Hismastersvoice
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 18,808
- 22,512
Marekani iliwahi kulisha chakula shule zote za Tanzania, hawakuishia hapo tu, wakatulisha yanga watanzania wote.Haya ni maoni yangu, nyuma ya huu msaada lazima kuna jambo ambalo hatulijui..
Wasiwasi wangu ni kwamba usalama wa hiki chakula upoje , kwanini kiletwe toka marekani?
Kwanini hawaja taka kuja kununua Tanzania ambapo kuna mchele kibao, hadi wautoe marekani?
Unaweza kuta jumla ya fedha zilizo tumika ni sawa na kujenga barabara toka dar hadi mlanzi, au kujenga hospitali 5 kama za benjamini mkapa.dodoma. kwanini wasilete fedha kusaidia maendeleo.
Siku moja niliwasikia wajeda wa JWTZ wanazungumza huko dodoma kwenye mashamba yao wakisema wanashiriki shughli za kilimo kwa sababu ni sehemu ya ulinzi na usalama wa nchi, mnaweza poteza nchi kwa kutumia chakula..
Pia nahisi kwamba marekani inaitangazia dunia kwamba Tanzania tuna afya mgogoro na njaa kama somalia au sudani wakati mahindi na michele i aozea shambani huko kilombero.. hapa nimemkumbuka Magufuli, asinge kubali haya mambo.
Tanzania sio maskini n wala hatuna njaa, tunauwezo wa kutoa msaada wa chakula hata marekani.. RIP Magufuli..
Tunaomba waziri bashe aje ajibie swala hili, imekuaje wapokee mchele huo, kwanini wasingeleta fedha hata kama wanasema kuna virutubisho.
Taifa salama ni lile linalo jitisheleza kwa chakula.
View attachment 2935710