Mshindi wa Mechi ya Leo ya Simba na Yanga Ajulikana!

Dar_Millionaire

JF-Expert Member
Aug 6, 2008
227
82
Mshindi wa mechi ya leo kati ya Simba ya Yanga ameshajulikana.

Ni Azam FC!

34567_131875510186147_131868543520177_159091_6055861_n.jpg

Leo hii Simba na Yanga watakapomenyana Uwanja wa Taifa kama kawaida watajaza uwanja mpaka pomoni. Ili kuwahi viti maelfu na maelfu ya wapenzi wa soka wamewahi uwanjani toka saa nne asubuhi.

Hii ina maana wengi watashikwa na kiu kwa kukaa muda mrefu uwanjani, na kwa kushangilia sana hapo baadae mechi ikishaanza. Hivyo lazima watakunywa kwa wingi vitu vifuatavyo:

  • Maji ya Uhai
  • Soda za Azam Cola, na Azam Malt
  • Na kulamba ashkrim za Azam
Wakati Simba na Yanga zitapigwa mabao ya kisigino na TFF kwenye mapato yatokanayo na mauzo ya tiketi, Azam atakusanya kiulaini mapato yake kutokana na mechi hiyo.

Sasa nani mshindi hapo? Kalagabaho na hizi timu za kichama. Azam FC ndio chama la ukweli la wajanja.
 
Embu tujuze kwani Azam ndio kanunua mechi au,kama ndio hii tenda ilitangazwa lini,pia hivyo vimiminwa vya Azam ndio vimeruhusiwa kuuzwa hapo uwanjani peke yake au na kama jibu ni ndio utaratibu gani umetumika ili auze peke yake na je kuna tenda ilitangazwa ,haya bana nchi ya kitu kidogo,kula kona kuna kaharufu kale kabaya ka ufisadi ,itabidi nikaombe kazi TFF
 
Mfianchi, hajanunua bali ye ndo muuzaji mkubwa wa hizo bidhaa.
 
Are u out of your mind? Coz the heading is very different from what you explained inside.i think you should find another title to fix the previous one. Enjoy the game
 
Back
Top Bottom