Msanii LULU aomba radhi

Status
Not open for further replies.
huyu binti amekwisha habari yake. shetani kammaliza. Mungu amsaidie tu. anatakiwa kuacha kabisa hizo filamu atengeneza maisha yake kwa njia ya elimu ya darasani. la sivyo, ataolewa kwa mganga wa kienyeji kama alivyofanya mwenzie Nora.

Usihukumu ndugu utahukumiwa...shetani is at work of course lakini haimaanishi kuwa ni mshindi...Mungu wetu ni wa rehema,tumuombee huyu mtoto ili apitie toba ya kweli na kuishi maisha sahihi...
 
MSANII ‘sidanganyiki’ wa filamu nchini, Elizabert Michael ‘Lulu’ ameamua kukiri maovu yake yote ambayo amekuwa akiyatenda huku akijua kwamba yeye ni kioo cha jamii.

Akiongea na Amani juzi, Lulu alisema kuwa amekaa chini na kutafakari yote yaliyokuwa yakiandikwa magazetini kuhusu yeye na kubaini kwamba amefanya makosa hivyo kuwaomba Watanzania wamsamehe.

Alisema kuwa, anaamini hakuna binadamu aliyekamilika na kwamba anakiri udhaifu wake huo na kuahidi kubadilika.

“Nimetenda dhambi nyingi sana hivyo nawaomba Watanzania wajue kuwa hakuna binadamu aliye mkamilifu chini ya jua.

“Wakati mwingine skendo zinazoelekezwa kwangu hazina ukweli ila kwakuwa nimebaini wapi nakosea, naahidi kujirekebisha, namuomba Mungu awe nami katika dhamira yangu hii,”alisema Lulu.

Katika siku za hivi karibuni binti huyu mwenye umri mdogo amekuwa akiandamwa na skendo za mapenzi, kuvaa kihasara na ulevi kiasi cha kuwafanya watu kumhurumia hasa kutokana na ukweli kuwa umri wake na mambo anayofanya ni tofauti kabisa.

Source: www.globalpublishers.info

MY TAKE:

Namwombea kwa Mungu ili awe anamaanisha kweli hayo maneno yake, bado ni binti mdogo sana asiyestahili kupoteza dira ya maisha katika umri alionao.

Jikumbushe vimbwanga vya kabinti haka kwa kubofya hapa.
Kama kakosa mie nshamsamehe.....
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom