Msaada kwa anayefahamu sheria za UK.

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
Habari wanaJF, nimeamua kutafuta msaada hapa kuhusu sheria za uhamiaji UK, kuna ndugu yangu alienda masomoni UK kama miaka 7 imepita na anafanya kazi huko, huku TZ aliacha mke na mtoto (16 years) kwa kua mke alikua muajiriwa lakini mama wa mtoto amefariki na jamaa alirudi kwa ajiri ya msiba. Baada ya mazishi wanandugu wakamuuliza kama ataondoka na mtoto jamaa anajibu sheria zinabana na kwakua ndugu wengi hawafahamu wanashindwa kuhoji. Sasa mtoto akibaki itabidi aende kijijini kwa bibi yake. Nimeamua kutafuta mawazo kuhusu hili suala. Je ni kweli sheria za UK ni ngumu kumchua mtoto kwenda kuishi nae?
AHSANTENI SANA WAKUU!
 
huyo ni mbabaishaji. mzazi anayohaki ya kumwombea mtoto wake kibali cha kuishi UK na hupewa uzito mkubwa kama baba anayo kazi inayoweza kumudu gharama za waote wawili. Labda awe hana ajira inayoeleweka...........au usikute kesha kamatwa huko na hakujielezea kuwa ana familia inamsubiria nyumbani...........
 
Dah ahsante sana mkuu na jumapili ndio kikao nitajaribu kuwasha moto
 
Wewe acha kujidanganya, sheria za UK ni ngumu, kwanza yeye mwenyewe anaishi kwa status gani huko UK? IMagine kama watangazaji wa BBC Swahili walikuwa wanasumbuliwa kipindi cha kujaza fomu kwenda na familia zao UK ndio itakuwa mbeba box?

Cha msingi kama ana uwezo amlipie shule UK na atakwenda kama mwanafunzi, zipo namna nyingi za kumsaidia huyo mtoto, lakini je mna uhakika na huyo Baba mtu maisha yake yakoje huko UK? Msidhani kila aliyepo Ulaya ni mambo safi, kuna watu wamepigika huko huko Ulaya.
 
Back
Top Bottom