Msaada karibu napata presha

Sweetlady niko hapa.

Nna mpango wa kuwakodi Majembe Auction Mart waje wanisaidie kudai deni langu.
Hahaha, usifanye hivyo tafadhal, nlpatwa na kijitatzo, ntakuPM unipe ushauri. Sitaki kumwaga mchele. Nisamehe sana babu.
 
Hahaha, usifanye hivyo tafadhal, nlpatwa na kijitatzo, ntakuPM unipe ushauri. Sitaki kumwaga mchele. Nisamehe sana babu.

Umesamehewa dhambi zako zote za juzi, jana, leo na utakazotenda kesho na kesho kutwa.....Sema AMINA.
 
Mheshimiwa, ulikosea kwenye msingi sasa hata ukiziba nyufa bado haitasaidi!
Cha kufanya chukua hatua ya kumuweka chini na hata akija juu au akikujibu majibu ya mkato demand ujue ukweli, una haki na wajibu wa kujua ukweli kuhusu mwenzako. kumbuka nyie SIO WAWILI TENA BALI NI MWILI MMOJA, SASA SIRI ZA NINI?

ndg yangu umenena vema.hata mie yalinikuta makubwa kuliko haya nikahangaika mno hadi niliposoma kitabu kiitwacho ndoa yangu, ningejua ndipo nikagundua kumbe nilianza vibaya.wanandoa wengi tunaumia kwa sababu tulianza vibbya
 
mkuu pole sana.kwanza una haki kama mume ya kusimamia kile ambacho unaona ni sahihi for the well-being of your family.nionavyo mimi kuna jamaa la kando 'linapiga' au ka-bizness kamemdatisha bi dada anaona huna ishu tena.cha kufanya,'mkazie sauti' kila unapofuatilia mambo ya chapaa.mambo ya pesa yana nafasi kubwa katika kuamua mustakabali wa familia(ndoa)yako jombaa!stop playing 'Mr. Nice Guy',dada zetu wa siku hizi wanasema it's BORING!akiendelea zingua we jikurupue tu siku moja chukua funguo za dukani na za gari lake,afu mkabidhi tiketi ya basi la kwenda kwao bila maelezo mengi.mwambie utamfuata baada miezi sita na usiruhusu maswali!mwenyewe atakaza akili nakwambia!si unajua jeuri dawa yakae ni kiburi!
 
Wana JF,Nashukuru kwa mawazo mbalimbali toka kwenu mmoja mmoja. Ni mawazo mazuri. Labda jambo la kufafanua ni kuwa tulichumbiana kwa taratibu zote. nikajitambulisha kwao na wazazi wake wakaridhia nimchukue, tukapanga kuwa katika priorities za maisha yetu la kwanza iwe ni kupiga vita umaskini na kujenga uwezo wa kumudu maisha. Hakuwa na kazi ya maana japo mimi nilikuwa na ajira ya kutosha kumtunza hata kama ni miaka 5. Lakini nikafikiria kuwa kuna leo na kesho. Inaweza tokea sipo duniani ataishije ilhali tuna mtoto. Ndipo wazo la kumfungulia biashara likaja na nikafanikisha. Sikupenda tuzae tena hadi pale naye atakapokuwa anaweza ku contribute nyumbani kwa matumizi ya kawaida tu. Na hilo nilimwambia wazi. Lengo lilikuwa kwamba hata iwapo kwa sababu yeyote sitakuwa capable kutunza nyumba basi mwenzi wangu yupo na hatutaadhirika. Hilo gari ni katika kufanya shughuli zake ziwe simple ili awe productive zaidi. Kuhusu marafiki lengo si kuwajua for that sake only bali ni kujua ni marafiki wa aina gani isiwe ni wale ambao wakiona unapiga hatua basi wanakuvuta nyuma. lakini hilo nikitaka kujua majibu yake kama huna patience unaweza kuishia segerea. Nitachambua ushauri nilioupata humu jamvini na naamini wengi wana experience na haya mambo na hamtachoka kunimegea ushauri.
 
Wewe kaa nae umwambie akweleze acha kuwa mpole itakutokea puani, marafiki si unawaona kwani huwa haum join mahala akiwa nao? hili najua hutashindwa kuwafahamu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom