Msaada tafadhari, kwani maisha nayaona magumu sababu ya afya yangu

Sajunne

Senior Member
Jul 19, 2011
104
58
Wadau Habari zenu, Mimi ni kijana wa kiume Nina umri wa miaka 18-22 nimekuwa nikisumbuliwa na maradhi mbali mbali, typhod, malaria ,tumbo kujaa gesi , kutokupata choo, mwili wote unauma na maradhi hayo yamekuwa yakinisumbua mara kwa Mara, ni muda sasa na nimekuwa sina utendaji mzuri ktk shughuli zangu mbali mbali. Msaada tafadhari ninaamini nitapata ufumbuzi.
 
Nenda hospitali,huduma na ushauri wa kitabibu utakusaidia zaidi.Fanya hilo kwanza.Na ukumbuke kumuomba Mungu akusaidie.
 
typhoid acha kula kachumbari safisha matunda vizuri na pia jitahidi kula vyakula visivyokuwa na gesi. kunywa maji mengi
 
Wahi hospital ukapate matibabu na ushauri nini ufanye...thn pendelea sana mazoezi na kunywa maji mengi,ni tiba asili hiyo.
 
Wadau Habari zenu, Mimi ni kijana wa kiume Nina umri wa miaka 18-22 nimekuwa nikisumbuliwa na maradhi mbali mbali, typhod, malaria ,tumbo kujaa gesi , kutokupata choo, mwili wote unauma na maradhi hayo yamekuwa yakinisumbua mara kwa Mara, ni muda sasa na nimekuwa sina utendaji mzuri ktk shughuli zangu mbali mbali. Msaada tafadhari ninaamini nitapata ufumbuzi.
Pole sana kwa hayo matatizo yako ilikuwa kabla ya kuja hapa Uende Hospitali kisha utibiwe na Ma-Dakatari utumie Dawa za Hospitali usipo pona ndio uje hapa utushitakie matatizo yako sio tu unakuja hap ana kueleza matatizo yako kabla ya kwenda Hospitali tutawezaje kukusaidia namna hivyo? Fanya hivi Kila Siku unapo amka Kabla ya kula kitu kunywa Maji ya Uvuguvugu Glasi 2 kisha baada ya kupiga mswaki kunywa tena maji ya uvuguvugu glasi 1 kisha kaa bila ya kula kitu au kunywa kitu kwa muda wa saa moja kisha waweza kula chakula cha asubuhi. Inapofika mchana kunywa tena glasi 2 ya kaji ya uvuguvugu kisha kaa kwa muda wa saa 1 bila kula kitu kisha baada ya hapo waweza kula chakula cha mchana. Nainapofika wakati wa usiku kunywa tena glasi 1 ya maji ya uvuguvugu kisha usile chakula baada ya saa moja waweza kula chakula na wakati wa kulala kunywa maji ya uvugvugu glasi 1 kisha lala fanya hivyo kila siku utapona hayo maradhi yako.

Dawa ingine tumia hii pendelea kula matunda na mboga za majani pia zitakusaidia matatizo ya kutopata choo kwa wepesi.

HOMA YA MATUMBO (Typhoid fever)
Ni ugonjwa unaoenezwa na bacteria jamii ya salmonella. Huenezwa kupitia maji yasiyo salama,chakula na kupitia mtu mwenye vjidudu hivyo bila dalili.

DALILI: Awali ni kama za malaria. Kujisikia joto linalopanda hadi kufikia 103-105F (39-40¬¬¬¬C), maumivu

ya kichwa,misuri, na kukosa hamu ya kula. Baada ya juma kama mbili hivi kuharisha kwaweza kuanza. Kama

matibabu hayatatolewa mgonjwa atazidi kuathilika hatimaye kifo.

TIBA ZAKE: Chagua Dawa mojawapo kwako wewe itakuwa ni Rahisi kuitumia na kuipata.


  • Miche ifwatayo itumike kumpa enema mgonjwa au kumpampu kwa njia ya bomba la sindano. Wakia mbili au cc 50-60 za dawa majani ya Red respbarry, magome ya White ork, au Magome ya mninga au Wild alum mizizi.
  • Songwa, ni mmea wa mashambani sio mti: Chuma majani 10 au kijiko kimoja cha chai kama imesagwa kuwa unga, koroga katika glasi moja ya maji moto. Ikiwa ni majani pika maji yachemke, kisha epua, ndipo uyatie hayo majani katika hayo maji mara moja, yakipoa kunywa.
    Dozi hiyo ni kwa siku 10 hadi 14. Dozi: Wazima kikombe 1 cha chai kutwa mara tatu kwa siku 7—14 kutegemea na ugonjwa. Vijana zaidi ya miaka 12 nusu kikombe cha chai kutwa mara tatu. Miaka 6-12 robo kikombe kutwa mara tatu Miaka 2-5Kijiko kikubwa mara tatu kutwa.
  • Msongwa; mti mkubwa wenye kutoa matunda yenye uchachu. Chemusha magome yake au yasage uwe unga.
    Dozi; Gome la ukubwa kiganja lichemshwe katika maji bilauri 6 kwa dakika 10, kisha kunywa vipimo kama namba mbili hapo juu.
  • Aloe vera; tumia dozi hiyo mara mbili. chemsha uwe unakunywa kutwa mara 2.
  • Tangawizi na jira; Saga viwe unga, tumia kijiko kimoja katika glasi moja la maji x2 kutwa. Pia tatizo la kuhara damu na la Amoeba tumia hiyo hiyo..
  • Sogoya:, nao ni mmea wa mashambani sio mti: Chuma majani 10 au kijiko kimoja cha chai kama imesagwa kuwa unga, koroga katika glasi moja ya maji moto. Ikiwa ni majani pika maji yachemke, kisha epua, ndipo uyatie hayo majani katika hayo maji mara moja, yakipoa kunywa. Dozi hiyo ni kwa siku 10 hadi 14.



aloverab.jpg

Aloe Vera Mshubiri


Dawa ingine ya Maradhi ya Typhoid: Tiba Mbadala Tafuta Mzizi wa Mlonge (Moringa Oleivera)Saga unga wake na kutumia kijiko cha chai mara tatu kwa siku


Pole sana mkuu!! Ndugu yetu MziziMkavu tafadhali msaada wako wahitajika hapa!!
 
Pole kaka jitahidi kula vyakula vilivyo salama na jitahidi kunywa maji mengi mungu atasaidia....
 
?

Mh kachumbari Typhoid ?

yesu na maria!!! jamani tena hupati typhoid tu na amoeba, yale maji wanayooshea hivo viungo je yanachemshwa..... nilipita sehemu moja ya kula kiherehere changu cha kutaka kujua mengi nikachungulia jikoni hayo maji wanayotengenezea kachumbari ni meusi sana ni balaaa!!!!, ukiangalia kucha mmmmh nisiseme sana...... kama za kupikwa sawa hizi hazipikwi mmmmmhhh si sawa
 
Back
Top Bottom