OscarkambonaJr
JF-Expert Member
- Jun 1, 2022
- 1,592
- 2,567
Ilikua Jioni majira ya saa 12 Mwaka 1995 Mkoani Mbeya alibishwa hodi nyumbani kwetu na mdogo wangu Asubisye Alitoka kwenda kuitikia wito na kumkaribisha mgeni.Alikua ni mama wa makamo amebeba begi na mfuko mkononi. Alikua,alipoingia malangoni kwetu Nilitoka jikoni nilipokua naandaa mlo wa mchana kwaajili ya familia na kuelekea sebureni na kupokelewa na sauti ya kilio huku nikikumbatiwa na mama Yule,Aliniita Nusume pole shangazi yangu,tumebaki peke yetu huku akinikalisha kwenye kochi. Alikua ni shangazi yangu mdogo wa wa baba yetu Tupilike akitokea Morogoro Kilombero.
Ghafla machozi yalitililika mashavuni mwangu baada akili kunijia kuwa mama yangu mzazi Tupokigwe hatunaye duniani maana alienda na baba kwaaliji ya kuuguzwa kijijini kwa baba na mama yetu. Nikiwa binti wa miaka 13 ,Mtoto wa kike pekee kwenye familia ya watoto wanne. Kaka yetu wa kwanza anaitwa Athur, wa pili ni Kulwa ambae ni pacha wangu na mwisho ni Asubisye ambae ni mdogo wetu.
Nilianza kuwaza Maisha bila mama yangu kipenzi ambaye alikua mwalimu wa shule ya msingi Iwambi wakati huo mbeya haijawa jiji.Baba yetu alikua afisa misitu Wilaya ya Kawetele.
Hata chakula nilichokua naandaa kilikosa maana tena majirani wakaanza kuja kujua nini kinaendelea,Kama kawaida viti vilitolewa nje na mikeka maandalizi ya msiba na taratibu nyingine zilianza kupangwa na watu wazima waliofika pale.Walimu na wafanyakazi we zake na baba wakawasili nyumbani kupanga mikakati ya mazishi huko kijijini kwetu Isoko wilaya ya Ileje. Kaka yangu nae aliporudi shule alikuta Hali ya msiba tukajumuika Kama familia nikiwa napelekwa tu maana kwa umri wangu ni tukio geni kabisa,Hata kaka yangu pia hakuwa na cha kufanya maana alikua mdogo pia.Kiufupi ilikua familia changa maana watoto wote tulikua under 18
Kesho yake zilikuja gari za serikali kutuchukua na baadhi ya majirani kuelekea Kijijini kwaajili ya mazishi.
Tulifika na kumkuta Baba na ndugu wengine hakika baba alikua na uchungu sana kupoteza kipenz chake alitukumbatia akalia kwa uchungu nakumbuka akasema nawapenda wanangu nitawatunza.
Baada ya mazishi tulibaki muda wa wiki mbili kijijini ndipo tukarudi nyumbani ili maisha mengine yaendelee. Nilifika nikakuta picha zote za marehem mama zimetolewa sebureni,Nilifanikiwa kupata picha moja tu ambayo mama yetu alipiga na Sisi tukiwa watoto wote wanne.
Hakika Maisha yalibadilika ghafla bila mama yangu kipenzi,afya ya mdogo wetu Asubisye wa miaka mine ilidhoofu.Baba alishindwa kuhikili kile kishindo kabisa.
Baba akamua kuomba msaada wa kutafutiwa dada wa kazi walau asaidie baadhi ya majukumu pale nyumbani ikiwemo kukuangalia mdogo wetu.Baada ya miezi kadhaa Hali ya mdogo wetu haikutengemaa,Shangazi yetu aliomba kumchukua kukaa nae kwakuwa alikua na watoto wa lika lake hivyo angechangamka akiwa huko.
ITAENDELEA……..