Msaada wenu tafadhari juu ya afya ya mwanangu

Isaac1

Member
Nov 12, 2018
79
70
Habari ndugu zangu wiki kama moja iliyopita mwanangu alilazwa na akachomwa sindano nyingi sana mikononi ni mtoto wa miezi 11.

Sindano zile zilimpelekea kuvimba mkono kwa juu nilivyowauliza hospital wakanijibu hali hiyo itaisha nimesubiri kwa muda wa siku nne sioni dalili za hali hiyo kuisha nikamua kwenda private hospital kupata ushauri.

Nikaambiwa kuwa inabidi apasuliwe mkono maana wanadai kuwa ndani pametengeneza kama jipu.
Nikawajibu acha nirudi kesho.

Kabla sijachukua maamuzi nikaona nitafute Dkt mwingine anipe ushauri pia yeye akaniambia kuwa mtoto kama huyo mishipa yake ni midogo sana kwahiyo kupasuliwa kunaweza kusababisha madhara zaidi akanipa dawa kuwa itamsaidia.

Sasa hapa nimebaki njia panda nimeona nije kwenu hapa maana naamini hapa kuna watu wengi wenye ujuzi na elimu tofauti asanteni.

IMG-20240325-WA0009.jpg
 
Duuh asee malezi ni mtihani mwanzo kabla ya kupata mtoto nilikuwa naona ni kitu simple ila baada ya kulea nakiri hakuna kazi ngumu kama kulea.

Mkuu pole sana asee jaribu kutafuta doctor ambaye atakuwa na moyo wa kukusaidia mana walio wengi ni pesa mbele.
 
Ilifaa umchue tu kwa spirt soon baada ya kuona hilo tatizo, itakua nurse alikosea kumchoma sindano dawa ikaenda kwenye nyama badala ya veins kwa ushauri tafuta kitambaa mchue kwa pamba ili dawa isambae sambae atarudi sawa.
 
Hiyo iliyoandikwa Flumox ndo nimeambiwa kuwa ni ya kuondoa huo uvimbe, sasa sijui nimsikilize huyu aliyenipa dawa au huyu aliyesema apasuliwe.View attachment 2944377
Pole. Inaonyesha kwenye kumchoma sindano kuna kosa lilifanyika. Uko sehemu gani? Kama ni Dar kuna hopsital zenye ma-specialist wa watoto au kuna specialist wenye hospital za watoto tu. Mpeleke.

Angalia sana kwa sababu hospital nyingi siku hizi hawana utu, hasa hivi vya mtaani.
 
Jitahd umpeleke kwa paediatrician mzuri mapema.

Worst case scenario anaeza kupata gangrene ambayo madhara yake siez kukwambia maana unaeza kupiga uuuwwwii barabarani
 
Back
Top Bottom