Mshahara wa Rais, Waziri Mkuu, Mawaziri na Watendaji Wakuu Serikalini

Annual salary of US President:
The president of the United States of America earns a $400,000 annual salary ($33,333 per month), along with a $50,000 annual expense account, a $100,000 nontaxable travel account and $19,000 for entertainment.
Over the past two centuries, the annual salary of the US Presidents has been adjusted as follows:

Date established

Salary
September 24, 1789

$25,000
March 3, 1873

$50,000
March 4, 1909

$75,000
January 19, 1949

$100,000
January 20, 1969

$200,000
January 20, 2001

$400,000

Salary of the President of the United Republic of Tanzania???
We need to know HOW our taxes are spend, and WHO spends WHAT…

Nahisi kama mshahara wa mwaka 1789 unaweza kuwa mkubwa mara 10 kuzidi ule wa sasa in terms of "purchasing power"
 
Wakuu tukiwa kama waajili wa hawa Viongozi ni shurti na haki yetu kujua malipo yao, hapa naongelea Mishahara yao, Posho zao, Marupurupu na Pension.

Tumejua ya wawakilishi wetu bungeni, na sasa ni hawa viongozi waandamizi wa Serikali.

Tumepiga kelele na kupinga ongezeko la sitting allowance (Posho) za wabunge na nadhani kwa kiasi kikubwa tuko mbioni kufanikiwa sasa ni wakati wa kuangalia malipo na posho za hawa viongozi wengine, hali ya maisha kwa mtanzania wa kawaida ni ngumu huku asilimia kubwa ikiishi chini ya Usd 1 kwa siku.

Mwenye hizi data atuwekee hapa, tuzijue na kuzipitia.

Asalaam

MODs Please msiunganishe thread hii na nyingine yeyote please.

Naona tuanza sisi kutaja mishahara yetu kabla kutaka kujuwa ya wengine, vinginevyo umbeya huo!
Wangu ni wa kima cha chini!
Jee ulioanzisha mada, wako ni kiasi gani?
 
Habari wana JF,
Naomba Nisaidiwe kujua scales za mshahara wa Rais wa Tanzania na Wakuu wengine kama Waziri Mkuu, Gavana na Mawaziri.
 
pole sana. umegusa mishahara ya masultani. hutapata jibu. hili swali tuliulizaga siku nyingi sana hapa. ila tunataka katiba ijayo iweke haya mambo wazi haiwezekani watu tuliowaajiri halafu tusijue tunawalipa shilingi ngapi. mbona nchi kama us inawezekana? kwanini isiwe hapa kwetu. na wale wanaojilipa sehemu kubwa kodi zetu huko mabandarini, tra, tanapa, maofisa huko majeshini, tanroads, mawaziri, yote tunataka iwe peupeeee kabisa.
 
Kama utajikita kuangalia MSHAHARA tu wa viongozi wetu, utakuwa UMEBUGI MEN! Mishahara yao ni ya kawaida sana ukilinganisha na nchi jirani za wenzetu na huenda mishahara yao ni midogo.

Ujanja uko kwenye marupurupu na posho, hapo ndiyo viongozi wa Tanzania wanapopiga BAO, tena mabao ya kufa mtu ya Lionel Messi (super star wa Barca) cha mtoto. Kila madudu ya UFISADI yako kwenye posho na marupurupu na mbaya zaidi hayo ma-posho na marupurupu hayakatwi kodi. Ndiyo maana inakuwa vigumu sana kuyaondoa kwani wanaofaidika na hayo VIGOGO WA SERIKALI.
 
Mimi nafikiri suala hili linapaswa kupewa kipaumbele kwenye katiba mpya. Haiingii akilini kulifanya jambo kubwa namna hii siri, ni hapo ndipo tunapo jenga mazingira ya ufisadi.
Haiwezekani nchi zinazo tupatia misaada mishahara ya viongozi wao ipo wazi, sisi tunafichaficha, sijui ni kwa manufaa ya nani?
 
'msijali bhandugu endeleeni tu kuwaghasi watawapatia majibu aithee msichoke,hivyo hivyo aithee'
 
Serikali ya Tanzania nna imani ina viwango vyake vya mishahara ambavyo vinafahamika kwa wafanyakazi wake. Ni kwa nini huwa hawaweki wazi mshahara wa Rais wa Tanzania kuwa ni shilingi ngapi? Kuna siri gani inayofichwa ndani ya huo mshahara? Kwani Rais wa Tanzania yeye siyo Mtumishi wa Umma? Kwa nini watumishi wengine viwango vya mishara vifahamike yeye wa kwake uwe siri?

Mbona wenzetu wapo open. Kwa mfano KENYA inafahamika publicly kuwa ni Ksh 1.2M. Kwa nini mambo ya UMMA sisi tunayafanya kuwa ni ya kificho na ya binafsi?
 
Sina uhakika kama kiwango kilitajwa ila nakumbuka JK alijipunguzia mshahara ukilinganisha na wa Ben ili kutuaminisha yeye ana uchungu na hali yetu mbaya kiuchumi.
 
Back
Top Bottom