Msajili wa Vyama vya Siasa akemea Tamko la CHADEMA

Hutaiona mkuu ni uhayawani tu na mapenzi ya chama kutoka kwa msajili wa vyama. Hizi nafasi bora ziwe zinatangazwa internationally ili tupate expatriate wa kusimamia vyama vya siasa. Wananchi waliitwa malofa na wapumbavu, huyu mgonjwa wala hakusikika kufunua kopo lake! Kule Zanzibar watu wakaitwa Hizbu na Waarabu Koko tena wanaambiwa watoke nchini kwao waende kutawala Oman, huyu mgonjwa hakufunua kopo lake! Wakati wa kampeni Lowassa ametukanwa weeeee huyu mgonjwa bado tu hakuthubutu kufunua kopo lake! Sasa leo anajidai kujua sheria, hebu atupishe huko ni bora angevaa koti la kijani tu ili tujue moja!!
Mkuu yote uliyoandika nilikua nataka niyaandike umeniwahi sina cha kuongeza
 
Za msingi kama zipi?

Mfano,Uhuru wa kujiamulia,uhuru wa kufikiri,uhuru wa kujieleza.Tukumbuke binaadamu tuna hatua tatu muhimu katika maisha,ya kwanza ni kuzaliwa,kuishi na kufa.
Hatua ya pili ni muhimu sana,hatua hii ndio inayoweza kumfanya mtu na taifa lake liendelee au liangamie.kumnyima mtu uwezo wa kufikiri,uwezo wa kujiamulia,uwezo wa kuja na fikra mpya ni kuliangamiza taifa.Mungu ibariki Tanzania
 
Huyu mzee atangaze tujue kama yeye ni mfuasi wa chama cha mapinduzi...
 
Mbona wanaccm wakitoa matamko yanayozuia demokrasia msajili huwa hatoi Tamko?
Thursday, July 28, 2016
JPM kuhutubia mkutano wa hadhara Jumapili. Hii ni kwa mujibu wa Mwananchi jana. lengo la mkutano ni kuwashukuru wananchi kwa kumpigia kura nyingi. Je hii si siasa? Mbona wapinzani wake walikatazwa kufanya hicho ambacho yeye anataka kufanya jumapili? Jamani tusiliingize taifa letu pabaya bure. Tunangoja tamko la Polisi na Msajili wa vyama vya siasa katika hili tupime standard
 
huyu ...endapo ikitokea shida hawezi kukwepa kuwajibika...alafu et ni Jaji...poor judiciary[/quote
Namfahamu tangu akiwa hakimu mfawidhi wa mkoa wa Iringa and he was real good na alikuwa na hofu ya Mungu kwani tulikuwa tunasali naye pale Mshindo roman. Sijui kapatwa na nini kwani hii character take ya sasa ni quet different from what he was before. Nimwombe aurudie utendaji wake na misimamo yake ya nyuma ili kuijenga upya heshima take iliyosalia na ili historian imwandike vyema kwenye kumbukumbu zake. Hivi hajiulizi alikopotelea John Tendwa?
 
Tuache unafiki na Mungu atusaidie, hivi lughu ya kuudhi maana yake nini? kuna mwenyekiti wa chama fulani cha siasa kawafananisha binadamu na ng'ombe waliokatwa mikia lkn msajiri alichekelea kwa kuwa hizo kauli zilitolewa na mfalme. Pia huyo Hugo mheshimiwa aliwaita. wanafunzi wa vyuo kuwa ni vilaza na wanaowatetea (yaani tasisi mbalimbali na wanasisa kuwa nao ni vilaza pia) lkn yeye huyo huyo alivyoitwa kama kilaza alimpeleka mtu kulokoloni akachangiwa faini ya sh 7000000/= milioni saba, na kama haitoshi wabunge wachama chake walitaka kukataa rufaa kwa kitendo cha baadhi ya watu kumchabgia yule mtuhumiwa aliyemwita mheshimiwa k.l.za, sasa kama watu mna bongo za binadamu wala si za kuku tafakarini hii nini?
 
Ungekuwa karibu nami leo nigelifokishwa kwenye faini ya million saba
Wewe achana na huyo mdogo wake Odinga kwani analinda uraia wake pacha. Hana hoja za msingi. Muulize kule kwao Kenya ODM wanafanya nini kwa wananchi na barabarani kila siku? Asijifanye kuijua siasa za bongo zaidi ya za kwao Kenya.
 
