Msaada message za kutisha za majambazi - dar

Speculator

Member
Mar 30, 2012
56
4
Pana jamaa yangu katumiwa meseji , hajajua hao majambazi walipo, wanamwamuru kuwapa pesa kwa simu ya voda, afanyeje ili ajue walipo hao majambazi , kama pana mtu anaweza saidia kujua hili tafadhali, au ushauri wowote wa kuyatambua/ kuyakamata hayo majambazi,
 
Hakuna jambazi anaeiba kwa naama hiyo!
Hana sifa ya kuitwa jambazi, huyo ni kibaka!

Anyway turudi kwenye mada;
Ni hivi apeleke fasta hy message Polisi ingawa nao hawaaminiki!
 
Mimi ni jambazi, nitumie millioni kumi haraka sana kwa 0765000000 kabla sijakutoa uhai wako!!
 
TCRA wanakitengo kinachoshirikiana na vyombo vya usalama kudhibiti uhalifu kwa njia ya mitandao. Waone watakupa ushirikiano mzuri tuu.
 
hakuna ujambazi hapo.....hao wanafahamiana na wanachezeana.........
 
Shukran mkuu office zao ziko wapi ?

TCRA- Tanzania Communications Regulatory Authority - Wako pale upanga opposite na California Dream Casino. Jengo la kwenye kona kabisa kama unaelekea muhimbili..(Institution hii inawasomi wazuri tuu, Watakusaidia bila kinyongo. Usihofu na wapo kwa ajili ya kutumikia wewe)
 
Mwambie azifuate mweyewe huyo Jambazi, mwambie amwambie kuwa laini yake haina M-Pesa.....
 
TCRA- Tanzania Communications Regulatory Authority - Wako pale upanga opposite na California Dream Casino. Jengo la kwenye kona kabisa kama unaelekea muhimbili..(Institution hii inawasomi wazuri tuu, Watakusaidia bila kinyongo. Usihofu na wapo kwa ajili ya kutumikia wewe)
Mkuu inaelekea ulipita siku nyingi sana hapo Upanga. Walisha hama hapo muda mrefu sasa. Ofisi zao mpya ziko Mawasiliano House along Sam Nujoma.
 
Mkuu inaelekea ulipita siku nyingi sana hapo Upanga. Walisha hama hapo muda mrefu sasa. Ofisi zao mpya ziko Mawasiliano House along Sam Nujoma.

Asante kwa update Mkuu. Kwakweli ni muda kidogo, Nikirudi nitatumia msaada huu.
Je bado wanahuduma nzuri?
 
Pana jamaa yangu katumiwa meseji , hajajua hao majambazi walipo, wanamwamuru kuwapa pesa kwa simu ya voda, afanyeje ili ajue walipo hao majambazi , kama pana mtu anaweza saidia kujua hili tafadhali, au ushauri wowote wa kuyatambua/ kuyakamata hayo majambazi,

1.-Polisi walishaacha siku nyingi kushughulika Na majambazi nowadays wanajihusishaga Na mambo ya kisiasa zaidi SIO usalama wetu raia.

2:- sidhani Kama kuna namba yenye usajili wa masifuri mengi that way, huyo ni ex-gal/hub anataka kukuweka roo juu juu.

3:- kumdhuru Mtu ni mpango rahisi Kwa Mtu mwenye dhamira mbaya nawe. Wanadamu ni free electron tunajibombast anytime, so huyo ni mpuuzi anayetaka akuone unavyohara.!

4:- kila anayekimbiza siku akikimbizwa hummaliza. Wanaokutisha jua nao hutishika Kwa kishindo. Huyo Na wewe unamtisha vilevile... Unamwandikia SMS faster.. NAKUROGA KESHO..!! Au nakufahamu sana wewe mjinga..!! SMS Kama hizo halali.. Utapoteza Muda wako kwenda mbali kumbe mbuzi flan anakusumbua..

5:- but kama una muda wa mnene Basi watembelee wewe mwenyewe, nenda Polisi utapata report Na Mpelelezi, mwezesha Mpelelezi aende faster TCRA, wataita Report ya Polisi ikionyesha namba ambazo hiyo namba imetumia au Kwa SMS au kubeep. Ila mara nyingi ni wanajifanya wajanja wanatumia namba just once Na kuitupa.but rekord ya imei Ipo pale pale itaonyesha mitandao yote ambayo cm hiyo imepiga. Kisha utaenda Usalama wa polisi wa Kanda Na kungamua current location ya cm hiyo Hata Kama anatumia mtandao mwingine. Ukipiga Mguu mwenyewe Na polisi mpelelezi uliyemwajiri Kwa Muda Hata three days haziishi utamjua..
 
Pana jamaa yangu katumiwa meseji , hajajua hao majambazi walipo, wanamwamuru kuwapa pesa kwa simu ya voda, afanyeje ili ajue walipo hao majambazi , kama pana mtu anaweza saidia kujua hili tafadhali, au ushauri wowote wa kuyatambua/ kuyakamata hayo majambazi,

ajaribu kuwatumia hela zaidi ya aliyonayo, itampatia majina ya wahusika, atoe taarifa polisi ili wazifuatilie namba hizo, aende kwenye kampuni za simu achukue taarifa za namba hizo, aina ya watu inazowasiliana na namba hizo kwa majina, akipata taarifa aje aulize plan B
 
Awajibu kwamba '"mimi ni Police namba zenu ninazo,siku nikiwakamata nitawapiga""
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom