Mshikaji wangu kampenda Mwanamke wa Club

G'taxi

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
6,565
8,426
Ndugu nisiwachoshe msinichoshe

Jamaa ametuijia leo akiomba msaada wa ushauri, tukasema acha wengine tuingie hapa, mshikaji kampenda mwanamke lakini hamjui vizuri, sisi tunaishi na mwanamke nyumba moja kama wapangaji maeneo ya kazi.

Mshikaji kampenda huyu mdada ambaye awali alikua anafanya kazi za barbershop, mara kwenye mahotel.

Nowdays mwanamke hanaga kazi yupo nyumbani, lakini anaweza kushinda geto mchana wote na ikifika saa kumi za jioni mwanamke anatoka na anarejea kwenye kuanzia saa tano mpaka hata saa nane.

Mshikaji akimbana mwanamke anamwambia ana mawazo na alienda club kupoteza mawazo, jamaa anampenda demu lakini bi dada anaonyesha Dalili zote za kua ni mwanamke w kudanga.

Jamaa anasema simu za mwanamke muda wote ziko busy mbaya mpaka wanagombana,mshikaji akisafiri inapofika usiku akiwa anampigia simu mwanamke huyu, mawasiliano yanakua ya tabu sana na wakati mwingine anamkatia simu,akija kumuuliza mwanamke anakua mkali na kumtamkia waachane.

Kimsingi jamaa kwa maoni yangu binafsi anapaswa amteme huyu demu,lakini kwa kua amekuja kuomba msaada wa ushauri nini afanye, tukasema tutaongea nae weekend, binafsi nikasema wako wadau waliokutana na kesi hizi za wanawake wa namna hii hebu niwaulizeni japo tumshauri nini hasa
 
Jamaa wako anaonyesha yeye ni kijana WA hovyo .

Unamtongazaje mpangaji mwenzako ?!
hii technical alitakuwa kuwa rafik WA faida. kibaya zaid ni mali ya kijiji , kijana ameonyeshwa Dalili zote za mahusiano ni big No bado anaendelea kuforce ..🥴

Mwambie huku JF kuna wadada wengi wanatak kuolewa ,,
 
Sina cha kukushauri, hapa nilipo najizuia tu kucheka🐒

20230618_202517.jpg
 
Ndugu nisiwachoshe msinichoshe

Jamaa ametuijia leo akiomba msaada wa ushauri, tukasema acha wengine tuingie hapa, mshikaji kampenda mwanamke lakini hamjui vizuri, sisi tunaishi na mwanamke nyumba moja kama wapangaji maeneo ya kazi.

end, binafsi nikasema wako wadau waliokutana na kesi hizi za wanawake wa namna hii hebu niwaulizeni japo tumshauri nini hasa
Muda ni Mali. Muda haurudi nyuma. Kosea kujenga lakini usikosee kuoa. Mwambie Jamaa awe serious aache utani na maisha. Hakuna mwanamke hapo. Ataishi kwa stress Hadi lini?

Eti kama vipi tuachane, nyendo zake utata mtupu...wa nini huyo mwanamke???

Aangalie maisha yake, asipofanya hivyo atateseka Hadi uzee na watoto pia watasota, hukuna mke hapo. Tafuteni dawa kama vipi mmtibu jamaa amsahau huyo demu( kama zipo lakini kama wakurungwa wanavyosema, maana mtampoteza huyo jamaa).
 
Sure,ushauri tutamfikishia
 
Back
Top Bottom