Msaada jamani

Danp36

JF-Expert Member
Jul 31, 2010
2,097
920
Wana jamii forum poleni na kazi za kulijenga taifa,naomba kuuliza,kuna rafiki yangu mtaani hapa anampenzi wake ambae anatarajia kutangaza uchumba.lakini huyo mwanamke kamwambia ukweli jamaa kwamba,yeye anatokea kwenye kabila wanalo practise fgm{wanakeketa},na wamemfanyia hicho kitendo tangu utotoni,je kuna matatizo gani jamaa atapata?,pia nasikia hawapati hisia kama wanawake wengie.msaada
 
Duh!Sina uhakika na ninachofikiri kama ni sahihi,ngoja waje wajuzi watakuambia!
 
Sasa kama jamaa ameambiwa ukweli na anataka kuoa wewe unataka msaada gani? I mean what specifically do you want us to advise?
 
Mbona kama amemwambia ni poa tu, hata mtu akikeketwa bado ni mtu na anaweza bado kuwa mama bora kabisa wa familia. Ni utamaduni uliopitwa na wakati na tunapaswa tuuchukie na kuupiga vita kwa nguvu zote ila haimaanishi kuwa waliopitia hiyo kitu tuwatenge, nadhani tatizo lake kubwa ni mama wakati wa kujifungua anapata shida na anaweza kuchanika zaidi na pia mama kukosa hamu ya baba. Tatizo la kujifungua waweza kuchagua upasuaji na ikawa sawa tu na tatizo la mama kukosa hamu ya tendo ni kukaa na kuzungumza nae mkaenda sawa. Asisitishe huo mpango aisee kama wanapendana
 
Sasa si ungeandika heading vizuri!! siyo unaandika msaada jamani ......ovyooo.
 
Mwambie aoe tu hawana noma, mie nilikuwa na girlfriend wangu alikuwa amekeketwa lakini sikumuoa kwa sababu dini ilikuwa ni kikwazo na wazazi wake walikataa na wakampeleka nje ya nchi kusoma ili kututenganisha.
 
Mwambie aoe tu hawana noma, mie nilikuwa na girlfriend wangu alikuwa amekeketwa lakini sikumuoa kwa sababu dini ilikuwa ni kikwazo na wazazi wake walikataa na wakampeleka nje ya nchi kusoma ili kututenganisha.
wewe nae......................... Wenzio tunazika, wewe unatongoza.
 
Hua nasikia wanawake waliofanyiwa fgm hua hawaenjoy tendo la ndoa kama wengine na pia wakati wa kujifungua wanapoteza damu nyingi sana!
 
Acha longo longo dogo. Kwani ukisema ukweli kwamba wewe ndio unataka kuvuta hicho kifaa kuna ubaya gani?.
Muda wote ulipokuwa unakula mzigo mbona hukugundua kama mashine ilishachongwa. Leo amekuambia mwenyewe hali halisi unataka kugairi. utoto huo!
 
Mwanamke aliyekeketwa ana enjoy sex kama wanawake wengine isipokuwa tu uwezekano wa ku-climax huwa ni mdogo sana,ila kadri mnavyoishi pamoja utakuja kugundua kuwa kuna positions ambazo mkizitumia (ukifanya mautundu flani) ana-climax bila matatizo yoyote,pia swala la kuchanika wakati wa kujifungua inategemea na alivyokeketwa kwani wengine wanajifungua bila hata ya kuchanika.
 
Back
Top Bottom