Habari ya Uzima wanajamvi. Natumai wengi wetu, Mungu wetu wa Rehema ametuvusha Salama kufika mwaka 2023. Jambo la Kumshukuru sana Mungu.
Nijikite sasa kwenye Mada yetu husika wanajamvi. Kama ilivyoada kila mwanadamu huwa ana malengo yake husika ndani ya Mwaka mzima ili kujiweka juu zaidi katika maendeleo yake.
Mwaka 2023 ni mwaka ambao nimejishuhudia kabsa kwamba, miongo 3 kamili inatosha sasa kwa Kijana Mimi kuishi maisha ya Mume na Mke na kupunguza au kuacha kabisa tabia za uzinzi.
Ninamshukuru Mungu mchumba amenipatia na Hatua zote za awali zilikamilika mwishoni mwa mwaka 2022 (posa na Mahali) na Sasa kilichosalia ni Ndoa ili kusudi familia ya mke wangu mtarajiwa wanikabidhi Mke rasmi.
Ombi langu sasa, Ninaomba Ushauri wenu wa mawazo kwa wale ambao wamefanikiwa kufunga ndoa: Ni hatua gani napaswa kuzifuata sasa ili michakato yote iweze kwenda sawa? Mpaka sasa sijajua wapi naanzia na wapi namalizia!
List ya wanakamati watakaonisaidia hili swala ninayo kichwani na bila shaka hakuna atakayenigomea kwa hao wote.
Swala la kadi za harusi sijajua naliandaaje, je ni kwamba nikaripoti kanisani kwanza ili nijue muda wa harusi ndipo niandae kadi za harusi au niandae kwanza kwa utashi wangu na kuzigawa kwa watu watakaonishika mkono kwa hilo?
Najikuta nachanganyikiwa sana Tafadhali kwa mliofunga ndoa hivi karibuni na mnafahamu hatua zote mlizopitia naomba tusaidieni kimawazo ili kusudi sisi wageni tupate kunufaika katk Hili na tuje kuwasaidia wengine.
Tusaidiane ili kasherehe kawe kazuri nisije nikamuaibisha Muhaya wangu na familia yake.
NB: Ndoa kwa mipango yangu ni mwezi wa sita (6).