tindikalikali
JF-Expert Member
- Jan 14, 2011
- 4,855
- 1,117
Sijisifu lakini najijua jinsi nilivyo na moyo wa uvumilivu pamoja na kubembeleza. Wasichana wote niliotumia muda{3} mrefu kuwapata, niligundua kwamba walinikubali kwasababu ya kuwaganda sana, mapenzi hayakudumu, waliniacha wakaenda. Sasa nimebadili uelekeo sitaki tena kusumbuana na mtu muda mrefu, lakini nikitafakari naona hii nayo inaweza kunigharimu. Naomba mawazo yenu, je reasonable time ya kumfatilia msichana ambaye ana +ve response ni upi? Nahis kushindwa na kukata tamaa.