Msiba mzito wa mama yetu, mwalimu wetu mpendwa

Original Pastor

JF-Expert Member
Nov 14, 2007
1,274
50
Msiba mzito wa mama yetu, mwalimu wetu mpendwa mama yetu na mwalimu wetu mpendwa Frida Mtunguja ambaye alikuwa anafundisha shule ya msingi chumbageni tanga amefariki jana tarehe 16/06/2009 saa 22:46:12 katika hospitali ya bombo baada ya kuugua maradhi ya homa ya manjano.

Msiba utakuwepo nyumbani kwake kisosora tanga na mipango ya mazishi inafanywa na ndugu na jamaa.

Kwa wale wanaoguswa kwa njia moja au nyingine hasa wanafunzi wa chumbageni ambapo marehemu alikuwa anawafundisha tunawapa pole sana. Kuhusu michango yenu inaweza kutufikia hapa nyumbani au hapo shule ya msingi chumbageni tanga.

Ukiwa kama ndugu, rafiki au jirani unaombwa kufika katika msiba huu wa mama yetu /mwalimu wetu mpendwa.

Kwa mawasiliano ya kutuma michango yako piga namba hii +255717062827 ni mwanae anaitwa mMichael Kuziwa (huyu alisoma Galanos Sekondari alimaliza mwaka 1999 form IV)
 
Nakumbuka tulikuwa na Dada mmoja naitwa Beatrice Mtunguja. Tulisoma nae Mkwawa Comlex Casino miaka hiyo 1996-98....hivi......Naamini atakuwa na undugu na marehemu...

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU PEMA PEPONI.... AMEN
NAAMANI WANA JF WAKO NANYI KATIKA KIPINDI HIKI CHA MAJONZI..
 
Poleni sana wadau mungu amuweke mahali pema peponi. Hata mimi namkumbuka huyu dada Beatrice Mtunguja kule complex bomba tatu miaka ya 1996-1998 enzi za mzee Rugunjamheto na akina Nguwi.Poleni sana ndugu zangu.
 
Tunashukuru kwa michango yenu tunajua mko pamoja na sisi ok sasa ukifika hapa nyumbani ni bora zaidi na kuhudhuria mazishi lakini wanandugu tukipanga tutawapa taarifa wadau wote.
Kufika kutoa mkono wa pole
 
Nakumbuka tulikuwa na Dada mmoja naitwa Beatrice Mtunguja. Tulisoma nae Mkwawa Comlex Casino miaka hiyo 1996-98....hivi......Naamini atakuwa na undugu na marehemu...

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU PEMA PEPONI.... AMEN
NAAMANI WANA JF WAKO NANYI KATIKA KIPINDI HIKI CHA MAJONZI..

Shiumiti nami nilipoona hilo jina la mtunguja nikamkumbuka Beatrice Mtunguja wa Mkwawa enzi hizo maana nilikua nae Bweni moja.

all in all poleni sana wafiwa.
 
Dunia ndio inateketea wazuri wote na wenye faida wanaondoka

MUNGU AILAZE ROHO YA MWALIMU WETU MAHALI PEME PEPONI
 
Poleni sana kwa msiba mkubwa, Mwenyezi Mungu amlaze marehemu mahali pema peponi~AMEN
 
Hakika sisi ni wa M'Mungu na kwake sote tutareje.

Moja ya kazi ninayo iheshimu sana hapa duniani ni Ualimu, kuondoka kwa Mwalim huyu ni moja ya pigo kubwa sana kwa wale wote waliopitia kwake kwa njia moja ama nyingine.

Basi nami nachukuwa nafasi hii kuwakilisha rambi rambi zangu kwa wafiwa, na Insha'Allah M'Mungu atawapa nguvu, uvumilivu na subra katika kipindi hiki cha maombolezo ya msiba huu mkubwa wa mwalimu wetu, mama yetu, dada yetu, rafiki yetu na jirani yetu aliye jitolea kwenye wito wa kutufundisha sisi na watoto zetu.

M'Mungu hawe nanyi kwa kipindi chote hiki cha majonzi Insha'Allah.

XP
 
Back
Top Bottom