Mshahara wa wabunge wapanda mpaka 11,000,000/-

SirBonge

JF-Expert Member
Jul 18, 2010
378
435
Mshahara wa wabunge umepanda kutoka Tsh 6,000,000/- kwa mwezi mpaka Tsh 10,000,000/- kwa mwezi mbali na marupurupu mengine!..

Hii inakuja ikiwa wadaktari tayari wameshatangaza mgogoro na serikali na kuipa wiki 2 kutimiza madai yao la sivyo watatangaza mgomo mkubwa nchi nzima kuanzia 23/6/2012...

Source: Mtanzania ya leo

"Hatuwezi kutatua matatizo kwa akili ile ile ambayo ilisababisha yawepo"..Mch. Peter Msigwa


Wabunge wazidi kuongezewa marupurupu:Monday, 30 July 2012 - Boniface Meena, Dodoma

MARUPURUPU ya wabunge ikiwamo mishahara imeongezwa kutoka Sh7.4 milioni kwa mwezi hadi takriban Sh11milioni kwa mwezi, hatua ambayo imeibua mjadala mwingine mzito miongoni mwao.

Tangu mwaka jana, wabunge wamekuwa katika vita ya kupokea au kutopokea posho ya vikao ambayo imekuwa ikikolezwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe ambaye alizikataa akisema mbunge anapokuwa kazini hahitaji kulipwa.
Hata hivyo, uchunguzi wa gazeti hili umebaini kwamba sasa vita kubwa ipo katika marupurupu mapya ambayo pamoja na kuchanganya na mshahara yanafikia Sh11milioni kwa mwezi.

Spika wa Bunge, Anne Makinda alipoulizwa jana alithibitisha kuhusu kuongezeka kwa malipo jumla ya wabunge kwa mwezi lakini akasema hafahamu kiwango halisi kilichoongezwa. Makinda alisema nyongeza iliyopo siyo kwa wabunge tu, bali watumishi wote wa Serikali na ilitangazwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma), wakati wa Bajeti ya Ofisi hiyo kwa mwaka 2012/13.

"Hiyo nyongeza siyo tu kwa wabunge, bali ni kwa watumishi wa Serikali. Tena hiyo ilitangazwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma). Sasa ukiniuliza kiasi gani hapo ndipo sielewei, ila najua nyongeza ipo," alisema Spika. Lakini, vyanzo kutoka ndani ya Bunge vilisema kwamba nyongeza hiyo ambayo tayari imeingia katika mshahara wa Julai ni Sh3.6milioni, hivyo kufanya jumla ya fedha anazochukua mbunge kufikia kiasi hicho cha Sh11milioni.

"Hiyo ni vita, kuna wabunge wana hasira kweli hawataki wananchi wajue kama marupurupu yameongezeka. Wanaona wananchi wakijua itakuwa ni tatizo kubwa, watapigiwa kelele lakini nyongeza hiyo ipo. Tayari wengine wamechukua tangu Ijumaa," kilisema chanzo kimoja kwa sharti la kutotajwa jina gazetini.

Hata hivyo, kwa mujibu wa chanzo hicho, baadhi ya wabunge kutoka kundi la wanaopinga posho kwa wabunge wamepinga pia nyongeza hiyo wakitaka fedha hizo zielekezwe katika sekta nyingine za kijamii.

Marupuru ya sasa

Hadi mwezi uliopita, mbunge alikuwa akipokea Sh7.4milioni kwa mwezi ambazo kati ya hizo Sh2.5milioni ni kwa ajili ya mafuta, Sh2.3 mshahara, Sh170,000 kwa ajili ya mshahara wa dereva, 100,000 kwa ajili ya katibu wa mbunge na posho ya jimbo.
Hata hivyo, katika nyongeza hiyo ya sasa haijawekwa wazi kwamba kiasi gani ni kwa ajili ya mshahara, fedha za mafuta ya gari la mbunge, za dereva, katibu na za posho ya jimbo na tayari baadhi ya wabunge wameanza kufuatilia mchanganuo wa nyongeza hiyo.

 
Haaahaaa! Nchi hii namna pekee ya kulindana ni kwa wanasiasa kula mali ya walipa kodi kwa kumegeana. Watu wanajaribu kula hata wasichopanda.
Madaktari kwa wana siasa wana umuhimu gani? Wakiumwa serikali inawapeleka fasta india
 
Kwa akili ile ile ya wapuumbavu kutaka kutatua matatizo kwa njia zilezile wakitegemea matokeo tofauti.
 
kwa kweli nitagombea ubunge 2015 ili nikale kwa niaba ya wapiga kura wangu.
 
