles kuhusu namna ya kujua, Signals of Change, kujua fursa ziko wapi (Opportunities), Ushindani uko wapi (Competitive Battles), namna gani ya kuwapunguza washindani (How to Size Up Competitors)na cha mwisho ni Strategic Choices.
Takwimu toka Worlb bank zaonesha, miaka ya ‘90, uchumi wa Tanzania ulikuwa USD 4.5 bil wakati Vietnam alikuwa na USD 6.5 bil. Wakati huo huo, Kenya alimzidi Vietnam GDP ya USD8.4bn.
Mwaka huu Uchumi wa Vietnam ni USD 260bil, Tanzania USD 60bil, Kenya USD 90 bil

Vietnam wananunua korosho yetu kwa wastani wa TZS4mil kwa tani kama kg moja ni TZS 4,000; wao wanauza zaidi ya TZS 50,000 kwa kg. Kama walinunua korosho ghafi tani 400,000 (tukapata 1.6 Tril). Wao waki-process wanapata

Check bei za consumables cashew products

Amazon.com : cashew

Ubuy Saudi Arabia Online Shopping For cashew in Affordable Prices.

View attachment 1440072

Mwisho niwashirikishe homework niliyokuwa nafanya na watoto wangu. Umeona tigers wangapi. 4, 6, 7, 8, 9, 10, 11, 12 au labda 14. Ikiwa mtu anaona 4 au 6 iko haja akashirikiana na yule anaeona 12 hadi 14 ili fursa walau zaidi ya 10 zitumike kwa tija kuliko zile 4 zilizo easily visible.

Kupanga ni kuchagua. Tuchague kwenye kuongeza exports za consumable.

Nawatakiwa Jumatano Njema.

Fred
Tukiachana na mada nimepata tigers 17
 
Kila mmoja anafahamu JKCI imeanzishwa na JK. Kazi ya JPM kwa nafasi yake ya Urais anawajibika kuendeleza mifumo ya huduma za jamii ikiwamo hospitali kama JKCI.
Sasa, sijui, mchangia mada ni wapi hujaelewa.
Nakiri wazi, sina Rais mwingine zaidi ya JPM kwa taratibu tulizojiwekea. Ntamsifu kwa mema anayofanya. Ntashauri kwa jukwaa la wazi kama hili kwa mambo ambayo nadhani yakifanyika yataongeza assets kwa mama Tanzania.

Pengine hata ungekuwa wewe ni Rais wa Tanzania, au mgombea wako 2015 angekuwa rais, ungefanya mema, ningesifia. Ungefanya yasiyokidhi matarajio yangu, ningetoa hoja mbadala ambayo kama ingefanyiwa kazi wewe sote tungefaidika
Napinga maneno ya kwenye post yako ya kwanza umeandika hivi;


"Tujipongeze Watanzania na hasa Hongera sana Mhe. Magufuli kwa kuweza kununua technology kufanyia operation za moyo JKCI."
 
Sio kweli kila kitu Kiko kwenye internet Kuna vyuo bubu Tanzania vya kufundisha watu kutengeneza pikipiki kuanzia mwanzo Hadi mwisho practically pikipiki zenye majina sifa kuu uwe fundi welding watu wanalipia ndio.maana nasema vyuo unaccredited viruhusiwe.Vijana wadogo tu wengi unaowaona mafundi pikipiki uwezo huo waliupata vyuo bubu mapema kabla hata VETA hawajaweka hizo course kwenye mitaala sababu wao walikuwa na course za kutengeneza magari tu sio pikipiki na bajaji

Wenye vyuo bubu wakaanza kutoa hizo course mapema kabla VETA hawajaamka!!!
Sio kweli kila kitu Kiko kwenye internet Kuna vyuo bubu Tanzania vya kufundisha watu kutengeneza pikipiki kuanzia mwanzo Hadi mwisho practically pikipiki zenye majina sifa kuu uwe fundi welding watu wanalipia ndio.maana nasema vyuo unaccredited viruhusiwe.Vijana wadogo tu wengi unaowaona mafundi pikipiki uwezo huo waliupata vyuo bubu mapema kabla hata VETA hawajaweka hizo course kwenye mitaala sababu wao walikuwa na course za kutengeneza magari tu sio pikipiki na bajaji

Wenye vyuo bubu wakaanza kutoa hizo course mapema kabla VETA hawajaamka!!!

Vyuo bubu vya kutengeneza simu za mkononib vliianza zamani Sana kabla VETA hawajaamka!! Vyuo bubu kibao Hadi vya kutengeneza Computer vikianza kabla ya VETA kuamka!!!

Serikali iruhusu tu unaccredited schools and colleges
Wapo mtaani watu ni wazuri kwenye tech wala hawasubiri vyuo hivo.Me machine yeyeto niitakayo najiundia
 
Wapo mtaani watu ni wazuri kwenye tech wala hawasubiri vyuo hivo.Me machine yeyeto niitakayo najiundia
Mkuu hongera anzisha chuo hata bubu uanza kufundisha mafundi wengine kutengeneza kwa kuwachaji pesa

Mafundi cherehani huwa na vyuo bubu .magereji pia ,mahotel nk weka chako
Waweza kukusaidia pia kuzalisha nyingi wakiwa mafunzoni ukaanza kuuza kwa wingi
 
Mkuu hongera anzisha chuo hata bubu uanza kufundisha mafundi wengine kutengeneza kwa kuwachaji pesa

Mafundi cherehani huwa na vyuo bubu .magereji pia ,mahotel nk weka chako
Waweza kukusaidia pia kuzalisha nyingi wakiwa mafunzoni ukaanza kuuza kwa wingi
Nimeingia YouTube nimetengeneza machine ya kusaga plastic, na ya kutoa lebo za plastic kwa jumla ya gharama ya milioni 4.5 ambazo kama ningeagiza China au India ingenipasa kutumia milioni 20.For the same kg output per hour.Sihitaji kununua dizeli Kwa ajili ya magari nazalisha mwenyewe kwa kusaga plastic.
Nimecheck Indonesia na Sri Lanka vijana chini ya mti kwa kutumia just grenda,welding machines,gas,bending machines wanasuka mabody classic ya mabus ya kisasa kabisa mchina akasome huku tunauziwa milioni 500 ,wacheck insta au YouTube ingia @ mjpm garage,wakati vijana wetu wako bize kusaka udaku na kushinda kuilamu ccm mitandaoni,wenzetu wa Asia wako bize kucheck new technology.
 
Back
Top Bottom