Wafute vyama vingi ili ijulikane moja sababu uwezo huo wanao, vinginevyo CDM msikubali kufungiwa ndani hadi 2020. Sheria ipo na uzuri zaidi waliitumga wenyewe. tunaisubiria siku ya mapambazuko ya mtanzania kwa shauku kubwa.
 
Kama kikwete aliwachoma kwa maji sasa wata chomwa kwa moto..maneno sio yangu Makamba Sr.
Na yakashangikiwa sana
Na hawa mawakili watakao kwenda kuwatetea watuhumiwa nao yutawasokomeza mahabusu nao wakateteane huko selo...nayo sio maneno yangu bali ni maneno ya askari mkuu wa upelelezi Msangi kule znz.
Huyu jamaa hakuibuka kukemea...sasa ajenda iongezwe na kumtaka mkuu wa vyama aache kufanya kazi za ccm...aache undumi la kuwili..naye aingizwe katika ukuta kama mzoroteshaji wa democrasia
 
Sababu zilizotolewa na SiSiem kuwa wapinzani wanaogopa Mahakama ya Mafisadi na Ukwepaji wa kodi, hazina mashiko; kwani ESCROW ni ya Wapinzani? No wonder wameteua Msemaji wa Chama aliyepata Division O; ili aweze kuzungumzia mambo ya hoooovyo.
 
Eti, "tangazo la serikali namba 215 la mwaka 2017" wakati ndiyo kwanza 2016. Jaji Mtungi bhana!
 
Mbona viongozi wa ccm wanapomtukana Lowasa na kumuita fisadi hadharani bila ushahidi hajasema kitu? Anajidhalilisha sana huyu jaji, au ndiyo vile kuwa sifa ya kwanza kuwa upande ule ni kujitoa ufahamu.
 
Mbona msajili wa vyama vya siasa huyo huyo hakuwahi kutoa tamko kuhusu kauli ya Magufuli kuzuia mikutano ya vyama vya siasa vya upinzani hadi mwaka 2020, wakati akiruhusu chama chake cha CCM kiendelee na shughuli za siasa wakati msajili akijua wazi kuwa tamko hilo la JPM ni uvunjaji wa wazi wa Ibara ya 3 ya Katiba ya nchi yetu inayoruhusu mfumo wa vyama vingi nchini?

Badala yake katika kumkingia kifua Magu msajili huyo akadai kuwa Rais hajazuia mikutano ya siasa bali vyama vya siasa vya upinzani wamemnukuu vibaya!

Hicho ndicho tunachoweza kuita kuwa msajili wa vyama vya siasa anafanya kazi yake kwa nidhamu ya woga kwa 'kumgwaya' Magufuli kwa kuhofia kumweleza pale 'anapobugi step'

Sasa wewe na Msajili wa Vyama vya Siasa nani anajua zaidi kuhusu sheria ya vyama vya siasa na shughuli za vyama hivyo? Na kumkingia kifua unamaanisha nini?
 
Mbona viongozi wa ccm wanapomtukana Lowasa na kumuita fisadi hadharani bila ushahidi hajasema kitu? Anajidhalilisha sana huyu jaji, au ndiyo vile kuwa sifa ya kwanza kuwa upande ule ni kujitoa ufahamu.

Tuweke kumbukumbu sawia: Walioanza kumuita Lowassa Fisadi ni CHADEMA wakiongozwa na Dr. Slaa, Lissu, Lema, Mnyika na wengineo kuanzia pale Mwembeyanga, September, 2007. Labda kama wewe kipindi hicho ulikuwa darasa la kwanza. Hivyo CCM wanarudia tu kile kilichosemwa na CHADEMA.
 
Wakati mikutano ya vyama vya siasa ikipigwa marufuku wakati anajua wazi ni kinyume cha sheria ya nchi alikaa kimya na sasa tunamwomba akae kimya kwasababu hajui wajibu wake.
Mkuu wakati mikutano ikipigwa marufuku yeye alikuwa busy akizungumza 'kama msemaji wa serikali'. Hakuona vifungu vya sharia

Leo anasema uchochezi, hivi kutangaza mikutano kwa chama cha siasa ni uchochezi?

Halafu kwenye barua anasema, vyama viepuke kuchonganisha umma na serikali. Yaani tayari ameshaju kitazungumzwa nini.

Kauli hiyo ni kama 'mseamji wa serikali' yeye si msemaji wa serikali ni msajili wa vyama. Hana sababu zozote za kuingilia shughuli za taasisi nyingine

Kama hatutakuwa na katiba mpya ya wananchi, haya yataendelea kila siku

Vituko nchi hii haviishi
 
Back
Top Bottom