Habar zenu ndugu zangu?.Natokea wilaya ya Muleba, mkoani Kagera, naombeni msaada wa mawazo na muongozo kwa wale wanachama wa LAPF.
Nilijifungua mwaka Jana 10/8/2018 nilijaza fomu na kuweka viambatanisho vyote kudai fao la uzazi. Tarehe 5/9/2018 barua zangu zilipokelewa ofisi za LAPF mwanza maana huku hatuna ofisi.
Kinachoniuma mpaka Sasa sijalipwa hela yoyote, huku makato ya Kila mwezi yakiendelea.
Nimefatilia mpaka kutuma emails, kupiga simu n.k lakini Cha ajabu najibiwa bado nisubiri wanasubilia muongozo!!.
Nimeangaika kwenda ofisini kwa wakala wao aliyekuwepo nimekuta watu wengine wakanijibu Lapf haipo tena baada ya muungano wa mifuko kufanyika!
Nilimfatilia huyo kaka ananijibu nizidi kusubili!!!. Kinachoniuma zaidi na zaidi gharama zangu kwa maana huku hakuna ofisi zao kuprocess kila kitu mpaka miuli ya mwanasheria, na hela ya kutuma kwenye gari kuipeleka zilipo ofisi zao huko mwanza nilitoa 50,000/=!! Na hizo nilizikopa kwani sikuwa na hela ndo nimejifungua tena kwa opresheni!
Jamani jamani naombeni muongozo wa hili suala kama kuna anayejua nifanyeje na kama kuna muhusika labda ni mfanyakazi wa huo mfuko LAPF tafadhari naombeni mnisaidie nipitie wapi hadi nipatiwe haki yangu.
Nitashukuru Sana wadau.