Msaada nina mtaji wa Tsh.5 milion nifanye biashara gani?

Ndele

Member
Dec 27, 2008
82
7
Wanajamii ninaomba msaada wa kibiashara nina milion hizo nashindwa nifanye biashara gani kwa wale wataalamu wa biashara wanishauri
 
yaani sijajua nifanye biashara gani kwani tangu nianze kani sijawai fanya biashara aina yeyote! ila kutokana na maisha yanavyozidi kuwa magumu imenibidi niwe na wazo la biashara
 
nunua mawese uwe unapeleka hapo ng'ambo Burundi.vilevile unaweza kufanya biashara ya dagaa kutoka kigoma kwenda mikoa mingine kama mwanza ,shinyanga,hasa geita.
 
Mkuu zipo biashara nyingi saana za kufanya
Kitakacho determine ufanye nini inategemea na mtaji,mahali unapoishi, interest, muda wako utakaowekeza kwenye hiyo biashara-Kumbuka kama wewe ni muajiriwa kuna baadhi ya biashara zitakushinda mfano kutoa bidhaa hapo kigoma na kupeleka mikoa mingine,

Chakufanya pitia hili jukwaa kuna MADA ya member moja anaitwa MBU- isome kuna michango mizuri saana, kuna mada za ufugaji wa kuku-wa kisasa na kienyeji, ukizisoma zote ka makini hutatoka kapa

Cha msingi huo mtaji ulionao unatosha kabisa kuongeza kipato, anza kuangalia mazingira unayoishi lazima kutakuwa na opportunities kibao, angalia watu wanakula nini, wanakunjwa nini, kipato chao, aina ya maisha watu wanayoishi,mila na desturi, ukiyafanyia kazi yote hayo naamini lazima utapata idea ya ni biashara gani ya kufanya. angalia kama ijumaa na jumamosi kunakuwaga na harusi nyingi- unaweza anzisha kabiashara ka upambaji, kama hakuna maduka ya vyakula unaweza fungua retail shop, kama kuna baa unaweza fikiria vinjwaji vya jumla na rejareja..

pia unaweza fikiria biashara ya ngua,,unaweza uza nguo za watoto, vijana, mali unaweza pata kariakoo kwa bei rahisi tu... ukishindwa yote hayo nunua pikipiki

kila la kheri
 
nashukuru sana mkuu prodigal son kwa ushauri wako mzuri ebu nisome hizo post
 
yaani sijajua nifanye biashara gani kwani tangu nianze kani sijawai fanya biashara aina yeyote! ila kutokana na maisha yanavyozidi kuwa magumu imenibidi niwe na wazo la biashara

Wewe binafsi unapenda nini?
Una uwezo kufanya nini?

Ukishajua hayo..nenda hatua mbele zaidi kuangalia je hicho unachotaka kufanya na una uwezo kukifanya ni kitu kitakacho"uzika" ?Maana biashara siyo sadaka.Unataka ufanye faida.
Hayo ni ya msingi kujua kabla ya kuangalia pesa.

Usianze na " nina sh. million 5..nifanye nini" Hii ni sawa na kuanza na mkokoteni mbele ya punda au farasi. Halitaenda.
 
Wewe binafsi unapenda nini?
Una uwezo kufanya nini?

Ukishajua hayo..nenda hatua mbele zaidi kuangalia je hicho unachotaka kufanya na una uwezo kukifanya ni kitu kitakacho"uzika" ?Maana biashara siyo sadaka.Unataka ufanye faida.
Hayo ni ya msingi kujua kabla ya kuangalia pesa.

Usianze na " nina sh. million 5..nifanye nini" Hii ni sawa na kuanza na mkokoteni mbele ya punda au farasi. Halitaenda.

kabisa
mtaji wa kwanza kwenye biashara ni wewe mwenyewe....sio pesa
 
Ikitokea ukaishiwa pesa,nenda pale JWTZ makao makuu. Muone kuna mshkaji mmoja ana kama Trilion 3 hivi na ushee. Kama una propozo fresh, uongo, atakutoa
 
Nashukuru sana wana jamvi! kimsingi wazo langu la mwanzo ilikua kwenda kusoma masters ndo maana nilitafuta hiyo pesa kwa mda mrefu kidogo! lakini nilipoomba kwa mwajiri wangu amedai nisubiri miaka miwili ndo nitaruhusiwa kwenda kusoma.sasa nikawa najiuliza hizi pesa kwa mda huu nizifanyie nini? wengine walinishauri niziweke na wengine wakasema nizungushe kwa kufanya biashara ndo maana nikaamua kuuliza ni biashara gani za kufanya. lakini baada ya michango ya watu wengi naona biashara ya kufuga na kuuza kuku wa kienyeji au kitimoto naweza kuimudu kwa kulingana na nafasi ya kikazi.NAOMBENI NISHAURINI KWA HAYO. japo biashara ya kuku wa kienyeji ndo naendelea kuisoma kwenye moja ya topiki zilizopo humu jamvini.
 
<outside the box>

Unaweza ukanunua hisa za shirika fulani e.g. CRDB. I know a friend alinunua baada ya miaka 2 zika double. Tafuta mashirika yanayouza hisa chagua lenye good future prospects nunua hisa za kama milioni 4 kaa nazo kama mwaka au miaka miwili mostly utakuwa na kama milioni 7 au 8. Its not that simple but it is possible.

Au unaweza ukaatafuta tenda ya ku spply bidhaa fulani kwenye shirika au taasisi fulani kana vile ku supply certain items UNHCR (sijui kama bado wapo kule Ngara)

si lazima ufanye biashara ambazo ni too obvious zinazofanywa na kila mtu.
 
Ndugu ndele nakushauri rudisha pesa yawatu biashara sio ndoto. If you can not count from one to ten how you can manage to count from thousands to millions?
 
nunua mawese uwe unapeleka hapo ng'ambo Burundi.vilevile unaweza kufanya biashara ya dagaa kutoka kigoma kwenda mikoa mingine kama mwanza ,shinyanga,hasa geita.

mkuu ni risk kama huyu mtu hana exprience ya biashara,lakini ni mtanzania gani huyu hajawahi fanya biashara??mkuu wewe ni mkimbizi?
 
Back
Top Bottom