Msanii Lady Jaydee atuhumiwa kuhamasisha matumizi ya Bangi kwenye wimbo wake

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,513
9,309
MSANII mkongwe wa Bongo Fleva nchini, Judith Wambura ‘Lady JayDee’ ameingia kwenye hatari ya kufungiwa wimbo wake mpya, unaokwenda kwa jina la ‘One Time’ baada ya kudaiwa kuhamasisha matumizi ya uvutaji wa bangi.

Hatua hiyo imekuja, baada ya Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), kuthibitisha kupokea malalamiko kutoka kwa wadau wa muziki, kuhusu mashairi ya wimbo huo.

Akizungumza na AMANI, Katibu Mtendaji wa Basata, Godfrey Mngereza alisema baada ya kupokea malalamiko hayo, sasa wanaendelea kufanya uchunguzi wa kisheria kuhusiana na nini hasa dhumuni la mstari huo kwenye hiyo nyimbo.

“Tumeliona hilo na suala hili lipo kwenye position ya kufanyiwa kazi, baada ya kuifuatilia. Kwa hiyo, niishie kusema tu kwamba, tunaendelea kulishughulikia jambo hili baada ya kufanya uchunguzi,”

Wimbo huo ambao Jide aliuachia Septemba 14, mwaka huu, unaripotiwa na wadau mbalimbali wa burudani kuwa, maudhui yake yanaonyesha kuhamasisha matumizi ya bangi.

Ndani ya wimbo huo, moja ya mistari yake unasema “Tusmoke weed one time” mstari uliozua utata, hasa kwa wadau wengi wakisema unakiuka maadili na unaonyesha jinsi gani mkongwe huyu ameishiwa mashairi, mpaka kufi kia hatua ya kutoa nyimbo kama hii.

Pia soma> BASATA mfungieni Lady Jaydee anahamasisha uvutaji bangi hadharani
 
Mbona Kuna Nyimbo Nyingi tuu zina hamasisha Watu kula Ndogo Hawajaziona hizo wameona Bangi tuu !?
Mfano; "Baby Papasa kichwaa Mjusi kafiri Nisafishe mtaro"
Mfano: "Watoto wa Mama wanacheza hadi kwenye matope"

Au kula Tigo sio kosa, kosa ni kula Bangi ??
hatr
 
Pamoja na kua mimi siamini uhalali wa mziki lakini huyu dada huwenda kitendo chake cha kukataa kushiriki/kutumbuiza katika kampeni za ccm kitamponza kwa njia moja au nyingine maana ccm wana chuki kama wanazi enzi za hitler.
Ushaanza kuingiza siasa
 
Mbona Kuna Nyimbo Nyingi tuu zina hamasisha Watu kula Ndogo Hawajaziona hizo wameona Bangi tuu !?
Mfano; "Baby Papasa kichwaa Mjusi kafiri Nisafishe mtaro"
Mfano: "Watoto wa Mama wanacheza hadi kwenye matope"

Au kula Tigo sio kosa, kosa ni kula Bangi ??
Tigo ni NYARA ya Serikali
 
Wimbo huo ambao Jide aliuachia Septemba 14, mwaka huu, unaripotiwa na wadau mbalimbali wa burudani kuwa, maudhui yake yanaonyesha kuhamasisha matumizi ya bangi.
ukweli ni kwamba Serikali inamuandama Jide kwakua amekataa kata kata kujiunga na siasa za CCM za maji taka. Ushahidi upo, kuna nyimbo za kipuuzi zaidi na za hovyo sana na hutakaa BASATA waongeee kitu
 
Mbona Kuna Nyimbo Nyingi tuu zina hamasisha Watu kula Ndogo Hawajaziona hizo wameona Bangi tuu !?
Mfano; "Baby Papasa kichwaa Mjusi kafiri Nisafishe mtaro"
Mfano: "Watoto wa Mama wanacheza hadi kwenye matope"

Au kula Tigo sio kosa, kosa ni kula Bangi ??
Next Man Hakuna mtu anayeweza kuamazishwa kufanya ngono kwa kuimbiwa na msanii labda ana tatizo kichwani utaamazishwa ngono labda tu mwanamke kapita sehemu kavaa nusu uchi au kanga moko au kuangalia website za porno
 
Back
Top Bottom