Eti Zitto, hii ni kweli?

Sisi Watanzania in the first place ni waongo, hatujui haki zetu na ni watu wa kulalamika tu mafisadi yanaiba tunalalamika tu, mikataba ya madini, tunalalamika tu, wawekezaji wanatunyanyasa tunalalamika tu, tunaibiwa kura tunalalamika tu!

Wabunge wanajipandishia mishahara tunalalamika tu, kodi zinanyonga wafanyakazi na wafanya biashara ndogondogo tunalalamika tu! tunakufa kwa kukosa huduma za afya huku tunachangia bima ya afya tunalalamika tu??Watoto wetu wanakaa chini shuleni wakati tunatoa michango ya dawati na ujenzi tunalalama tu??

Mafisadi yanatamba tunalalamika tu? serikali inadharau maazimio ya bunge ambalo ndio midomo yetu wananchi tunalalama tu??watoto wa viongozi wanapewa madaraka na kujiimbikizia mali tunalalama tu??

Huwezi kufanya kitu kimoja kila siku kwa mbinu ileile ukitarajia matokeo tofauti(mch. Msigwa) na sisi Watanzania hatuwezi kuendelea kulalamika tu tukitegemea mambo yatabadilika! Bila kuingia mitaani na kuitikisa serikali hii dokozi na bunge lililojaa vilaza wa magamba hatutaweza kubadili kitu!

Tuamke tuache kulalama tuchukue hatua tena wakati huu wa budget ndio wakati muafaka wa kuonyesha hasira zetu!!kinyume cha hapo tuvumilie haya na mengine makubwa zaidi yanayokuja!
 
Ina maana hata Dr Slaa ataongezewa mshahara ili ufanane na wa wabunge?
The unseen is illustrated by the seen.
 
Mshahara wa wabunge umepanda kutoka Tsh 6,000,000/- kwa mwezi mpaka Tsh 10,000,000/- kwa mwezi mbali na marupurupu mengine!..Hii inakuja ikiwa wadaktari tayari wameshatangaza mgogoro na serikali na kuipa wiki 2 kutimiza madai yao la sivyo watatangaza mgomo mkubwa nchi nzima kuanzia 23/6/2012...
Source: Mtanzania ya leo

"Hatuwezi kutatua matatizo kwa akili ile ile ambayo ilisababisha yawepo"..Mch. Peter Msigwa

Je bado bajeti ya 2012/2013 haikidhi haja za Watanzania? teh teh tehe, Wabunge bana wapige kelele basi wagomee na hivyo viwango vipya vya mishahara yao
 
Serikali ya ccm mnatupeleka wapi jamani? Mbona mnatunyanyasa wazi ndani ya nchi yetu?tofauti ya kipato inazidi kuongezeka,tizama wabunge mishahara mikubwa waalimu ambao ndo nguzo na msingi wa kila kitu wamesahauliwa na kutengwa pia wananchi wa vijijini mmewasaliti oneni aibu na pia msitegemee kurudi bungeni ktk uchaguzi ujao na pia muache unafiki kuwa mnawapenda watanzania wengi mpo kwa manufaa yenu na cyo yetu tuliowachagua
 
We hujui kuwa aliamua kujilipa mshahara sawa na ule wa wabunge baada ya kuukosa Urais 2010?
The unseen is illustrated by the seen.

...acha uongo ww!aliamua kujilipa lini?ww unajua kinachoendelea au unaongea tu?uliza uambiwe c o kuandika vitu usivyo na uhakika navyo
 
We hujui kuwa aliamua kujilipa mshahara sawa na ule wa wabunge baada ya kuukosa Urais 2010?
The unseen is illustrated by the seen.

Barnabas Shadrack, kuna uhusiano wowote kati ya hii nyongeza ya mshahara kwa wabunge (kama ni kweli) na mbadiliko wa ghafla wa wabunge wa CCM kuanza kuitetea budget wakati week iliyopita walikuwa wanaongea na vyombo vya habari wakisema hawataikubali?

Pili, unaweza kutuambia Mukama analipwa kiasi gani kwa mwezi?
 
Back
Top Bottom