Jaamani Habarinii za asubuhi!!kuna hili swala la hawa wafanyakazi wa eroplink.Kuna Bank Moja maarufu jina kapuni nilibahatika kufanya kazi mwaka mmoja chini ya hii kampuni ya erolink bahati nzuri nikaajiriwa sehemu nyingine,cha kushangaza mpka sasa wale wenzangu woote zaidi ya 50 bado wapo mpka leo chini ya erolink,wananyanyasika,wanakosa haki zao za msingi,wengine wamewekwa kwenye idara nyeti lakini cha kushangaza wapo temporay mwaka wa pili unaisha sasa,no fringe benefits kama medical allowance,housing allowance,na pia hata zile pension zao inasemekana hawazipeleki sehem husika!!mshahara unamegwa mpka unabaki mdogo ambao huo huo atoe hela ya kodi,matibabu na mambo mengine,MIKATABA YAO SASA NDO HATARI!kila baada ya miezi mitatu wanarenew unakuta mtu toka ameanza ana miaka miwili ila hajui hatma ya ajira yaka baada ya miezi mitatu mbele,wanaenda tuu kwa sababu wanashida na ajira zimekuwa ngumu,swali langu wanasheria,hivi ni sahihi hii aina ya ajira inavyokwenda?na ni sahihi mtu kuwa temporary zaidi ya miezi sita?msaada jamani!