Msaada: Jinsi ya kupunguza mafuta shingoni

cuchi

JF-Expert Member
Oct 1, 2012
218
74
Habari wana JF.

Mimi ni binti mwenye unene wa kawaida ila tatizo langu lipo kwenye shingo yaan ikitokea nimeongeza uzito kidogo ninakuwa na mafuta mengi shingoni kiasi cha kwamba hta nikiinamisha kichwa kidogo yale manyama chini ya kidevu yanafika kifuani.

Hii hali inanikosesha amani yaani naonekana mnene usoni kuliko hata mwili.nimejaribi kutumia bidhaa tofauti kama aloevera toner naona hamna mabadiliko.

Msaada wana jamii wenzangu.
 
Jamani umesema kwa kumaanisha mpaka nimetamani kukusaidia maana binafsi hiyo makitu siipendi pia nna rafiki yangu nae anayo
kwani ukifanya mazoezi ya shingo na kunywa maji ya moto yenye ndimu kila muda itashindikana kweli?
 
Lakini pia inawezekana una asili ya kujaa shingo fanya mazoezi ya shingo kila muda
 
Jamani umesema kwa kumaanisha mpaka nimetamani kukusaidia maana binafsi hiyo makitu siipendi pia nna rafiki yangu nae anayo
kwani ukifanya mazoezi ya shingo na kunywa maji ya moto yenye ndimu kila muda itashindikana kweli?

Nahisi unaweza hisi hii kitu inavyoninyima raha..hata sielewi nafanyaje but ntaanza ni huo utaratibu wa maji moto asbh naomba isaidie.sitaki hta kupiga picha
 
Mwelekeze hayo mazoezi ya shingo. Kwa faida ya wengine pia.

Hapa kuna namna ya kupunguza unene wa shingo kwa kuzingatia mpangilio wa chakula lakini pia wameweka na mazoezi ya shingo .pia wameweka na tahadhari namna ya kufanya hayo mazoezi kwa uangalifu jitahidi kuyapitia sio magumu .
Link ipo chini hapo sijui kama ntakuwa nimetoa msaada.
6 Ways to Get Rid of Neck Fat - wikiHow
 
Kama ndio maumbile yako chamsingi ni ujitune uwe mwembamba siku zote usinenepe kabisa ili uepukane na hiyo adha, maana wengine wanalalama mafuta yanakimbilia makalioni wengi tumboni wengine mapajani, wengine kifuani minido inakuwa mikubwa, sasa wewe ni shingoni ndio ujitahidi usiwe mnene ili uwe naamani.
 
Asante mdau...ntajitahidi sana kuhakikisha namaintain mwili wangu
 
Hapa kuna namna ya kupunguza unene wa shingo kwa kuzingatia mpangilio wa chakula lakini pia wameweka na mazoezi ya shingo .pia wameweka na tahadhari namna ya kufanya hayo mazoezi kwa uangalifu jitahidi kuyapitia sio magumu .
Link ipo chini hapo sijui kama ntakuwa nimetoa msaada.
6 Ways to Get Rid of Neck Fat - wikiHow

Asante sana sana Gemmy. Mengine nimekuwa nikiyafanya tu kumbe ni zoezi tosha na hakika sina fats katika shingo baada ya kuanza haya mazoezi ya neck turning.
 
Last edited by a moderator:
Asante sana sana Gemmy. Mengine nimekuwa nikiyafanya tu kumbe ni zoezi tosha na hakika sina fats katika shingo baada ya kuanza haya mazoezi ya neck turning.

Safi sana mkuu yaani kuna vitu vinaharibu muonekano lakini kuna vimazoezi vingine ni vidogo tuu vinaokoa hiyo hali yaani yangu inainakaribia kuwa kama ya twiga sasa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom