msaada wanajf kuhusu haya maneno!

Jakubumba

JF-Expert Member
Mar 5, 2011
1,624
500
Kuna haya maneno ya kiswahili yananisumbua sana tangu nasoma hadi sasa,nitofautishie tafadhali hata kwa sentesi.
1.Kuona
2.Kutazama
3.Kuangalia


Mfano,
.Juma alienda kuangalia mpira
.Juma alienda kuona mpira
.Juma alienda kutazama mpira

so ni sentesi ipi sahihi hapo?
 
Sipendi kuona (shuhudia) watu wakipigana.
Sipendi kutazama (kuangalia) watu wakipigana.
Sipendi kuangalia (tazama) watu wakipigana.
 
Nikusaidie kiduchu. Ingekua katika lugha ya kiarab ungeelewa zaidi. Lakin kwa swahil yote yanafaa.
1-Kuona ni kitu uumeona kwa ghafla. Mfano ulitoka nje ukaona mtu.
2-kutazama ni kukuta kitu umesha kiona unaendelea kutazama.
3-kuangalia umesikia kitu ukaenda kikiona kisha ukaendelea kukiangalia. Hapa mara nyingi kuangalia ni kwa umakin zaid. Kama ulikua hutarajii kumuona juma sasa ulipomuona ukaendelea kumuangalia. Ukitafuta uthibitisho.
Nimejarib kueleza kwa ufupi.
 
Kuona ni kitendo cha uweza wa kutumia macho kuona yaani ni kitendo cha kimaumbile hata km hujakusudia lazima uone madhali macho yapo na sio kipofu. Kuangalia na kutazama ni neno moja sema angalia zaidi inatumika bara na tazama ni huku kwetu Z'bar na maana yake ni kudhamiria kutazama au kusudia kutazama. Hapa hata mwenye matatizo ya macho anwea kutazama.
 
mantiki ni moja ila matumizi ni tofauti,

kwa kingereza

ona- see
tazama-look
angalia-watch

nadhani tuko pamoja sasa
 
Back
Top Bottom