Msaada tutani, ramani na fundi mbobevu wa kujenga nyumba za kupangisha

Aigle

JF-Expert Member
Jul 4, 2020
711
6,187
Habarini..

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, kama nitaweza kupata ramani zinazoonesha ujenzi wa nyumba (unit) za kupangisha pamoja na lodges nitashukuru.

Pia kama ni FUNDI mbobevu wa ujenzi na umeshafanya project hizo za nyumba za kupangisha pamoja na lodge nzuri yenye muonekano mzuri wa kisasa na kuvutia, basi karibu tuyajenge, na pia uwe tayar kunionesha hizo project ulizofanya. Tafadhali tusidanganyane, usichuke picha mahali halafu useme unaeza ujenzi na kiuhalisia huwezi, bora uache tusije sumbuana mwisho wa siku, sababu fundi ujenzi mzuri kazi zake zinajieleza.

Ramani ndani iwe hivi, chumba kimoja ambacho ni self, sebule, na jiko. Hii ni kwa nyumba za kupangisha, ambazo nataka iwe kama mstari wa vyumba saba upande mmoja, na saba upande mwingine. Na nje kue na public toilet.

Akhsante.
 
Ramani ni wazo /mawazo, mtaalam atafanya kuhamishia kwenye karatasi na kuboresha, Ili kipatikane kitu Bora zaidi na kinacho vutia.

Wewe huna Idea ya unacho taka ?

Vyumba vya kupanga sawa.
Ziwe je? Ikae msitari kama Shule?
Je ikae chumba na sebure?
Je choo , kiwe nje ,au Kila chumba na choo chake?
Au chumba kimojakimoja?


Je unatani two in one? room 2 sting, kitchen na toilet 🚽 humo humo?

Ukisha jipatia maji ndena kwa wachoraji wa ramani watakusaidia.

Fundi ahusishwe ukiwa na ramani Yako mkononi.
 
Unachotakiwa kufanya, jaribu kuweka mchoro kwa kile unachokihitaji; tafuta mtaalamu akutengenezee ramani pamoja na vipimo.

Nunua mali ghafi; anza ujenzi; mafundi ni wengi sana
 
Mimi nifundi wa kutengeneza madirisha ya aluminum milango kabati na shelf Kama Kuna kazi tujulishane tufanye kazi kwa Bei nafuu
0745866224,0629985887
 
Back
Top Bottom