Msaada wa kupata shule na maelekezo

Majita

JF-Expert Member
Jan 13, 2008
609
190
Ndugu wanaJF wenzangu,habari zenu.
Samahani naomba mnisaidie maelezo ama jinsi ya kupata shule A level Tanzania.Maelezo ni kuwa nina mdogo wangu yuko Mwanza ambae namsomesha.Matokeo yake ya O level hayakuwa mazuri,so alikosa credits 3 ambazo ni C tatu kwa ajili ya kuendelea na masomo yake ya A level.Zamani kidogo nikiwa Tanzania tulizoea kuona wanafunzi wakienda private na wakiwa form five wana-reseat masomo ya O level kwa ajili ya kupata credits hizo ambazo hawakuwa nae.Nimeongea nae amesema kuwa siku hizi utaratibu huo haupo.Naamini kuwa hapa kuna watu ambao wanaujuvi na mambo hayo na wanaweza kunisaidi namna ama kunishauri jinsi ya kufanya.

Nasubiri kwa hamu kupata ushauri wenu ndg zangu ikizingatiwa kuwa sasa hivi muda wa kuanza form five unakaribia so najiandaa.Nia yangu ni kumsaidia huyu bwana mdogo kielimu zaidi ya kitu chochote.
Natanguliza shukurani na nitashukuru kama nitapata na shule ambako wanaweza kumpokea kwa huo ushindi alionao wa chini ya C tatu na ningefurahi kama itakuwa ni Mwanza,shinyanga au Musoma ili kuokoa gharama kwa ajili ya usafiri.Nikipata boarding nitafurahi zaidi.Ni mtoto wa kiume.
Regards
 
Kumbe utaratibu huo haupo siku hizi? Kwa maoni yangu, ni vyema atafutiwe center wanakofundisha wale wanao reseat badala ya kutafuta shule itakayompokea bila credit tatu. It is motivating to be with others who are planning to reseat as opposed to be in a form five class. He will be affected (negatively) psychologically being in a form five class. Ajiunge na form five baada ya kupata credit 3.

.
 
asipokuwa na credit tatu sidhani kama ataruhusiwa kufanya mtihani wa kidato cha sita. Utakuwa umepotezea muda na pesa vile vile.
 
labda unaweza kumpeleka private? Kama credit tatu zinatakiwa kufanya form6 them mpeleke ambayo wanafuata "International" standard. Ila sijui kama hawa wanaweza kuingia UDSM wakimaliza.
 
Ndugu wanaJF wenzangu,habari zenu.
Samahani naomba mnisaidie maelezo ama jinsi ya kupata shule A level Tanzania.Maelezo ni kuwa nina mdogo wangu yuko Mwanza ambae namsomesha.Matokeo yake ya O level hayakuwa mazuri,so alikosa credits 3 ambazo ni C tatu kwa ajili ya kuendelea na masomo yake ya A level.Zamani kidogo nikiwa Tanzania tulizoea kuona wanafunzi wakienda private na wakiwa form five wana-reseat masomo ya O level kwa ajili ya kupata credits hizo ambazo hawakuwa nae.Nimeongea nae amesema kuwa siku hizi utaratibu huo haupo.Naamini kuwa hapa kuna watu ambao wanaujuvi na mambo hayo na wanaweza kunisaidi namna ama kunishauri jinsi ya kufanya.

Nasubiri kwa hamu kupata ushauri wenu ndg zangu ikizingatiwa kuwa sasa hivi muda wa kuanza form five unakaribia so najiandaa.Nia yangu ni kumsaidia huyu bwana mdogo kielimu zaidi ya kitu chochote.
Natanguliza shukurani na nitashukuru kama nitapata na shule ambako wanaweza kumpokea kwa huo ushindi alionao wa chini ya C tatu na ningefurahi kama itakuwa ni Mwanza,shinyanga au Musoma ili kuokoa gharama kwa ajili ya usafiri.Nikipata boarding nitafurahi zaidi.Ni mtoto wa kiume.
Regards

Majita, hata kama utaratibu huo upo au ungekuwepo ingekuwa si busara kumpleka Form % akiwa hana credits za kutosha. wakati ikiwa Form 5 na 6 utaratibu ule wa kusoma A level na kutafuta credit za O level uliwagharimu wanafunzi wengi kwani hadi tunamaliza wengine hawakuweza kupata hizo credit na wale waliopata tukiwa Form 6 walipata taabu zana kupata namba za mitihani hadi wakajikuta wanafany mitiahani ya A level mwaka uliofuata na hapo ndo maana NECTA wakapiga marufuku.

Nakushauri kuwa umtafutie shule nyingine ya private ili arudie mwaka mzima na afanye mtihani wa Form 4 akiwa kama mtahiniwa binafsi.

Nimefanya hivyo kwa wadogo zangu wa wawili, mmoja ameshamaliza Chuo Kikuu kwani baada ya kurudia shule na kupata credit nilimpeleka A level na akafaulu vizuri na mwingine anasubiri matokeo.
 
Mhhh sidhani kama hicho kitu cha kuresit kama umefel O-level hamna labda wawe wamebadilisha mwaka huu..........Maana nina bwana mdogo wangu na yeye aliferi O-Level mwaka 2006 ikabidi 2007 arudie masomo alitofeli tena ni Makongo.....Mimi ninavyojuwa anaweza kurudia lakini kama hicho kitu hamna ndio kwanza nasikia sasa hivi hapa kwenu ila labda tusubiri majibu ya wadau wengine watasemaje
 
ndgu zangu nashukuru sana kwa ushauri.
Kaka Ibra nakushukuru sana kwa maelezo.Mimi nilikuwa na wazo hilo la kumpeleka form five halafu akiwa huko ndo a-reseat masomo yake alofeli.Nashukuru sana kwa maelekezo yenu mazuri na nasubiri kusikia zaidi
 
Back
Top Bottom