Mrejesho: Biashara ya Nyumba za Kupangisha Vs Nyumba za Kulala Wageni

Grahams

JF-Expert Member
Mar 19, 2016
11,103
34,229
Mwishoni mwa Mwaka 2022 nilianza Ujenzi wa nyumba ya Kulala Wageni.

Ni Moja ya biashara niliyokuwa naifikiria Kwa muda mrefu. Nilianza Ujenzi Kwa kudunduliza kama ilivyo desturi ya Wajasirimali wengi Nchini. Nilikuwa na akiba ya shilingi 35M wakati naanza, ambapo nilianza Kwa kununua Kiwanja ambacho kilikuwa kipo katikati ya Makao Makuu ya Wilaya. Kiwanja kina Ukubwa wa mita 35 Kwa 43.5.

Kilinigharimu kiasi cha shilingi 11.8M kukinunua.

Bahati nzuri nilisanifu mwenyewe ramani niliyodhani ingefaa kujenga nyumba ya Wageni pamoja na mahitaji muhimu ya mashimo ya Maji machafu/Parking n.k

Niliweza kupata ramani ya vyumba 10 pamoja na Chumba cha Mhudumu/stoo/Public Toilet n.k

Baada ya kukamilisha taratibu za Vibali kutoka Halmashauri nikaanza Ujenzi. Nilitafuta Mafundi Kwa makundi kadri ya mahitaji.

Ujenzi uliweza kuchukua miezi 12 hadi kukamilika kwake. Hii ilitokana na Changamoto ya Fedha.

Nashukuru Mungu Mwaka Jana Mwezi September, 2023 nilikamilisha Mradi wangu wa Lodge ikiwa na accessories zote tayari Kwa kuanza kutoa huduma.

Jumla ya gharama nilizotumia zimefika shilingi 110,787,700TShs.

Baada ya kuanza huduma trend ya Mapato ghafi ilikuwa shilingi millioni 3.6 Kwa Mwezi.

Ambapo nimekadiria kuweza kukusanya shilingi 43,200,000 Kwa Mwaka ambapo nimechukulia kuwa Kila Siku watalala Wageni 4 kati ya Vyumba vyote 10.

Ikitokea wamelala wateja 10 itasaidia kufidia Siku ambazo hakutakuwa na mteja aliyelala ama walipolala pungufu ya Idadi tarajiwa.

Hata hivyo ninatumia kiasi cha shilingi 987,000 Kwa Mwezi kwaajili ya Mishahara pamoja na gharama nyingine za Uendeshaji sawa na shilingi 11,844,000 Kwa Mwaka.

Ili kujua kama fedha niliyowekeza itarudi ama itapotea nilijaribu kufanya tathmini Kwa kuangalia;

~Muda wa Kurejesha kiasi cha fedha nilichowekeza (Payback Period on investment)

Ambapo nilichukua kiasi cha Mtaji nilichowekeza÷Kiasi cha Faida ninachokadiria kupata kama Faida

=110,787,700/31,356,000
PBP= 3.53Years

Utaona naweza Kurejesha kiasi nilichotumia kwenye Uwekezaji wangu Kwa kipindi cha miaka 3 na nusu hivi.

VIPI KAMA INGEKUWA NYUMBA YA KUPANGISHA?

Gharama ningetumia hizo hizo ama zingepungua kidogo Kwa kuondoa gharama za Kununua TV/Magodoro/Vitanda/Ving'amuzi n.k ambapo pengine ingepungua labda 16M kutoka kwenye gharama za awali ya shilingi 110,787,700 na kuwa 94,787,700

Hivyo kupata muda wa kurudisha fedha uliyotumia kuwekeza ukizingatia bei ya Chumba self chenye hadhi hiyo hutozwa shilingi 60,000 Kwa Mwezi

Hivyo ningezalisha kiasi cha shilingi 600,000 Kwa Mwezi Kwa Vyumba vyote 10 na shilingi 7,200,000 Kwa Mwaka.

Hivyo Payback Period yetu ingekuwa = 94,787,700÷7,200,000
Miaka 13.2 hivi

Kwa kuifanya Nyumba ya Kupangisha ingenichukua miaka 13.2 hivi kuweza kurudisha Mtaji wangu wote niliyowekeza.

Kwa Kuhitimisha utaona Biashara ya Lodge ina unafuu Mkubwa kwenye Uwekezaji hasa Kwa kuangalia muda mchache wa kurudisha fedha uliyotumia kuwekeza (3.5yrs) kuliko Biashara ya Nyumba za Kupangisha(13.2yrs).

Nimeambatisha mchanganuo wa gharama nilizotumia,Mapato na Matumizi niyafanyayo (O&M).

Changamoto nilizopitia kwenye Biashara hii ni;
....Kutoaminika na Mabenki hasa kwenye start up project. Mabenki hayakopeshi Kwa biashara inayoanza ila Kwa biashara inayoendelea.

.....Wizi Kwa Wahudumu, licha ya kufunga CCTV Camera bado Mhudumu anaiba Kwa kuharibu Camera isifanye kazi.

All in all Biashara ya Lodge ni nzuri sana hasa Ukipata eneo lenye Mzunguko Mkubwa wa Watu.
 
Attachments

  • Lodge.pdf
    90.8 KB · Views: 23
  • Lodge II.pdf
    88.5 KB · Views: 18

All in Biashara ya Lodge ni nzuri sana hasa Ukipata eneo lenye Mzunguko Mkubwa wa Watu.
Moja ya application ya shule ni hii....
Hongera sana mkuu!
 
Asante Mkuu, ila Benki zinasumbua sana kwenye kutoa Mikopo Kwa biashara mpya.

Kuna haja Wizara ya Fedha/Benki Kuu wakalegeza masharti kwenye hizo Taasisi za Kibenki

Vinginevyo ndogo za Wajasirimali wengi zinakufa
Nadhani wako sahihi kwa upande flani,, huwezi ukampatia mtu hela bila kujiridhisha kwanza biashara yake kama inaweza kuingiza kiasi cha rejesho husika. Na inasaidia pia kumpunguzia risks mkopaji maana biashara mpya hadi ije isimame sio mchezo mchezo
 
Nadhani wako sahihi kwa upande flani,, huwezi ukampatia mtu hela bila kujiridhisha kwanza biashara yake kama inaweza kuingiza kiasi cha rejesho mhusika. Na inasaidia pia kupunguza risks mkopaji maana biashara mpya hadi ije isimame sio mchezo mchezo
Ni kweli....nina Mameneja baadhi wa Benki nafahamiana nao walinipa hii sababu.
 
Usiruhusu wakukadirie utapigwa kodi zisizo na kichwa wala miguu. Fungua kampuni uwe unajikadiria mwenyewe (kwa kutumia wahasibu) kila mwisho wa mwaka kwa kuangalia mapato na matumizi!
Sawa

Japo Kwenye hili nilimfata Meneja Mmoja nafahamiana naye alinisaidia kunipa favor kidogo.

Vinginevyo hali ingekuwa mbaya Mkuu hasa Kwa startup project
 
Back
Top Bottom