benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,504
- 3,034
Na Ezekiel Kamwaga
Msalaba wa Urais Katika kipindi cha miaka 30 iliyopita, mmoja wa wanafamilia ya Rais aliye madarakani amekuwa akizushiwa tuhuma za rushwa na ufisadi.
Lakini tuhuma hizo hudumu wakati wa urais wa mume/baba/mke/mjomba na husahaulika anapoingia mwingine tuhuma hizo huyeyuka. Mara Nyingi huwa utajiri na ufisadi haujawahi kuonekana wala kuthibitishwa.
Wakati wa utawala wa Rais Mwinyi, tuliambiwa Mama Sitti ndiye kinara wa ufisadi na kwamba ameigeuza Ikulu kuwa pango la wezi na mafisadi. Kuna wakati alianza kufananishwa na Imelda Marcos wa Ufilipino.
TUHUMA
Alipoingia Benjamin Mkapa, Ikawa zamu ya Mama Anna Mkapa. Tukaambiwa Taasisi ya Fursa Sawa kwa Wote (EOTF) ilikuwa inanufaika na Urais na ni kichaka cha wapiga dili. Tukaambiwa Mama Anna ni tajiri wa kutupwa kwa sababu ya ufisadi wa taasisi hiyo.
Alipoingia Dkt Jakaya Kikwete
Ikawa zamu ya Ridhiwani Kikwete. Akiitwa Riz One wakati huo. Tukaambiwa kwamba anamiliki vituo vya mafuta na ana ukwasi usio na maelezo. Nchi nzima kulikuwa na nyumba, vituo vya mafuta na magari yake. JK alipotoka madarakani, utajiri wa mwanaye ukaishia hapo.
Alipoingia Dkt John Pombe Magufuli
Ikawa zamu ya Dotto James. Kila mradi mkubwa, kila uwekezaji na kila tajiri aliyeibuka, ilielezwa kuna mkono wa Dotto. Baada ya Magufuli, Dotto sasa hana shida. Na huo utajiri na ukwasi wake hauonekani popote.
Katika namna ileile ya Mwinyi, Mkapa, Kikwete na Magufuli, kwenye Urais wa Dkt Samia Suluhu
Naona sasa ‘jumba bovu’ linaanza kumwangukia mtoto wake Abdul. Staili ni ileile ya Mama Siti, Mama Anna, Ridhiwani na Dotto. Tuhuma nyingi bila ushahidi. Bila shaka Urais wa Samia ukiisha Tutahamia kwa mtoto/mke/mume/binamu/Kaka wa Rais mwingine atayekuja.
Sidhani kama huu ni utamaduni mzuri kuwa nao. Tunaharibu maisha na afya ya akili ya watu pasi na kujali. Wakati wazazi wao wakiwa marais, Ridhiwani na Abdul walikuwa vijana wadogo wenye umri chini ya miaka 30. Baadhi ya maneno na tuhuma wanazosikia kuwahusu zitawaachia makovu ya kudumu kwenye maisha yao.
Mimi ni mwandishi na nafahamu umuhimu wa kuwa na jamii iliyo tayari kufichua maovu. Hata hivyo, ni muhimu kutenda haki. Hii ‘kawaida yetu’ inaharibu maisha ya watu. Hakuna mtu aliyeomba kuzaliwa na fulani hapa duniani.
Nafahamu machungu ya baadhi ya watu waliowahi kutuhumiwa huko nyuma. Usiombe kupitishwa kwenye hicho kikombe. Leo kwa mwenzio, kesho kwako.
Siasa nyepesi sana hizi, kikubwa lazima watambue kwa nafasi walioko na ukaribu walioko na Rais ni rahisi sana kuzusha mambo kama hayo na kuaminika kirahisi. Hakuna haja ya kuibeba na kuiweka moyoni na kuacha makovu wachukulie ni sehemu ya maisha kwa watu wa karibu na Rais.